Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  29 Ramadan 1442 Na: 1442/11 H
M.  Jumanne, 11 Mei 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tunawapa Salamu za Eid ul-Fitr

 Harakati ya Hizb ut-Tahrir/ Kenya ingependa kutuma salaam zake za dhati kwa Waislamu wa humu nchini na ulimwengu kwa ujumla kwa munasaba wa siku kuu ya Eid ul-Fitri. Idi hii inawadia huku utawala wa kikatili wa umbo la Kiyahudi unafanya mashambulizi ya anga kwa Mji wa uliozingirwa wa Ghaza ambayo hada sasa tayari watu 21 wakiwemo watoto wameuwawa! Cha kuhuzunisha ni kwamba ukatili huu unaotekelezwa na jeshi la kiyahudi hadi sasa haujachemsha damu wala mioyo au mishipa ya viongozi wa Kiislamu na majeshi yao!. Viongozi hawa wa Kiislamu ambao kiuhalisia ni maruwaibidhwa (Viongozi duni wasomudu kusimamia mambo ya watu) kwa hakika wamekua siku hadi siku wakiunga mkono mipango miovu ya mayahudi kama mpango wa ujengaji wa mahusiano na dola hii ya kibaguzi ya Kizayuni.

Kwa yakini tunafahamu kwamba kadhia ya Palestina haitotatuliwa kwa kufanywa mikutano ya dharura na baraza kuu la usalama la umoja wa mataifa,au maneno matupu yatokayo kwa viongozi wa Riyadh, Tehran, Islamabad am Istanbul kwani yote haya ni yenye kuunga mkono ukaliaji wa kimabavu wa Filastin ardhi tukufu ya Isra’ wal Miiraj. Suala la Palestina linahitaji Khilafah- serikali itakayoweza kupeleka  jeshi la Kiislamu kuondosha utawala dhalimu na kukomboa sio tu Palestina bali biladi zote za Kiislamu na kuweka chini ya bendera ya Laa ilaha ila llah  Muhammada Rusul-llah

Tunajua kwa yakini Inshallah nusra iko karibu sana. Kwa siku tukufu hii ya Eid, tunamuomba MwenyeziMungu aipe Hizb ut-Tahrir ushindi/nusra chini ya amiri wake Mwanachuoni mkubwa Ataa bin Khalil Abu Rashta wa kuisimamisha tena Khilafah kwa mfumo wa unabii ambayo kiukweli ndio itakayolinda na kuhifadhi Waislamu na walimwengu wote kwa ujumla kutokana na majanga ya ulimwengu.

(لِلَّهِ الأمْرُ مِنْ قَبْلُ وَمِنْ بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ بِنَصْرِ اللَّهِ)

Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. [Ar-Rum: 4]

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari  Hizb ut Tahrir in Kenya

#AqsaCallsArmies
#Aqsa_calls_armies

الأقصى_يستصرخ_الجيوش#

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu