Afisi ya Habari
Kenya
H. 7 Muharram 1438 | Na: 1438/01 |
M. Jumamosi, 08 Oktoba 2016 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
﴾فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّى يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ)
“Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa,”
Msanii maarufu wa Marekani Chris Brown yuko katika ziara ya Jiji la Mwambao wa Pwani la Mombasa Kenya kufanya tamasha la muziki katika Bustani ya Mama Ngina. Msanii huyu si maarufu tu kwa wapenzi wa muziki bali pia katika upande wa ujambazi. Mwishoni mwa Agosti 2016, alikamatwa nyumbani kwake jijini Los Angeles kwa madai ya kumuelekezea mwanamke bunduki. Suluki yake chafu inadhihirika wakati alipoivunja vunja simu ya rununu ya mmoja wa mashabiki alipojaribu kupiga picha naye jijini Mombasa. Kuhusiana na hili, sisi Hizb ut Tahrir / Kenya tunapinga vikali tamasha hili na twapenda kuangazia yafuatayo:
Hafla hii ya uharibifu ni utovu wa heshima kwa Waislamu wa Mombasa na Kenya kwa jumla kutokana na kuwa Mombasa inachukuliwa kuwa kitovu cha Uislamu Kenya. Kuandaa hafla kama hii ambayo sasa imekuwa ni ada imeigeuza Mombasa kuwa jukwaa la kumuasi Mwenyezi Mungu (swt) waziwazi!
Ni aibu kuwaona wale wanaoitwa viongozi wa Waislamu kunyamaza kimya kama cha mtu aliyekufa kana kwamba Mwenyezi Mungu anaridhishwa na yale yanayotokea Mombasa. Kwa yakini tungependa kuwakumbusha kuwa Mwenyezi Mungu atawahisabu kwa uongozi wao. Kuhusu Wanachuoni Waislamu ambao ndio warithi wa Mitume watukufu wa Mwenyezi Mungu (amani iwe juu yao), tungependa kuwakumbusha kubeba jukumu lao kubwa la kupinga uovu wowote bila ya uoga wala upendeleo. Ingawa tunajua kwamba Wanachuoni wengi kwa kawaida huamua kunyamaza kimya kutokana na manufaa duni ya kiulimwengu wanayoyapata kutoka kwa matajiri na sio kwa sababu hawana habari ya munkar huu.
Tunasema kufanya matamasha kama haya ya uharibifu chini ya bango la kuimarisha utalii na kutia faida imeonyesha jinsi gani nidhamu ya Kirasilimali inavyo vitazama vitendo na vitu. Ni kutokana na vipimo hivi yaani vitendo kutazamwa kuwa ni vizuri na vyenye maslahi kwa msingi wa faida, wanademokrasia wa kirasilimali hufanya hafla ovu kama hizi bila ya kujali athari mbaya ya muda mfupi au muda mrefu juu ya kizazi chetu. Ni wangapi katika vijana wetu wameshambuliwa na kuharibiwa akhlaqi zao na hao wanaoitwa kuwa ni watalii? Tunaendelea kusema kuwa fikra ya uhuru wa kibinafsi inayolinganiwa na wanademokrasia wa kirasilimali imewaweka mbali vijana wetu na maadili ya Kiislamu hivyo basi kuwatia katika 'burudani' angamivu.
Uislamu umetufunza vipimo vya kweli vya maisha kuwa ni Halali na Haramu huku lengo pekee la vitendo vya mwanadamu likiwa ni kupata radhi za Mwenyezi Mungu na sio manufaa ya kimada. Kutokana na haya, Uislamu umetufunza kuwa burudani na tamasha hayapaswi kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na kwamba Siku ya Kiyama, wanadamu watahisabiwa kwa vitendo vyao katika ulimwengu huu. Ni katika msingi huu ambapo Khilafah itapiga marufuku matamasha yote ambayo yatakiuka mafunzo ya Kiislamu.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir in Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |