Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  23 Shawwal 1437 Na: 1437/02 H
M.  Alhamisi, 28 Julai 2016

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Fikra za Kijambazi za Usekula Ndio Chanzo Kikuu cha Moto Shuleni

Kufuatia msusuru wa matukio ya kuchomwa shule na wanafunzi ambapo sasa imefikia shule 105, Hizb ut Tahrir / Kenya ingependa kuangazia yafuatayo:

Ujambazi huu unaoendelea umesababisha pakubwa kupotea kwa mali na majeruhi unapaswa kukemewa vikali na kukomeshwa mara moja. Inasikitisha kuwa serikali imekuwa ikijivuta katika kuzuia uovu kama huu ilhali ni jukumu lake kutatua tatizo hili na mengine mengi yanayo ikumba jamii.

Kwa yakini sisi hatushangazwi na moto huu wa mara kwa mara shuleni kutokana na sababu mbili kuu:

a) Si ajabu kushuhudia vitendo hivi vya kihalifu katika mujtama ambao umeikumbatia fikra ovu inayo chipuza kutokana na itikadi ya kihuria ya kisekula. Kwa yakini, madai kuwa baadhi ya watu wako nyuma ya kuchomwa kwa shule yana asilimia kubwa ya ukweli. Hii ni kwa sababu usekula huu huuweka mbali umma kutokana na hisia ya kumcha Muumba Mtukufu badala yake huwasukuma kuwa na matakwa huru yaani kufanya kitendo chochote kwa mujibu wa matamanio yake. Hivyo basi katika mujtama kama huo si ajabu kuona wanafunzi wakifanya vitendo vichafu kama ulevi, vitendo vya ngono na maovu mengine mengi.

b)  Katika mfumo huu wa kirasilimali, elimu imechochea matatizo mengi zaidi badala ya kuyatatua na fahamu mbaya zaidi ni kufungamanisha elimu na ajira. Hili limewasukuma wanafunzi kutafuta elimu kama njia ya kupata ajira na sio kuwa wanafikra. Vyeti ghushi na udanganyifu wa mitihani ni miongoni tu mwa matatizo machache yanayo ikumba elimu ya kisekula. Maafisa wa elimu wamekuwa wakipewa hongo na wazazi ili kuvujisha makaratasi ya mtihani. Hili limefanywa mchana peupe na kwa ridhaa ya walimu wakuu wa shule. Hivi ndivyo namna urasilimali unavyo zalisha na kukuza mgogoro. Uhalisia wa elimu ni chombo tu cha kinadharia ambacho kiko mbali na maisha halisi.

Kinyume na Uislamu – mfumo mpana uliojengwa juu ya itikadi imara inayo kinaisha akili ya kumuamini Muumba Mtukufu Mwenyezi Mungu (swt). Itikadi ambayo inawataka wanadamu kuendesha mambo yao kwa mujibu wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Na kwamba wanadamu wanapaswa kutegemeza vitendo vyao kwa mujibu wa matakwa ya Mwenyezi Mungu. Ni juu ya msingi huu ndio sera ya elimu inapaswa kujengwa na yenye lengo la kuzalisha wanafikra wakubwa ambao maisha yao yataendeshwa pekee kwa nidhamu hii ya kiwahyi.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu