Afisi ya Habari
Kenya
H. 9 Dhu al-Hijjah 1437 | Na: 1437/07 H |
M. Jumapili, 11 Septemba 2016 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tunawapa Salamu za Idd al-Adha
Kwa furaha kubwa kutoka ndani ya nyoyo zetu, sisi katika Hizb ut Tahrir Kenya tungependa kutoa salamu zetu za dhati za Idd al-Adha iliyo barikiwa kwa Waislamu nchini Kenya na ulimwengu mzima kwa jumla. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) ayakubali matendo yetu mema na atuongoze hadi Idd ya mwakani tukiwa chini ya kivuli cha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itaviunganisha vijidola vyote vya Waislamu ulimwenguni chini ya bendera ya 'Laa ilaha illah Allah Muhammad Rasul Allah'.
Idd hii iliyo barikiwa inajiri huku Mamlaka za Kenya zimeanzisha mkakati mpya wa kupigana na Uislamu chini ya pazia ya kupambana na misimamo mikali. Tuna yakini kuwa hii ni kampeni inayo sukumwa na Magharibi katika kujaribu kuubadilisha Uislamu na fikra zake. Magharibi inataka Itikadi (Aqeedah) ya Kiislamu na fikra zake zitazamwe kwa kejeli na shauku. Fauka ya hayo mkakati huu si chochote ila ni kupanua hofu inayo ziruhusu serikali kuchukua hatua zinazo karibia kuwa za dola ya kipolisi dhidi ya Waislamu.
Idd inajiri huku kaka na dada zetu nchini Syria, Afghanistan, Iraq na Yemen wakimiminiwa mabomu makali na serikali za Kimagharibi na vibaraka wao. Mauaji haya yanayo tekelezwa na serikali za Kimagharibi na vibaraka wao katika Waislamu bado hayaja chemsha nyoyo wala mishipa ya majeshi ya Waislamu!
Tunaikumbusha jamii ya Waislamu wajibu wao mkubwa wa kubeba ujumbe wa Uislamu kupitia mchakato wa kifikra na kisiasa kuonyesha kuwa ni mfumo kamili kwa wanadamu ulio na suluhisho katika nyanja za kiroho, kiuchumi, kijamii na kisiasa. Tunawasihi zaidi Waislamu kuchukua fursa hii nzuri kuwaalika Waislamu na wasiokuwa Waislamu katika mazungumzo ili kuwaelimisha juu ya uhalisia wa kweli wa Uislamu kama ulivyo teremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Ili waweze kutofautisha kati ya Uislamu na uvumi wa Wamagharibi wanaodai kuwa Uislamu ni ugaidi na kufahamu kuwa nyakati ngumu wanazo kumbana nazo maishani ni dalili ya kufeli kwa Urasilimali na mfumo wa kikoloni.
Tunajua kwa yakini kuwa wakati wa Nusra uko karibu sana inshaAllah. Tuna imani kuwa kitendo kitukufu cha ubebaji ulinganizi (da'wah) kitazaa natija kubwa ambayo ni kuleta mabadiliko ya kimsingi ya kusimamisha Khilafah ya Uongofu ya pili kwa njia ya Utume katika ulimwengu wa Waislamu. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayo ng'oa dhulma zote dhidi ya Waislamu kupitia kuziondoa nidhamu za kikafiri za Kimagharibi na kuzibadilisha kwa nidhamu za Mwenyezi Mungu na siku hiyo, waumini watafurahi kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt).
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |