Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  29 Ramadan 1437 Na: 1437/04 H
M.  Jumatatu, 04 Julai 2016

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mateso na Ukatili Ndio Silaha Pekee za Kawaida za Warasilimali

Harakati ya Kiislamu ya Hizb ut Tahrir inakemea vikali mauaji ya kikatili ya Wakili Willie Kimani na watu wengine wawili akiwemo mteja wake Josephat Mwenda. Hiki ni kitendo cha kinyama hususan baada ya miili hiyo mitatu kupatikana imetupwa katika mto huku macho ya mmoja ya miili hiyo yakiwa yamenyofolewa. Inasikitisha kupata ripoti za habari kuwa polisi wa Utawala wanahusishwa na mauaji hayo!

Ukatili huu ni sehemu tu ya kesi kubwa za mauaji zinazo ikabili idara ya usalama. Inashtua kuona majibu ya kikatili ya polisi kwa waandamanaji ambao baadhi yao hata waliuawa kwa kupigwa risasi! Ukweli ni kuwa vitendo hivi vya kinyama vinazidi kuthibitisha kuwa kikosi cha polisi sio watekelezaji sheria bali ni wavunjaji sheria ambao sasa wamegeuka kuwa genge la wauaji. Makala maalumu ya habari ya Aljazeera ya mwaka jana yalifichua mauaji yasiyo julikana ya raia kupitia polisi. Ufichuzi huo ulionyesha picha fiche za maafisa wa usalama wakiungama kuwauwa washukiwa wa ugaidi. Jamii ya Waislamu imeibua wasiwasi wake kuhusiana na kupotezwa kusiko eleweka kwa vijana na polisi wamekuwa ndio washukiwa wakubwa wa maovu haya. La kusikitisha hakuna hatua yoyote kali na muhimu iliyo chukuliwa na Serikali dhidi ya maafisa hao wakorofi wa polisi.      

Kwa kuwa tunaishi chini ya mfumo batili wa kirasilimali ambao silaha yake ya kawaida ni kutumia ukatili dhidi ya raia basi bila shaka usalama wetu na maisha yetu yamo hatarini. Chini ya mfumo huu, maajenti wa usalama si kazi yao kumlinda mtu wa kawaida bali kulinda maslahi ya kipote cha watu wachache wenye ushawishi ambao hawana utu wa aina yoyote kwani wanauamini pakubwa msemo: Mwenye Nguvu Mpishe. Yeyote anaye jaribu kufichua maovu ya tabaka la viongozi awe wakili au mwanahabari basi maisha yake yako hatarini. 

Ni chini ya Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume pekee ambayo karibuni itasimama katika mojawapo ya nchi za Waislamu yenye nguvu ambapo majeshi ya polisi yatajitolea kikamilifu katika kudumisha sheria na utulivu. Khilafah ya Uongofu itakuwa na mpangilio mzuri zaidi wa usalama ambao utadhamini na kulinda maisha na mali za raia wote bila ya kujali rangi, kabila au cheo.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu