Afisi ya Habari
Kenya
H. 1 Shawwal 1437 | Na: 1437/05 H |
M. Jumatano, 06 Julai 2016 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ziara ya Netanyahu ni ya Maangamivu Ambayo Haistahiki Kufurahikiwa wala Makaribisho: Ni Wewe na Dola Yako Ndio Munao Nuka Harufu ya Damu Zisizo na Hatia za Watu Wasio na Ulinzi Wowote
Waziri Mkuu wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, kwa sasa yuko katika ziara rasmi ya nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika. Ziara yake ilianzia nchini Uganda, ikifuatiwa na Kenya, Jumanne 04 Julai 2016. Kisha kuelekea Rwanda, kabla ya hatimaye kuzuri Uhabeshi. Hii ikiwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi wa Kizayuni barani Afrika tangu ziara ya Yitzhak Rabin, waziri mkuu wa tano wa Kizayuni kuzuru Moroko mnamo 1994. Netanyahu ameiita ziara hii kipima chachu kwa "Israel kurudi kwa kishindo barani Afrika."
Mtu huyu asiye na aibu anazunguka Afrika akidai kuhubiri amani, vita dhidi ya ugaidi na kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya utawala wake na nchi za Kiafrika katika juhudi za kuimarisha sekta ya ukulima na afya.
Hakika, Hizb ut Tahrir Kenya, ingependa kuifafanua ziara hii kupitia nukta muhimu zifuatazo:
Kwanza: Ni ukweli uso kifani kuwa chuki mbaya dhidi ya uhalifu muovu uliotekelezwa na utawala wa Kizayuni ungali unaendelea kutawala anga kote duniani ikiwemo Afrika. Hivyo basi, lengo pekee la ziara yake ni kuitongoza Afrika kuendelea kuunga mkono utawala huu wa kidhalimu. Ukizingatia kuwa nchi nyingi za Kiafrika kwa haraka zilikata mahusiano ya kidiplomasia na nchi hii ya kikatili kufuatia vita vya 1973, ambapo Misri ikishirikiana na Syria ilipigana vikali dhidi ya nchi hiyo. Inasikitisha kutambua kuwa bara lote la Afrika lingali linatawaliwa na viongozi duni wasioweza kusimama imara dhidi ya shinikizo la kigeni la kisiasa, kwa sababu ingali chini ya minyororo miovu ya ukoloni mambo leo na kihakika bado haiko huru. Natija yake kuifanya Afrika kuwa kitoweo rahisi cha njama ya wakoloni na vibaraka wao.
Pili: Hakika Netanyahu ni mtu asiye na aibu ambaye hukasira kwa haraka na hutenda kwa mujibu wa matamanio yake. Yeye ni nani wa kujidai kuhubiri amani na utulivu, ilhali yeye mwenyewe ni alama ya kudumu ya ghasia? Netanyahu hastahili muda wa kuzungumzia mahubiri na utulivu, kwa sababu chini ya watu wake wa dini wa Kimarekani yeye binafsi ameongoza uvamizi dhidi ya kambi ya PLO katika oparesheni inayojulikana kama Oparesheni ya Moto. Je, Netanyahu anadhani kuwa ulimwengu umesahau vitendo hivyo viovu vilivyo tekelezwa na mikono yake ilyojaa damu katika Vita vya Karamah mnamo 1968? Je, muuaji huyu katili wa watoto, wanawake na wazee anadhani kuwa hakuna ajuaye kuhusu uhaini wa enzi yake yeye mwenyewe katika ukiukaji wa ile inayoitwa mikataba ya amani? Kwa hakika huyu katili hastahili makaribisho yoyote. Anapo zungumzia amani na Wapalestina, anacho maanisha ni kuwa wanajeshi wake katili waendelee kumwaga damu ya Wapalestina wasio na hatia pasi na hofu yoyote ya kuhisabiwa au kulipizwa na walio dhulumiwa.
Tatu: Sasa ni dhahiri kama sauti ya kengele kuwa vita dhidi ya ugaidi ni kadhia ya uhai na kifo kwa Wamagharibi ambao ndio watungaji wa maana ya ugaidi na magaidi. Vilevile ni dhahiri shahiri kuwa nchi za Kiafrika zinatumiwa kupigana vita hivi, ambavyo kihakika, si chengine ila ni vita dhidi ya Uislamu. Ni wajibu kwa bara la Afrika kutambua kuwa wakoloni wa Kimagharibi wamebuni vita dhidi ya ugaidi kama ala madhubuti na rahisi ili kuwawezesha kuiba rasilimali za nchi za Kiafrika ikiwemo Kenya. Inajulikana vyema kuwa taasisi yake ya ujasusi Mossad hushirikiana na nchi za Kiafrika ikiwemo Kenya katika mauaji katili ya Waislamu nje ya sheria chini ya kisingizio cha kupambana na ugaidi. Ni utawala huu huu wa Kizayuni ndio uliotekeleza ugaidi mbaya zaidi ulimwenguni pindi ulipowafurusha Wapalestina wasio na hatia kutoka katika ardhi yao na kuwasha moto makaazi yao yanayo kadiriwa kuwa zaidi ya 700,000 katika kiu ya kuasisi umbile la Kizayuni. Ingawa kitendo hiki cha kinyama kamwe hakikuitwa ugaidi. Hii inatoa taswira wazi kuwa ufafanuzi wa upi ni ugaidi uko kwa Marekani pekee: mdhamini mkubwa wa umbile la Kiyahudi. Yote haya, ilhali Netanyahu anasubutu kuzuru Rwanda na kutoa mahubiri makali kuhusu mauaji ya halaiki ya 1994. Ikiwa ugaidi kweli upo, basi Mayahudi pamoja na mlezi wao mpendwa na wa dhati Amerika, wanapaswa kushika bendera kati orodha ya magaidi.
Nne: Ni aibu isyio kifani kwa viongozi wa Kiafrika kuendelea kuonekana wakitegemea misaada ya nje katika juhudi za kukidhi matibabu, elimu, usafiri nk ya watu wao wenyewe. Mahusiano ya kibiashara kati ya Mayahudi na Afrika ni njia ya kuyaruhusu mashirika ya kiserikali ya kirasilimali ili kuendelea na utumwa wao wa kiuchumi barani Afrika ambalo linaendelea kuporwa na kudhulumiwa kiuchumi si kwa sababu nyingine ila maamuzi yake ya kimakosa ya kuukumbatia mfumo mlafi wa kirasilimali. Bara hili kamwe haliwezi kuokolewa kutokana na mzigo wa kiuchumi kupitia kutegemea mikopo ya kiuchumi pekee ambayo huleta pamoja nayo riba kubwa mno.
Tano: Ni wazi kuwa kilichomleta muuaji huyu katili si chengine isipokuwa ni kujaribu kuficha kucha zake za urasilimali zinazo endelea kukoloni ulimwengu kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ni wazi ziara hii imejiri kama natija ya baadhi ya maelekezo kutoka kwa wakubwa wa Kimarekani ambao ni wafuasi sugu wa umbile la mauaji ya kinyama la Kiyahudi. Dola pekee ambayo inaweza kukomesha peupe mauaji ya Mayahudi dhidi ya viumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu wasio na hatia ni Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume; ina nguvu ya kumaliza kiburi, fahari na mapendeleo ya Mayahudi. Sifa ambazo zimepelekea tabia yao ya kuchukiza.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |