Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afrika Mashariki

H.  28 Jumada I 1436 Na: 1436/10 H
M.  Alhamisi, 19 Machi 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ufisadi: Saratani Nyingine Ndani ya Mujtama wa Kirasilimali Ambayo Haiwezi Kutibiwa Kupitia Kuondoa Dalili Zake!

Mwenyekiti wa Kamati ya Uhasibu wa Umma (PAC) Ababu Namwamba anatuhumiwa pamoja na baadhi ya wanachama wake kwa kashfa ya ufisadi. Anatuhumiwa juu ya madai ya kupewa hongo na Katibu Mkuu wa Ulinzi ili kugeuza ripoti kufuatia uchunguzi wa Sh. bilioni 2.9 zilizoingizwa katika akaunti za siri. Sakata hii ya PAC imesababisha mihemko miongoni mwa wabunge hususan baada ya Namwamba kukiri kuwa ufisadi ndio sare za kiongozi wa Kenya. Na mabalozi wa Amerika, Uingereza na Uswizi wameisihi Serikali ya Kenya kufuatilia na kuyauwa mazimwi ya ufisadi. Kuhusiana na hili, Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki ingependa kutaja yafuatayo:  

Kwanza: Ufisadi umeenea sana nchini na haujazikumba taasisi za umma pekee bali pia za kibinafsi. Kupitia kashfa kubwa za ufisadi kama vile 'kashfa ya kuku' maarufu ya Tume Huru ya Muda ya Uchaguzi na Mipaka (IIEBC), Anglo Leasing na Goldenberg na nyingi nyingine, Mabilioni ya pesa za umma yameishia matumboni mwa wanasiasa. Kwa hakika hii ni khiyana wazi na dhulma kwa zile zinazoitwa mamlaka zenye kushikilia nyadhifa za umma kudai kuwakilisha maslahi ya umma, badala ya kufanya kazi kuimarisha kiwango cha maisha ya raia; wao wanashindania kwa nguvu juu ya ufujaji wa pesa za umma. Cha kusikitisha ni kuwa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya yeyote kati yao wala kushtakiwa na baya zaidi ni kashfa hizi hatimaye hugeuzwa kuwa sarakasi ya kisiasa pekee. Hii ni mojawapo ya fedheha na urongo wa nidhamu ya kisiasa ya Kimagharibi ya Demokrasia ambayo inadai kuwa bunge huwakilisha na kulinda matakwa ya Taifa huku uhalisia ukiwa ni jukwaa la 'Watu Muhimu Mno' kufikia wizi wao wa mali ya umma.

Pili: kuhusu kelele zinazopigwa na mabalozi wa Kimagharibi kuisihi Kenya kuwasaka washukiwa wote wakuu wa ufisadi, hiyo ni kuwakejeli tu Wakenya wasiojua lolote. Nchi za Kimagharibi zimekumbwa na kashfa kubwa mno na hutumia ubepari wao wa kisiasa na vitisho dhidi ya zile zinazoitwa nchi za ulimwengu wa tatu kuzilazimisha kutia saini mikataba ya muda mrefu na kampuni zao ili kuendelea kufuja rasilimali zetu. Hali hii imesababisha kuenea kwa umasikini mbaya ulimwenguni na hususan barani Afrika. Na hakika huu ni ufisadi mkubwa mno ambapo ikiwa wao ni wasafi wangekuwa washaung'oa!

Tatu: Tume na taasisi nyingi zilizoundwa kupigana na ufisadi zimefeli vibaya mno kutatua janga hili, badala ya kupambana na tatizo la ufisadi; zinaishia kuzama ndani ya ufisadi. Hili liko wazi kabisa. Kwa mfano mbali na kuundwa na kubadilishwa majina ya tume na taasisi hizi, kadhia ya ufisadi ingali inaendelea na inaenea kwa kasi mno.

Sababu pekee ya kufeli kwao ikiwa ni kuwa, badala ya kutafiti na kutatua kiini cha tatizo hili, wao wanayapa mgongo matokeo. Dhati ya ufisadi nchini Kenya na, ulimwengu mzima kwa jumla, inachipuza kutokamana na uhadaifu wa kuukumbatia mfumo wa kimakosa wa kikoloni: demokrasia ya urasilimali ambao umejaa ushibishaji wa kimada kama kipimo pekee cha maisha. Kipimo hiki, huwachochea watu wakiwemo viongozi kuathirika na ulafi wa kulimbikiza mali kupitia njia yoyote ile bila ya kujali ikiwa ni sahihi au ya kimakosa. Hivyo basi si ajabu kuwaona viongozi wa kirasilimali wakizama ndani ya wizi, rushwa, ufisadi na ufujaji. Hili laonyesha kuwa uongozi katika urasilimali ni njia tu ya kulimbikiza mali na sio kutumikia watu.   

Nne: Kwa kuwa chanzo cha tatizo hili ni demokrasia urasilimali, suluhisho halisi na la kihakika liko katika kuachana na mfumo huu muovu pekee. Na kuubadilisha kwa mfumo adilifu ambao si mwingine ila ni Uislamu. Hapo chini ni mukhtasari wa namna mfumo wa Kiislamu unapambana vikali na ufisadi. Uislamu unawalaani wale wote wanaojihusisha na rushwa na ufisadi.

• Jukumu na kazi ya kupigana na ufisadi limegatuliwa kwa kila mtu na sio tu watu au tume fulani pekee.

• Katika Uislamu, uongozi ni amana ambayo kwayo wale walio kabidhiwa amana hii watahesabiwa Siku ya Mwisho.

• Uislamu unamtaka kiongozi kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote anayejihusisha na ufisadi bila la kujali hadhi yao katika mujtama.

Kupitia hatua hizi, Uislamu kwa karne kumi na tatu ambapo ulitawala nusu ya ulimwengu, kesi za ufisadi zilikuwa nadra kama kulikuweko na yoyote. Vilevile, endapo Khilafah itasimamishwa tena, janga la ufisadi na maovu mengineyo yataangamizwa.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afrika Mashariki
Address & Website
Tel: +254 717 606 667 / +254 737 606 667
www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail:  abuhusna84@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu