Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afrika Mashariki

H.  19 Jumada I 1436 Na: 1436/09 H
M.  Jumanne, 10 Machi 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mkakati wa Amerika Kujiimarisha Ndani ya Afrika Mashariki

Amerika chini ya majeshi yake maalumu barani Afrika yaani United States Army Africa (USARAF) hivi majuzi imeanzisha usimamizi maalumu wa kijeshi katika mji wa Jinja ulio mashariki mwa jiji kuu la Uganda, Kampala. Zoezi hilo lililopewa jina "ANGAMIZA UGAIDI 2015" lin jumuisha WANAJESHI WA MAJINI wa Amerika, vikosi vya Uganda, Tanzania, Burundi, Uholanzi na Rwanda. Huku Rwanda pekee ikichangia wanajeshi 300.  

Amerika inadai kuwa lengo kuu la zoezi hilo ni kuvitayarisha kimikakati vikosi hivyo ili kuviwezesha kuwa imara katika kutekeleza misheni za amani, ili kuzilinda serikali za kidemokrasia pamoja na kupambana na tishio la ugaidi.

Kidhati, zoezi hilo si chochote ila ni njama ya Amerika inayolenga kuendeleza unyanyasaji wa Waislamu na kuupiga vita Uislamu kama mfumo: katika jaribio la kujiimarisha ndani ya eneo la Afrika Mashariki. Eneo ambalo mwanzoni liliwahi kuwa ngome ya Uingereza; dola nyingine ya kikoloni.

Ama kuhusu malengo makuu matatu ya zoezi hilo kama yalivyotajwa na Amerika:

1. Kuhifadhi amani.

2. Kudumisha demokrasia na

3. Kupambana na ugaidi, Amerika ni lazima ijue haiwezi tena kumhadaa kila mtu ili ijiokoe yenyewe!

Amerika inatumia mwito wa vita dhidi ya ugaidi, ili kuhalalisha maovu yake dhidi ya Waislamu na Uislamu, kwani ndicho kikwazo cha mfumo wao wa kirasilimali. Wanajaribu kwa uwezo wao wote kuusitisha Uislamu kutokana na kurudi katika uwanja wa kisiasa wa kiulimwengu kwa hofu kuwa itauangamiza mfumo wa kirasilimali, hivyo basi kuwakomboa Waislamu na wasiokuwa Waislamu hali kadhalika kutokana na minyororo iliyojaa damu ya mfumo huo katili.

Inatumia pazia ovu ya kigaidi ili kusababisha ghasia na mizozo katika nchi fulani kama Kenya, kuharibu mshikamano wa kijamii katika mujtama. Juu ya hayo, inatumia mbinu ile ile ya kuwadhibiti wapinzani wa maendeleo yake ya kibepari. Sawia na ilivyofanya nchini Zanzibar, kuwabandika vibandiko vya ugaidi dhidi ya wale wanaotaka mamlaka kamili ya Zanzibar, kitu ambacho kwa sasa kiko dhidi ya sera ya Amerika.

Ama kadhia ya kuhifadhi amani na kuzilinda serikali za kidemokrasia. Lengo ni kuzilinda serikali hizo zinazotii kwa unyenyekevu amri za Amerika na kuzidhibiti nchi nyingine zinazosimama kama tishio katika eneo hili. Uwepo wa rasilimali nyingi asili, hususan mafuta, gesi na madini mengine, ndio sababu ya Amerika kuja na hatua hizi ili kuhakikisha ulinzi wa rasilimali hizi asili na kuwapa usalama washirika wake ambao wako tayari kurahisisha malengo hayo ya kibepari.

Amerika haina chochote cha kuwapa wanadamu, sio tu Afrika pekee bali kwingine kote. Kidhati, ndio sababu ya utovu wa amani na utulivu. Ulimwengu mzima una tamani dola itakayofuata mfumo halisi wa Kiislamu katika jaribio la kukombolewa kutokana na minyororo ya Amerika pamoja na unyanyasaji wa nchi nyingine za kirasilimali.

Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afrika Mashariki
Address & Website
Tel: +254 717 606 667 / +254 737 606 667
www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail:  abuhusna84@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu