Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afrika Mashariki

H.  5 Jumada I 1436 Na: 1436/08 H
M.  Jumanne, 24 Februari 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Nadharia ya Kimakosa ya Uchumi wa Kirasilimali Ndicho Chanzo cha Umasikini Nchini Kenya na Ulimwengu Mzima kwa Ujumla

Kenya imeorodheshwa nchi ya sita masikini zaidi barani humu. Matokeo kamili yanapatikana ndani ya ripoti tegemewa ya Taasisi ya Masomo ya Usalama (ISS). ISS imegundua kuwa Wakenya 18.4 milioni wanaishi katika umasikini zaidi. Kuhusiana na hili, sisi Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki tungependa kufafanua yafuatayo: 

Hizi sio takwimu halisi bali ni za wastani tu, ukweli ni kwamba nusu ya wakaazi wa Kenya wanaishi katika umasikini mbaya mno. Maelezo kutoka kwa baadhi ya mashirika ya kimataifa kama vile UNICEF yanasema kuwa asilimia 46 ya Wakenya wanaishi chini ya msitari wa umasikini. Cha kufedhehesha zaidi, huku takwimu hizi zikitolewa, Kenya ingali inajifakhiri kuwa uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki na miongoni mwa nchi kumi za kwanza zenye uchumi wa juu Afrika. Ni wazi kuwa matatizo ya umasikini nchini yanasalia kuwa saratani. Hii ni ishara ya kushindwa kikamilifu kwa serikali iliyopo kama vile serikali zilizo tangulia katika kumaliza tatizo hili

Chanzo kikuu cha kushindwa kwa Serikali kukabiliana na tatizo hili ni kujifunga kwake na falsafa ya kimakosa ya uchumi wa kirasilimali. Ile inayoitwa nadharia ya udondoshaji chini au mkono usioonekana inayodai kuwa tatizo la kiuchumi hutatuliwa kupitia uzalishaji wa rasilimali na sio ugavi. Nadharia hii inadai zaidi kuwa kupitia uzalishaji ndio utakao wawezesha watu kushibisha mahitaji yao. Hii ndio sababu katika nchi nyingi za kirasilimali ambazo ni tajiri katika rasilimali asili raia wake wengi wangali ni masikini. Warasilimali hupima mafanikio ya kiuchumi ya nchi kwa msingi wa ongezeko la uzalishaji yaani utajiri jumla wa nchi (GDP) na sio utajiri wa mtu binafsi. Kwa upande mwingine, tabaka la wanasiasa wa kirasilimali ndio wafisadi wakubwa hivyo hawawezi kutatua tatizo la umasikini. Wao hukusanya mali kwa njia ovu kupitia ufujaji mabilioni ya pesa za umma, kuongeza marupurupu manene kwa lengo moja tu yaani kujitajirisha nafsi zao na sio mtu wa kawaida. Baya zaidi, wanasukuma ile wanayoiita miradi ya maendeleo kama njia ya kuhalalisha ufisadi wao.   

Tungependa kusema waziwazi kuwa umasikini unaweza kutatuliwa pekee ikiwa nidhamu hii ya kiuchumi ya Kimagharibi itatupwa kwenye jaa la kihistoria na mahali pake kubadilishwa kwa nidhamu imara ya kiuchumi ya Kiislamu. Uislamu sio dini pekee bali ni mfumo ulio fungamanishwa na mpangilio kamili wa maisha unaoweza kutatua matatizo yote ya mwanadamu. Ama swali juu ya jinsi gani Uislamu hutatua matatizo haya, ni kwa sababu umefafanua kuwa chanzo kikuu cha matatizo haya kiko katika usambazaji wa rasilimali badala ya uzalishaji. Hili litamwezesha kila mtu kuwa huru kushibisha mahitaji yake msingi. Uislamu umesisitiza zaidi juu ya kadhia ya mizani ya usambazaji rasilimali kuliko tu juu ya fikra ya uzalishaji pekee. Mbali na kuharamisha ukiritimba wa rasilimali kuzunguka miongoni mwa matajiri pekee. Hili lamaanisha, tatizo linalo wakumba watu ulimwenguni haliko katika uhaba wa rasilimali kama warasilimali wanavyo jaribu kuonyesha, ukweli ni lau rasilimali zisambazwa kwa usawa, basi kadhia ya umasikini ingekuwa imetatuliwa. Ni kupitia nidhamu hii ya kiuchumi ambapo Uislamu chini ya usimamizi wa Dola ya Khilafah utaweza kuangamiza umasikini kwa raia wote Waislamu na wasiokuwa Waislamu vilevile. Mwenyezi Mungu akipenda pindi Dola ya Khilafah itakapo simamishwa tena, kadhia ya umasikini itazikwa katika kaburi la sahau.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afrika Mashariki
Address & Website
Tel: +254 717 606 667 / +254 737 606 667
www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail:  abuhusna84@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu