Jumanne, 14 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  29 Jumada I 1440 Na: 1440/016
M.  Jumatatu, 04 Februari 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Mwaelekea Wapi, Enyi Munao Simamia Muongozo wa Utoaji Fatwa wa Kiulimwengu?!!

(Imetafsiriwa)

Baadhi ya wanaume wa Al-Azhar wanaendelea kutembea juu ya barabara ya kuushambulia Uislamu na Hukmu zake pasi na maono wala hofu kwa Mwenyezi Mungu (swt). Wanaendelea kuifanya Al-Azhar Al-Sharif – ambayo ilikuwa ndio ngome dhidi ya njama za maadui wa Uislamu – jukwaa ambalo wanavishambulia vipengee vya Uislamu na Hukmu zake zinazo husiana na wanawake. Meza ya Utoaji Fatwa wa Kiulimwengu ya Jumba la Fatwa la Misri (Dar al-Ifta) zilisema kuwa, “fatwa juu ya kadhia ya ndoa kwa watoto wadogo zimeifunga ndoa kwa watoto wadogo katika mahusiano ya kijinsia pekee, na kwamba Hizb ut Tahrir imeifunga ndoa katika mahusiano ya kijinsia pekee, ikiondoa upande wa kisaikolojia, kiafya, kiakili na mambo ya kimwili, na kuweka mbali kiwango cha uvumilivu na jukumu ambalo mkataba wa ndoa unalazimisha juu ya pande zote mbili …” Hili, kwa kuanzia, linagongana na yale ambayo Quran Tukufu imeeleza kuhusu fahamu ya ndoa kama utulivu na huruma.

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجاً لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿

“Na katika alama Zake ni kukuumbieni kutokana na nafsi zenu wake ili mupate utulivu ndani yao; na Akajaalia baina yenu mapenzi na huruma. Hakika katika hilo kuna alama kwa watu wenye kutafakari.” [Ar-Rum: 11]

Zaidi ya hayo, Uislamu haukuweka umri maalumu kwa ajili ya ndoa, Allah (swt) asema katika Kitabu Chake Kitukufu:

  وَأَنْكِحُوا الْأَيَامَى مِنْكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ﴿

“Na oeni wasio na waume miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu.” [An-Nur: 32]

Neno أَيِّم “Aiim” lamaanisha: mwanamke ambaye hajaolewa asiyekuwa na mume, ima ni bikra au mke mkuu, na mwanamume ambaye hajaoa asiyekuwa na mke, na dalili ni ya jumla kwa kila mwanamume ambaye hajaoa au mwanamke ambaye hajaolewa pasi na kufafanua umri maalumu wa ndoa, hivyo basi, hakuna kile kinachoitwa “ndoa ya chini ya umri” au hata ndoa ya mapema au ndoa ya kucheleweshwa katika Uislamu. Msichana aweza kuolewa hata kabla ya kuanza hedhi, kama Yeye (swt) anavyo sema: 

وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِنْ نِسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ﴿

“Na wale ambao hawapati tena hedhi miongoni mwa wake zenu – ikiwa munashaka, basi eda zao ni miezi mitatu na (pia) wale ambao kamwe hawajawahi kupata hedhi.”  [At-Talaq: 4]

Hii yamaanisha kuwa inaruhusiwa kwa msichana kuolewa kabla ya kuanza hedhi, na sio tu kwa kutimu umri wa Taklif (kulazimishwa kujifunga na Shari’ah); hizi ndizo hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) na sio rai ya Hizb ut Tahrir.

Wanajigamba pia kwa kusema, “Imethibitishwa kupitia afya na watafiti wa kijamii kuwa msichana hudhurika kimwili na kisaikolojia; huenda hata akafa kutokana na ndoa za mapema.” Na hapa tunawauliza kuhusu mahusiano haramu ambayo yameenea katika nchi za kimagharibi kati ya wale wanaoitwa kuwa ni watoto, mimba haramu za wasichana kati ya umri wa miaka 12 na 18, na kinamama ambao hawajaolewa katika umri huu!!! Je, kuvunjwa huku kunakubalika na hakusababishi madhara ya kimwili na kisaikolojia kwao, na hakukiuki haki zao kama watoto, huku ndoa ya halali inayo hifadhi haki na utu ikionekana kama ukiukaji wa haki hizo na kupoteza afya ya kiakili na kimwili?! Ni uovu ulioje kuhukumu kwao huku …

Wamepuuza pia kuwa Uislamu, vipengee na sheria yake zinakubalika katika kila zama na mahali kwa sababu ni sheria ya Mola wa wanadamu, na Yeye ni mjuzi zaidi wa vile alivyo viumba, na sheria zake hazibadiliki kwa kubadilika zama, mahali, hali na desturi … Kwa hivyo, mtu hapaswi kusema, yale yaliyokubalika na kutendeka wakati wa zama za mama zetu na bibi zetu sasa hayakubaliki kwa sababu ya maendeleo, na mahitaji ya maisha, na kwamba wasichana sasa hawawezi kuchukua jukumu la nyumba, mume na watoto … Madai haya ni natija ya elimu ya kimakosa ambayo msichana halelewi kuwa mama na mke, bali analelewa kuwa mfanyikazi na mshindani kwa wanaume katika uwanja wa kazi hata kama ni kwa gharama ya nafsi yake na nyumba yake na watoto wake. Vile vile, kijana hawezi kugharamia kuoa na kubeba mizigo ya kimada, sio kwa sababu ya umri wake mchanga, bali kutokana na ulafi wa nidhamu ya kirasilimali na dhuluma za serikali zake zinazo dhibiti mali na utajiri wa nchi na hazidhamini raia wake kujimudu au ajira, ikipelekea kuenea kwa ukosefu wa ajira na umasikini. Lau Uislamu ungetekelezwa, mahitaji msingi ya chakula, mavazi na makaazi yangedhaminiwa, na dola hiyo ingewahakikishia vijana kazi na hivyo kuwasaidia kuhimili familia na mizigo ya kimada … Maisha hayo yangekuwa tofauti kiasi gani na maisha yetu ya leo ya mateso, ufukara, dhuluma na taabu.  

Tunapo angalia mapendekezo ya Kamati hii ya al-Ifta ya kuweka kiwango cha umri wa ndoa kwa msichana kuwa miaka kumi na nane na kuwaadhibu wale wanaofungisha ndoa ambayo iko chini ya umri huu au kuhusika katika ndoa kama hii, chini ya uwazi na enzi ya uhuru na Fitna na kuporomoka kwa thamani na maadili ambayo tunaishi ndani yake, tunatambua kuwa ni fikra ya Kimagharibi pekee ambayo kwayo wanataka kueneza uchafu miongoni mwa Waislamu;

  إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿

“Hakika, wale ambao wanapenda uchafu (zinaa) uenee kwa waumini watapata adhabu kali duniani na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamujui.” [An-Nur: 19]

Kwa hivyo, zingatieni, Enyi watu wenye akili.

Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu