Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 17 Jumada II 1360 | Na: 1440/018 |
M. Ijumaa, 22 Februari 2019 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wanawake wa Palestina Wangali Wanamsubiri Al-Mu’tassim ili Kuitikia Kilio Chao!!
(Imetafsiriwa)
Vyombo vya habari vilichapisha picha na video za majeshi vamizi ya umbile la Kiyahudi yakifurusha katika nyumba moja ya familia ya Jerusalem eneo la Aqaba Al-Khalidiya katika mji wa kale wa Jerusalem kwa kutumia nguvu za kijeshi. Vyombo hivyo vya habari vilionyesha nduru na malalamishi ya wanawake waliolalamikia shambulizi la polisi wa Kiyahudi katika nyumba hiyo, wakimpiga na kumkamata mwenye nyumba hiyo, na kuwaacha wao bila ya ulinzi na makao baada ya nyumba yao kuchukuliwa.
Ni muhimu kutambua kuwa idadi kubwa ya majeshi hayo vamizi yalivamia nyumba hiyo na kuweka kizuizi cha kijeshi pambizoni mwake, na kuitoa familia katika nyumba yao, ambayo wameishi ndani yake kwa miaka 65, ili kunufaisha mashirika ya makao kwa mujibu wa kanuni ya makao “msimamizi wa mali ya asiyekuwepo”; ukizingatia kuwa wakili wa familia hiyo alichukua uamuzi wiki moja iliyopita kupitia mahakama ya Wavamizi hao kuakhirisha ufurushaji huo hadi mwisho wa mwezi huu.
Misururu ya kutia Uyahudi jiji la Jerusalem na kuondolewa wakaazi wake kutoka humo kunaendelea kupitia mbinu tofauti tofauti. Shambulizi juu ya al-Aqsa lingali linaendelea vikali na katika mielekeo kadha wa kadha, ikiwemo ufurushaji katika nyumba zinazo elekeana na Msikiti wa Al-Aqsa, kuzichukua na kisha kuzikabidhi kwa walowezi hao, ambayo yamo ndani ya sera ya Mayahudi wanaotafuta kuwafukuza Wanati wa Jerusalem na kubadilisha idadi ya wakaazi ndani ya mitaa ya eneo la Mashariki ili wengi wao wawe ni Mayahudi.
Kuna njama kabambe za kuwafurusha Wanati wa Jerusalem kupitia kutabanni misururu ya mipangilio ya kisheria yenye ubaguzi wa rangi, kutokana na utozaji ushuru mzito juu ya Wanati wa Jerusalem, na kuwazuia kujenga, pamoja na sera ya ubomoaji inayofuatwa na umbile la Kiyahudi inayowalazimisha Wazaliwa wa Jerusalem kubomoa nyumba zao kwa mikono yao wenyewe ili kuepukana na faini nzito zinazotozwa na manispaa hiyo vamizi endapo vifaa vya manispaa vitatumika kubomoa. Mwaka jana, ubomoaji wa nyumba 136 na maduka 20 ulirekodiwa, na mwaka huu, zaidi ya ubomoaji 20 umerekodiwa.
Mchakato huu wa kutia Uyahudi hauathiri tu nyumba pekee. Majaribio yangali yanafanywa ili kuchukua kilichobakia katika makaburi ya Bab al-Rahma, ikiongezewa na jaribio la kuangamiza kumbukumbu za kidini, ikiwemo kuharamisha Adhana.
Na hawa hawapa ni wanawake na watoto zaidi waliotupwa mabarabarani bila ya makao wala hifadhi huku ulimwengu mzima ukitazama, na hivi hapa vilio, nduru na miito ya msaada ya wanawake hawa, iliyopasua mawingu angani, wakiwa hawana msaidizi wala mwokozi wa kuwaitikia! Hata mamlaka hiyo ya aibu haitoi hata neno moja ambalo angaa litaonyesha shutuma zake kwa yale yanayojiri; haumiliki tena wala kuweza kutoa hata kauli!!
Enyi Ummah wa Kiislamu!
Mwasubiri nini zaidi?!! Pindi vyombo vya habari vinapoonyesha kilio au nduru ya mwanamke anayedai kudhulumiwa kwa kutekelezewa Hukumu ya Shari'ah, ulimwengu mzima hutulizia makini sana hili, lakini hujitia uziwi na upofu mbele ya wale wanaofurushwa majumbani wao pasi na hata ya kuwa na fursa ya kufunganya mali zao binafsi!! Ni mizani ovu ilioje hii ya upimaji mambo na matukio …
Enyi Watu wa Ardhi Tukufu (Palestina):
Matukio yanaendelea kuthibitisha siku hadi siku muozo wa mamlaka ya aibu na khiyana zake dhidi ya biladi hiyo na watu wake, na kusisitiza sera ya utumwa kwa Mayahudi na nguvu dhidi ya watu. Ni sharti musimame kwa umoja dhidi yake, ili ikome kuvuka mipaka yake na ijue kuwa khiyana yake sasa idhahiri kwa kila mtu, kijana au mzee …
(وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ)
“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka!” [26:227]
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |