Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  2 Jumada I 1445 Na: 1445 H / 016
M.  Alhamisi, 16 Novemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kampeni ya Kimataifa na Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina Kuyaita Majeshi ya Waislamu Kuwaokoa Wanawake na Watoto wa Gaza na Kuikomboa Ardhi Yote ya Al Aqsa

(Imetafsiriwa)

Huku ulipuaji mabomu wa kikatili wa Gaza ukiendelea na umbile uaji la 'Kizayuni', ni wanawake na watoto ndio wanaohimili makali ya mauaji haya ya halaiki, wakijumuisha 70% ya wale waliouawa. Mvua ya mabomu kwenye majengo ya makaazi, maeneo ya hifadhi, shule, hospitali na vitongoji yamesababisha Gaza kuwa makaburi kwa wanawake na watoto, huku watoto zaidi ya 4500 na wanawake 3000 wakiuawa tangu Oktoba 7. Uvamizi huo wa kihalifu imepiga mabomu Hospitali ya Uzazi ya Al-Mahdi, na hospitali za watoto za Al Nasr na Al Rantisi ambazo zilikuwa zikiwahifadhi wanawake na watoto waliokosa makao; Ndege zake za kivita zimeshuka fosforasi nyeupe kwenye shule; na mtoto mmoja wa Palestina anauawa kila dakika 10.

Kuzingirwa huku kwa kikatili kumesababisha wanawake kufanyiwa upasuaji wa uzazu pasi na dawa za kuzima maumivu, madaktari kukata viungo vya watoto waliojeruhiwa pasi na dawa za kuzima maumivu, na watoto ndani ya incubators wakifa kwa sababu ya hospitali kukosa oksijeni na mafuta. Lengo la wazi ni kuangamiza na mauaji ya kimbari kwa idadi ya mustakbali ya Wapalestina kutoka Ardhi Iliyobarikiwa ya Al Aqsa.

Katika kujibu mauaji haya ya halaiki ya karne ya 21 na Nakba, Kitengo cha wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa kushirikiana na Wanawake wa Hizb ut Tahrir ulimwenguni wamezindua kampeni kubwa ya kimataifa inayoongoza hadi "Siku ya Kimataifa ya Wanawake Kuchukua Hatua kwa ajili ya Palestina" Mnamo tarehe 26 Novemba kuyataka majeshi nchi za Waislamu kutaharaki haraka kuwaokoa wanawake na watoto wa Gaza na kuikomboa ardhi nzima iliyobarikiwa ya Palestina kutokana na saratani hii. Siku ya Kuchukua Hatua itaenea zaidi ya mabara 5 na itajumuisha maandamano, semina na amali zengine za wanawake nchini Palestina, Uturuki, Indonesia, Tunisia, Lebanon, Malaysia, Kenya, Amerika, Australia, Denmark, Uholanzi, Ubelgiji na Uingereza.

Wanawake wa Kiislamu na watoto wa Gaza wametelekezwa kwa mauaji haya ya halaiki na kila serikali ya ulimwengu. Serikali za Kimagharibi zimethibitisha msimamo wao kama washirika wa mauaji haya ya halaiki, zikiwa tayari kulinda na kuunga mkono msingi wa sera zao za kikoloni - umbile la Kizayuni - bila kujali kiwango cha uhalifu wake na kiwango cha kukiuka sheria zao wenyewe za kimataifa. Wakati huo huo, watawala na serikali za ardhi za Waislamu wanaendelea kutoa taarifa tupu na wanaitisha mikutano tasa huku wakifunga minyororo majeshi yao kwenye kambi zao wakati Ummah wao unatiririka damu. Wamatengeneza fani yao kutokana na usaliti wa Waislamu na Dini yetu, baada ya kuhalalisha mahusiano na uvamizi huu wa kikatili na kuimarisha mkono wake kupitia mikataba ya biashara ya mabilioni ya dolari.

Kama wanawake wa Ummah huyu mtukufu, tunawaomba kaka zetu katika majeshi ya Waislamu kuzinduka kwenye kusudi lao la kweli kama watetezi wa Waislamu na Dini yao na kuandamana hadi Al Quds kwenda kuwakomboa wanaume, wanawake na watoto wa Palestina kutokana na uvamizi huu muovu, kwa kuwa wao pekee ndio walio na ndege, mizinga, silaha, na askari wa kukomesha jinamizi hili lililopo milele. Tunatoa wito kwa maafisa wa majeshi ya Waislamu kufuta mipaka hii ya bandia iliyowekwa na wakoloni baina ya ardhi zetu unayotumiwa kutugawanya sisi Waislamu na kuwaruhusu maadui zetu kututesa. Tunawataka waving’oe viti vya utawala vya watawala hawa wakatili na wasaliti na serikali ambazo zimetumika kama walinzi halisi wa umbile hili la Kiyahudi. Na tunatoa wito kwao wajibu vilio vya dhiki vya kina mama, wajane na watoto yatima wa Gaza wanaaoomboleza na kwenda kuwatetea na kutoa Nusrah (msaada wa kimada) kwa ajili ya kusimamisha uongozi na mfumo wa kweli wa Kiislamu, Khilafah kwa njia ya Utume itakayohamasisha majeshi kukomboa kila shubiri ya ardhi ya Kiislamu inayokaliwa kimabavu na Waislamu wote wanaokandamizwa kote ulimwenguni. Tunawakumbusha maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako” [An-Nisa: 75].

Kampeni hii inaweza kufuatiliwa katika ukurasa wa Kiingereza: https://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/hizbuttahrir/25393.html

Ukurasa wa Kiswahili: https://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/afisi-kuu-ya-habari/3583.html na Facebook: Women’s Section CMO – HT. Linki ya video fupi ya Kampeni: https://youtu.be/E4bkN60x8MI. Alama Ishara ya Kampeni: #ArmiesToAqsa

Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu