Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 29 Rabi' II 1445 | Na: 1445 H / 014 |
M. Jumatatu, 13 Novemba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watu wetu mjini Gaza Wanaangamizwa Huku Watawala Wasaliti Wanatazama Hivi Wako Wapi Watu wenye Ikhlasi katika Ummah wa Uislamu?
(Imetafsiriwa)
Mnamo siku ya 35 ya vita vyake dhidi ya Ukanda wa Gaza, umbile la Kiyahudi lilivisukuma vikosi vyake pamoja na vifaru vyake karibu na eneo la Uwanja wa Hospitali katikati mwa mji wa Gaza, ambalo linajumuisha hospitali 4, Al-Rantisi, Al-Nasr, Al-Ayoun, na hospitali ya afya ya akili. Vikosi vyake vilizingira maeneo yake huku kukiwa na mzoroto mkubwa katika sekta ya afya, haswa kufuatia mzingiro mkali uliuweka kwenye Ukanda wote wa Gaza tangu Oktoba 7.
Licha ya kile kilichoainishwa katika mikusanyiko ya kimataifa na sheria zinazoharamisha mashambulizi kwa taasisi na vitengo vya afya, zikiwemo hospitali, umbile hili la kikatili limepitiliza mno katika udanganyifu na udhalimu wake na limelenga Uwanja wa mahospitali mjini Gaza. Kifungu cha 18 cha Mkutano wa Geneva IV, kilitenga ulinzi maalum kwa mahospitali. Hairuhusiwi - kwa hali yoyote ile - kulenga hospitali za raia zinazotoa huduma kwa waliojeruhiwa, wagonjwa, walemavu, na wanawake, na lazima waheshimiwe na kulindwa wakati wote. Mkutano huo pia unaelezea katika kifungu chake cha 19 kwamba "ulinzi kwa hospitali za raia kamwe hautakoma." Ulinzi huu unaenea hadi kwa waliojeruhiwa na wagonjwa, pamoja na wafanyikazi wa matibabu na njia za usafirishaji.
Umbile la Kiyahudi halikufuata sheria na makubaliano haya na kuvunja maagano, kwa kiburi na jeuri zote. Jambo hili halikuwa mbali nao, kwani hii ilikuwa ndio tabia yao na wanayojulikana kwayo, hawakutimiza ahadi wala ujamaa wowote na wagonjwa na watoto. Walizizingira hospitali hizo zilizokuwa na maelfu ya wagonjwa, wafanyikazi wa matibabu, na watu waliokosa makao ambao hawana mahitaji msingi ya kuishi walionyimwa maji au chakula. Eneo hili pia linajumuisha shule nyingi na majengo ya makaazi.
Umbile hili geni hutumia kila aina ya visingizio. Linadai kwamba lengo la operesheni zake ni kumaliza "magaidi" na harakati ya Hamas. Linatoa madai ya uvumi kwamba wapiganaji wa harakati hii wanatumia hospitali kadhaa mjini Gaza kama kambi kwa viongozi wao walio mafichoni. Pengine linataka kufanya vitendo vyake vya kihalifu viwe chini ya kile makubaliano yao yanakiita "takhsisi," kama vile matumizi ya vituo vya matibabu na moja ya pande za mzozo kufanya "kitendo cha kumdhuru adui," nje ya wigo wa misheni za kibinadamu. Hata sheria wanazotunga na makubaliano wanayohitimisha yana mianya ambayo wanaweza kukwepa kushutumiwa, ingawa umbile hili la kihalifu halitilii maanani shutma au adhabu, kwa sababu linaungwa mkono na Magharibi ambayo inaunga mkono vita vyake dhidi ya watu wa Palestina na Waislamu kwa jumla.
Ewe Ummah wa Uislamu! Je! Udhalilishaji huu utadumu mpaka lini? Watu wa batili wanasaidiana wao kwa wao na kuungana kupiga vita Uislamu na Waislamu, na nyinyi enyi watu wa haki, ni kama povu kwenye bahari ambayo mataifa yanapigana dhidi yenu kama wanyama wanavyopigania chakula chao?! Watu wa Gaza wanaangamizwa huku Ummah wa Uislamu ukiwaangalia kutoka mbali, na kubwa wanaloweza kufanya ni dua na kilio kirefu?! Wanalisaidia umbile la Kiyahudi kwa ndege, wanajeshi na vifaa, huku sisi, Ummah wa Uislamu, tukijaribu kutuma bidhaa na dawa?! Je! Hivi ndivyo nusra yetu na msaada wetu utakavyokuwa kwao?
Afisi ya Habari ya Serikali mjini Gaza ilitangaza mnamo Ijumaa, Novemba 10, kwamba umbile la Kiyahudi lililipua Ukanda wa Gaza kwa takriban tani 32,000 za vilipuzi na mabomu zaidi ya 13,000, yenye wastani wa tani 87 za vilipuzi kwa kila kilomita moja mraba. Aliongeza kuwa zaidi ya asilimia 50 ya nyumba za makaazi mjini Gaza ziliharibiwa na uvamizi na mabomu, huku nyumba 40,000 zilibomolewa kabisa.
Enyi majeshi ya Ummah wa Uislamu! Je! Hamjachochorwa na kile wahalifu hawa wanachofanya dhidi ya watoto wa Ummah wenu?! Je! Damu yenu haichemki kwenye mishipa yenu ili kuwaokoa, kuwa msaada kwao, na kuzuia uvamizi huu wa kikatili kutoka kwao?! Je! Hamna ujasiri wa kuzuia mauaji haya ya halaiki kufanywa dhidi ya watoto na wanawake wa Ummah huu?!
Katika taarifa yake, Wizara ya Afya ilitangaza kwamba hospitali 18 katika Ukanda wa Gaza zilikosa huduma tangu kuanza kwa uvamizi wa umbile la Kiyahudi mnamo Oktoba 7, na kusema kwamba umbile hili lilikuwa linafanya "uhalifu mkubwa dhidi ya mahospitali na wafanyikazi wa matibabu. Lilianza kwa kuzuia kuingia kwa mafuta na vifaa vya matibabu ndani yazo, na leo linamalizia kwa kulenga mahospitali moja kwa moja na moto na mabomu." Hivi wako wapi watawala wa Kiislamu kuhusiana kile kinachotokea kwa watoto wasio na hatia na wagonjwa na watu wa Gaza na Palestina?! Barakoa zao zimepomoka, utiifu wao na uaminifu wao kwa adui, na uhalalishaji wao wa mahusiano nalo umefichuliwa. Wamesimama nalo dhidi ya Ummah wao na kuuza nafsi zao kwa badali ya viti na utawala. Enyi Ummah wa Uislamu, mnatarajia nini kutoka kwa watu hawa? Je! Watahamasisha majeshi ili kuikomboa Al-Aqsa na kuinusuru Gaza na Palestina?!
Enyi Ummah wa Uislamu: Mtakaa kimya mpaka lini? Ndugu na dada zetu wanaangamizwa, watawala wanatazama, na majeshi yamefungwa kwenye kambi! Je! Sio wakati sasa wa kuangamiza viti vya utawala na kuhamasisha majeshi?! Enyi Ummah wa Uislamu: Mamlaka yako mikononi mwenu, kwa hivyo anzisheni mapinduzi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katik kuinusuru Dini yake, na muwabadilishe wasaliti hawa kwa watu waaminifu ili waweze kukuongozeni kwenye njia sahihi na kukutoeni kwenye giza la Mfumo wa kisekula wa kirasilimali hadi kwenye nuru ya mfumo wa Mola wenu unaochipuza kutokana na Aqida yenu (itikadi).
Sisi, katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, tunamuomba kila mtu mwenye ikhlasi katika Ummah huu kuwataka watu wanaomiliki nguvu na ulinzi kuchukua hatua za haraka kuzuia mauaji haya ya halaiki yanayofanywa na umbile hili halifu, na kufanya kazi na watu wa Ummah wao kuung’oa na kuuondoa mfumo huu wa kisekula na kusimamisha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu chini ya hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) ambao aliuteremsha kama rehma kwa walimwengu. Mwenyezi Mungu (swt) aliahidi kumnusuru (Nusrah) yeyote anayemnusuru Yeye, kwa hivyo tangazeni hilo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt).
[إنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الأَشْهَادُ]
“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi” [Ghafir: 51]
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |