Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  9 Rajab 1439 Na: 1439/018
M.  Jumanne, 27 Machi 2018

 

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watoto wa Ardhi Tukufu (Palestina) Wanaendelea Kutolewa Kafara Kutokana na Uhaini na Utiifu wa Biladi (za Waislamu kwa makafiri)!
(Imetafsiriwa)

Katika ripoti iliyo chapishwa na kituo cha habari cha Al-Jazeera idhaa ya Kiingereza, maafisa wa Umoja wa Mataifa (UM) walishutumu kuendelea kukamatwa kiholela kwa watoto katika Ardhi Tukufu (Palestina) na umbile la Kiyahudi, ikisema kuwa “Unyimaji uhuru huu kwa watoto hawa ni wa kitaasisi, kinidhamu, na ulio enea pakubwa”. Msururu wa ripoti za UM zilizo wasilishwa katika lile linaloitwa Baraza la Haki za Kibinadamu zimeonyesha jinsi hali za maisha za watu wa ardhi tukufu ya Palestina na Ukingo wa Magharibi na Gaza zilivyo zidi kudorora kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, na jinsi watoto wanavyo himili ukatili wa uvamizi wa umbile la Kiyahudi, kwa mujibu wa Kate Gilmore, Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa UM.  

Na shahidi kutoka katika familia zao alitoa ushuhuda, kuwa serikali ya umbile la Kiyahudi inaendelea kutekeleza ukamataji kiholela wa watoto wa ardhi tukufu (Palestina), ambapo mamia ya watoto wamekamatwa kiidara, yaani, bila ya kufunguliwa mashtaka, ikiongezewa na mamia ya wengine waliokamatwa siku za nyuma. Pia inawapa vifungo vya nyumbani na kuwatendea vitendo vya kinyama mno vitokanavyo na ugaidi wa serikali hiyo, ikikiuka yote ile inayoitwa mikataba ya kimataifa iliyo tarajiwa kuwalinda watoto na kuwahifadhi chini ya kanuni ya kimataifa. Hivyo basi, inabakia kuwa “dola” pekee ulimwenguni ambayo inawakamata na kuwashtaki watoto katika mahakama za kijeshi na kuwachukulia kama watu wazima na kuwalazimishia juu yao mipangilio ya kinyama katika magereza, ambamo, wanapitia unyanyasaji na dhulma, na aina tofauti tofauti za mateso na ghasia, inayo peleka kuangamia na kuvunjika moyo kwa watoto hawa.

Licha ya ripoti hizi, jamii ya kimataifa na “mashirika ya haki za kibinadamu” yamesalia kimya yakitazama, kuthibitisha tena na tena kuwa hayatetei haki wala wenye kudhulumiwa na kamwe hayajali chochote kuhusu haki za kibinadamu au haki za watoto kama yanavyo dai. Hayachukui hatua yoyote zaidi ya kuandika na kutoa taarifa pekee, kimya chao hugeuka kuwa uziwi zinapokuja kadhia zinazo husiana na Uislamu na vipengee vyake. Lakini, utaona tarumbeta zao zikipuliza na mikono yao kufanya kazi kushambulia vipengee hivi, ikivizingatia kuwa vyenye kukiuka haki za watoto!! Na kuna dalili nyingi ya hili… Pia hatuoni mamlaka ya Dayton ikichukua hatua ya kusitisha ukiukaji na ukamataji huu dhidi ya watoto hawa, hususan katika muktadha wa mpangilio wa kiusalama unao hifadhi umbile la Kiyahudi…

Enyi Watu wetu katika Ardhi Tukufu (Palestina):

Matukio haya yanathibitisha tena na daima kuwa hakuna kitakacho mkomesha mvamizi huyu na kuondoa dhulma kwenu na watoto wenu, isipokuwa dola yenye nguvu inayo tawala kwa Uislamu na kueneza uadilifu; dola ya Khilafah Rashidah katika njia ya Utume. Hivyo basi, fanyeni kazi na wale wanaoifanyia kazi na kung’oa serikali za mabwege (ruwaibidhat) ambazo ni mchomo wa kisu vifuani mwenu.

 (إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ وَإِذَا أَرَادَ اللّهُ بِقَوْمٍ سُوءًا فَلاَ مَرَدَّ لَهُ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِ مِن وَالٍ)

“Hakika, Allah habadilishi hali za watu mpaka wabadilishe yale yaliyo ndani ya nafsi zao. Na Allah anapo watakia mabaya watu, hakuna cha kuzuia. Wala hawana mlinzi yeyote badala yake.”  [Ar-Ra’d: 11]

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu