Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  1 Ramadan 1439 Na: 1439/024
M.  Alhamisi, 17 Mei 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Risasi Zimechukua Maisha ya Watu … Na Serikali Zinacheza Densi Juu ya Majeraha!
(Imetafsiriwa)

Kwa mujibu wa mashirika ya habari; mtoto wa miezi 8 Laila Al-Ghandour alifariki mnamo Jumanne asubuhi eneo la Mashariki mwa Gaza baada ya kuvuta gesi. Tukio hili linaongeza idadi ya mashuhadaa wa “Msafara wa Mkubwa wa Maregeo” na kufikia idadi ya 61, wakiwemo watoto 7 na majeruhi 2,800, wengi wao wakiwa ni kutokana na risasi na wengine wakiwa ni kutokana na vipande vya mabomu na gesi ya sumu wakati wa uzimaji msafara na majeshi ya umbile la Kiyahudi iliyoanza maeneo tofauti Mashariki mwa ukanda wa Gaza katika kumbukumbu ya miaka 70 ya Nakba, na ambayo ilipinga na kukataa kuhamishwa kwa ubalozi wa Amerika jijini Al-Quds (Jerusalem).

Misafara hii ilianzishwa katika ukanda wa Gaza mnamo 30/3/2018 ikiafikiana na kumbukumbu ya Siku ya Ardhi, huku kukiwa na juhudi za kulainisha kadhia ya Ardhi Tukufu (Palestina) na kumakinisha uwepo wa umbile la Kiyahudi na kusawazisha mahusiano nalo ambapo kadhia hiyo ilifikia nukta ya kuwa umbile hili linasherehekea kumbukumbu ya kubuniwa kwake katika miji ya Kiarabu. Wajumbe kutoka Imarati na Bahrain walishiriki katika marathon kusherehekea tukio hilo hilo, wakiipuuza na kuicha mkono Palestina na majanga yake na kukaliwa kwake, kupitia utabikishaji wa kimakosa na wa kufedhehesha wa kanuni za mkataba wa karne hii, na kuharakisha kwa Trump kuutabikisha, ili kukamilisha mradi wa umbile la Kiyahudi unaowakilishwa na Netanyahu.

Hili linafanywa kupitia kushiriki na baraka kutoka kwa mamlaka ya Abbas, yanayoshajiisha uvamizi juu ya Gaza, na kujadiliana na Mayahudi na Wamagharibi, na hata kupeane kile ambacho si haki yake Abbas kama kawaida ya hamasa zake kwa mauwaji ya Mayahudi dhidi ya watu wa Gaza na Palestina, aliomba kufanyika kwa kikao cha dharura cha Baraza la Usalama kujadili yale yanayo endelea katika Ardhi Tukufu (Palestina), na kuunda tume huru ili kuchunguza ukiukaji wa haki za kibinadamu uliotekelezwa na majeshi ya Kiyahudi dhidi ya Waislamu katika Ardhi Tukufu (Palestina).

Aliamua pia “kutangaza mashambulizi mapana na bendera (za kundi) kupeperushwa nusu mlingoti katika kuomboleza mashuhadaa, ambao roho zao zilitoka wakati wa misafara ya maregeo kutokana na kuhami haki zao halali za kuasisi dola yao huru ya Palestina huku Jerusalem Mashariki ikiwa makao yake makuu na kuhami matukufu yao ya Kiislamu na ya Kikristo na kupinga tangazo la Trump na kufunguliwa kwa ubalozi wa Amerika jijini Jerusalem, na haki yao ya kuregea majumbani mwao na ardhi yao ambayo walilazimishwa kuondoka!!” Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi asema kuwa Jerusalem ni makao makuu ya milele ya umbile lake la kikatili, huku Abbas akiigawanya Mashariki na Magharibi!! Aibu ilioje kwake yeye na maamuzi yake.

Huku risasi za jeshi vamizi katili zikichukua uhai wa mashuhadaa eneo la Gaza, na kina mama na baba wakiwaaga wapendwa wao, serikali yake, kupitia baraka za watawala wa biladi za Waislamu, ilikuwa ikicheza densi juu ya damu zao katika sherehe ya ufunguzi wa ubalozi wa Amerika eneo la Al-Quds mbele ya ujumbe wa Kiamerika ulioongozwa na binti wa Raisi wa Amerika na mumewe, mshauri wake.

Enyi watu wa Ardhi Tukufu (Palestina): ikiwa mwadhani kuhamishwa kwa ubalozi hadi Al-Quds ni uchungu, basi kuwepo kwa Ummah wa Kiislamu bila ya dola inayotekeleza sheria ya Allah na kukomboa biladi na watu ni dhulma na uchungu zaidi. Al-Quds (Jerusalem) ni kama Jaffa, Haifa na Tel Al-Rabee’ (Tel Aviv), zote zimekaliwa na kunyakuliwa, na ukombozi wake sio kupitia majadiliano wala maridhiano ya kufuatana; wala kwa kupitia suluhisho la dola mbili wala misafara, lakini ukombozi wake ni kupitia kuwepo kwa jeshi lililojipanga na kujihami likiongozwa na Imam na Khalifah atakaye kata mizizi ya Mayahudi na wafuasi wao.

Enyi Waislamu popote mulipo: katika biladi za Waislamu kuna zaidi ya wanajeshi milioni 10, ndege 20,000, vifaru 50,000 na mamilioni ya silaha na mamilioni ya watu waliotayari kujitokeza kuikomboa Ardhi Tukufu (Palestina) ili kuiregesha kwa Waislamu. Ikiwa hakuna tamaa kwa viongozi na watawala, basi tamaa yetu iko kwa maafisa na wanajeshi wenye ikhlasi, kwa hivyo zungumzeni nao na familia zao kuwakumbusha jukumu lao kwa Ummah wao na Dini yao, na hasira za Allah juu yao ikiwa watanyamazia kimya, kutazama na kutii maagizo ya viongozi na watawala wao vibaraka walioajiriwa wanaofeli kutekeleza sheria ya Allah. Ardhi Tukufu (Palestina) ni amana juu ya shingo za Waislamu wote, na hairuhusiwi kukhini amana hii au kuitupa. Allah (swt) asema:

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَخُونُواْ اللّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُواْ أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ)

“Enyi Mulioamini, musimkhini Allah na Mtume na mukakhini amana zenu na hali nyinyi munajua [matokeo ya hilo].” [Al-Anfal: 27]

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu