Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 28 Dhu al-Hijjah 1439 | Na: 1439/030 |
M. Ijumaa, 10 Agosti 2018 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Faini ya Kwanza ya Denmark kwa Wanawake Wanaovaa Niqab Itawasukuma Waislamu Kushikamana na Maadili ya Kiislamu Hata Zaidi!
Mnamo Agosti 4, 2018, shirika la habari la BBC liliripoti juu ya mwanamke wa kwanza wa Kiislamu kulipishwa faini nchini Denmark kwa ajili ya kuvaa niqab hadharani. “Bunge la Denmark liliidhinisha mswada mnamo Mei 2018 wa kumwadhibu yeyote anayevaa niqab kwa faini” (BBC, 31 Mei 2018). Kwa sasa sheria hiyo haitaji burka na niqab kwa majina, bali inaeleza, “Yeyote anayevaa nguo inayofinika uso hadharani ataadhibiwa kwa faini”. Marufuku hiyo ilipangwa kuanza utekelezwaji wake mnamo Agosti 2018. Mnamo Ijumaa 3 Agosti 2018 mwanamke wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 28 aliyekuwa amevaa niqab katika soko kuu la hadhara mjini Horshom, km 25 (maili 15) kaskazini mwa Copenhagen, alishambuliwa kwa nguvu na mwanamke mwengine aliyepinga vazi lake na kuchukua hatua mikononi mwake kumvua kwa lazima vazi hilo la Kiislamu. Polisi waliitwa katika eneo hilo la “vita” na baada ya kuangalia kanda ya CCTV walimweleza mwanamke huyo wa Kiislamu kuwa angelipishwa faini ya kroner 1,000 ($155; £120) baada ya kukataa kuvua niqab hiyo kwa agizo la polisi. Kwa sasa faini hiyo imeongezeka mara kumi zaidi hadi kroner 10,000 ($1,500; £1,200) kwa wahalifu wanaorudia kosa.
Wanawake wa Hizb ut Tahrir wanasimama kidete pamoja na dada zetu waliodhulumiwa nchini Denmark ambao wamefanywa kuwa wahalifu kutokana na kutekeleza uhuru ule ule wa kujiamulia na kuwa na fikra huru ambazo zinapaswa kuwa uti wa mgongo wa Demokrasia na hadhara! Utafiti wa polisi una thibitisha kuwa sheria huru za kidemokrasia zinawakilisha tu mkusanyiko wa maadili hatari na ya kinafiki ambayo hayaleti ustawi wa kihakika au usalama kwa watu. Uvunjaji hadhi ya kibinadamu kwa kushambuliwa hadharani kamwe haukuchuliwa kama uhalifu mbaya, bali mwathiriwa alikumbana na adhabu maradufu kwa kuwa “wanawake wote wawili walishtakiwa kwa kuvuruga amani” huku mwanamke yule wa Kiislamu akikabiliwa na shtaka la ziada la “kukiuka sheria dhidi ya vazi linalofinika uso kikamilifu” (ilhali kiuwazi sheria hii haiko!). Katika mfano huu twaweza kuona shambulizi la wazi na la moja kwa moja ambalo limetekelezwa hususan dhidi ya wanawake wa Kiislamu na jinsi sheria za kidemokrasia zinavyo halalisha kulengwa kwao kwa ajili ya uhalifu wa kichuki na kuyadhibiti maisha yao ya kila siku ya kijamii na ya kisiasa. Denmark ni kesi mojawapo ya majaribio ya mtindo wa ukiukaji haki za kibinadamu kwa kisingizio cha “kulinda uhuru” ambao ndio ada ya sasa ulimwenguni. Hatua hizi za kutapatapa za kupitisha sheria na faini zilizopitwa na wakati zinathibitisha pekee kuwa nidhamu ya kisiasa ya Kimagharibi imefilisika kifikra na imepoteza matumaini na kunadi mtazamo wake hadaifu wa ukombozi kwa wanawake wa Kiislamu. Kutokana na maadili huru na harakati za wanawake kuwa katika majaribio kwa miongo mingi iliyopelekea tu vugu vugu la #MeToo linalojumuisha mamilioni na zaidi, wanawake wa Kiislamu sasa wataona waziwazi kuliko mwanzoni kuwa ni nidhamu ya Kisiasa ya Kiislamu pekee ndiyo inayobeba mbinu za hadhi ya kweli, fursa na usalama kwa wanadamu kila mahali. Serikali ya Denmark na vibaraka wake wa kimataifa wanaweza kuongeza faini zao mara 100,000 zaidi ila itawapata wanawake wa Kiislamu daima kuwa tayari kuwa wahalifu wa kurudia makosa katika kuzipa mgongo sheria za kibinadamu na uwezo wao wa kikamilifu wa kujitoa mhanga katika kila hali ya kimaisha katika kumtii Allah (swt) kama mtunzi halali wa sheria kamwe hauwezi kupima kwa thamani yoyote ile. Watawala wa Waislamu katika ardhi zetu ndio wanaopaswa kushtakiwa kwa sifa ya kuwa washirika wa uhalifu kutokana na kimya chao kikuu na utumwa wao muovu kwa watawala wa kikoloni wanaotekeleza unyanyasaji wa mamilioni ya wanawake na watoto wa Kiislamu kila siku. Sisi tunawaambia wote hao kuwa chuma chao kimotoni kwani Allah daima amekuwa akizipa tawala za kiimla mwisho unaostahiki; tawala zisizojua mengine yoyote isipokuwa uongozi wa kimabavu, uongo na ufisadi. Allah (swt) Muumba wa wanadamu anayafahamu yaliyopita, yaliyoko na yatakayokuja ya vitu vyote na akavipa muongozo wa wazi wa namna ya kuikabili mitihani hii mikubwa katika maisha yetu ya kila siku kama Waislamu. Ni rahisi na yenye kuondoa kila mgongano katika hukmu za Kiislamu:
( وَأَنْ اعْبُدُونِي هَذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ )
“Na muniabudu Mimi (ALLAH) hii ndio njia iliyo nyooka.” [36:61]
Ni kwa mtazamo huu safi wa kipekee ambapo kila mwanamke wa Kiislamu anapaswa kushajiishwa nao na ujumbe huu ndio utakaopatikana kikamilifu kwa kurudi kwa nidhamu kamilifu ya kiutawala ya Kiislamu, Khilafah ambapo hatutaona tena wanawake waliovalia kwa heshima wakigeuzwa kuwa wahalifu bali tutawatafuta na kuwaadhibu wakiukaji halisi wa maadili ya kijamii na uvaaji wa kiheshima kwa njia sahihi pasi na mapendeleo au chuki.
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |