Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 23 Muharram 1439 | Na: 1440/003 |
M. Jumatano, 03 Oktoba 2018 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kampeni ya Kimataifa: “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu” iliyo Zinduliwa na Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Mnamo 3 Oktoba, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kilizindua kampeni muhimu ya kiulimwengu kwa anwani, “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu” ambayo itamalizikia katika kongamano la kimataifa la wanawake mwishoni mwa Oktoba litakalo hudhuriwa na wazungumzaji kutoka pembe zote za dunia.
Miundo imara, yenye umoja wa familia ndio kitovu cha mujtamaa imara, zisotingishika, na zenye mafanikio. Ni muhimu mno katika utoaji usaidizi wa kimwili, kihisia, na kimada na kuwepo kwa hali nzuri ya wanachama wake wote na kuhakikisha uchungaji thabiti na ulezi mwema wa watoto. Lakini, leo kuna mgogoro unaoathiri utulivu na umoja wa maisha ya ndoa na familia katika jamii kote duniani, ikiwemo ndani ya biladi za Kiislamu. Kuingizwa kwa thaqafa ya kimagharibi katika ulimwengu wa Kiislamu, pamoja na uharibifu wa uhuru zake za kijinsia zisizo na mipaka, muozo wa nyendo za ubinafsi za kimaisha, maadili ya kimada ya kirasilimali na mtafaruku wa fahamu za utetezi wa kijinsia kama vile usawa wa kijinsia, kupitia majukwaa kama vile sekta ya burudani, nidhamu za elimu, mitandao ya kijamii, na mashirika ya utetezi wa kijinsia yameharibu na kumomonyoa taasisi ya ndoa na kusababisha janga la kuvunjika kwa familia. Hii imechochewa na kupitia kuweko kwa mila za Kiarabu, Kihindi, au Kiafrika zisizokuwa za Kiislamu ndani ya jamii zetu za Kiislamu zinazobeba mitazamo na vitendo vyenye madhara ambavyo vimesababisha mizozo katika maisha ya ndoa na familia. Yote haya, pamoja na ukosefu wa ufahamu safi wa sheria za kijamii za Kiislamu, yamepelekea matarajio maovu katika ndoa, kusababisha kuchanganyikiwa kuhusiana na dori na haki za waume na wake katika maisha ya ndoa na familia, na kupelekea ongezeko kubwa la mahusiano nje ya ndoa, ghasia za kinyumbani na talaka katika jamii za Kiislamu kote duniani. Hii ni pamoja na kusababisha kurefuka kwa umri wa kuoa, kudunishwa kwa cheo cha mama na mgogoro wa uwezo wa kuzaa kutokana na wanandoa kuchagua kuwa na watoto wachache. Kuvunjika huku kwa maisha ya familia katika biladi za Kiislamu kumechangiwa na utawala fisidifu wa serikali za kisekula zisokuwa za Kiislamu katika eneo hilo kupitia upigiaji debe na utekelezwaji wa maadili huru, ya kisekula ya kirasilimali, sera, sheria na nidhamu zinazoeneza fikra na miondoko michafu ya kimaisha ndani ya mujtamaa zao. Fauka ya hao, serikali hizi, pamoja na serikali za Kimagharibi, mashirika ya kimataifa kama UN na harakati za utetezi wa kijinsia zimejiingiza katika mvutano mkubwa ili kubadilisha zaidi familia ya Kiislamu na sheria za kijamii kwa misingi ya uhuru ya kisekula pamoja na kuimarisha maadili huru ya kijinsia na usawa ndani ya jamii za Kiislamu mbazo tayari zishapanda mfadhaiko wa kijamii ndani ya madola. Hali ya kiungo cha familia ndani ya Ummah wa Kiislamu hivyo basi inafuata njia hiyo hiyo ya kimakosa kuelekea katika maangamivu yanayoonekana Magharibi ambako muundo wa familia unayeyuka. Hii ni licha ya kuwa nguvu, umoja na utulivu wa maisha ya familia mwanzoni ilikuwa ni sifa kuu ya Ummah wa Kiislamu.
Ukosefu wa furaha, kuvunjika na kutofanya kazi kwa maisha ya ndoa na familia imesababisha machafuko makubwa ya kihisia kwa wote waliomo na huenda ikawa na athari mbaya zaidi juu ya watoto, watu binafsi na mujtamaa. Hivyo basi ni muhimu sana kutiliwa maanani na kuwa makini katika kuzungumziwa mgogoro huu katika kiungo cha familia na kuiokoa kutokana na maangamivu. Katika kampeni na kongamano hili muhimu, tutaangazia hatari za mabadiliko ya sura ya muundo wa familia katika ulimwengu wa leo. Tutatambulisha mambo makuu yanayodhuru taasisi ya ndoa na utulivu wa maisha ya ndoa, ikiwemo dori ya vyombo vya habari na serikali katika kukoleza mgogoro huu. Tutafichua ajenda za kitaifa na kimataifa za kutia usekula katika familia za Kiislamu na sheria za kijamii ili kuwaeka mbali zaidi Waislamu kutokana na Dini yao. Na muhimu vile vile, tutaangazia nidhamu ya kijamii ya Kiislamu na kuonyesha jinsi mtazamo wake wa kipekee katika kupangilia mahusiano ya kijinsia, kwa misingi yake sahihi, maadili na sheria, ukiwemo ufafanuzi wake wazi wa majukumu ya wanaume na wanawake ndani ya maisha ya familia, unavyo weza kulinda ndoa, kukuza utulivu na maelewano ndani ya maisha ya ndoa, kunyanyua cheo cha mama katika hadhi kuu inachostahiki na kuasisi na kuhifadhi viungo vya familia imara zilizo na umoja. Kampeni na kongamano hili pia litafafanua dori muhimu mno ya usimamizi wa Kiislamu chini ya dola ya Khilafah iliyojengwa juu ya Utume katika kukuza, kupigia debe na kulinda viungo imara vya ndoa na familia ili kuonyesha namna gani Uislamu kihakika ndio ngome ya familia!
Kampeni hii yaweza kufuatiliwa katika:
http://www.hizb-ut tahrir.info/en/index.php/dawah/cmo/16024.html
Ukurasa wa Facebook:
www.facebook.com/WomenandShariah
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |