Jumamosi, 09 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  9 Ramadan 1445 Na: 1445 H / 029
M.  Jumanne, 19 Machi 2024

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waislamu nchini China Wanalazimishwa Kufungua Saumu kwa Pombe na Dada zetu Nguo zao Zinakatwa kuwa Fupi!

(Imetafsiriwa)

Ajenda ya kilimwengu ya kukandamiza kitambulisho cha Kiislamu na kutumia unyanyasaji mkali kwa Ummah wa Muhammad (saw) iko hai na inatumika katika DOAMuslims, tovuti ambayo imebobea katika kunakili dhulma dhidi ya Waislamu, kupakia picha na kunukuu maeneo ambayo wanawake wa Kiislamu wanalazimishwa kukata nguo zao ziwe fupi. Haya ni matusi ya moja kwa moja na unyanyasaji wa kuwadhalilisha wanawake katika kudhihirisha kwao kujisitiri.

Pia kumekuwa na matukio mengi yaliyo nakiliwa ambapo Waislamu wanalazimishwa kufuturu kwa pombe. Vitendo hivi vya kuudhi vinaruhusiwa kutokea kwa vile kuna ufahamu unaojulikana vyema kuwa hakuna kizuizi katika kutusi matendo ya Kiislamu. Wanawake wachamungu wa Kiislamu wameachwa wakipuuzwa na kutelekezwa, kuaibishwa na kuumizwa mikononi mwa maadui wa Uislamu.

Kuna maelfu mengi ya Waislamu katika kambi za kufanyishwa kazi kwa lazima wakipangwa upya kisaikolojia ili kukumbatia maadili yasiyo ya Kiislamu katika mwezi huu wa Ramadhan. Watoto wa Waislamu nchini China mara nyingi huchukuliwa kutoka kwa wazazi wao na kupewa familia zisizo za Kiislamu. Hali hii ya kuudhi imekuwa katika mchakato mbele ya macho ya ulimwengu kwa miaka mingi.

Je, ni Ramadhan ngapi zaidi zitapita huku dada zetu wakilazimishwa kufunga uzazi na kukatazwa kuficha heshima zao hadharani?

Ni viongozi wangapi zaidi watakuja na kuondoka bila kufanya chochote kusaidia mateso na aibu yao? Yuko wapi kiongozi mchamungu, mkweli wa Waislamu wa kuukomboa Ummah kutoka kwa dhalimu wa Shirki!!??

Ni lazima tusimame dhidi ya mifumo inayoruhusu hili kutokea na kufanya kazi kwa kila juhudi ili kusimamisha Khilafah kwani ndio hitaji la dharura zaidi la wakati wetu. Watoto wetu hawawezi kukengeushwa na burudani zisizo na maana za dunia na lazima wakumbushwe wajibu wao wa kufanya kazi kwa namna ya Mtume (saw).

Imarisheni dua kwa dada zetu katika kipindi chao cha mitihani na hatutasahau wajibu wetu wa kufichua ukandamizwaji wao.

[وَالَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ إِلَّا تَفْعَلُوهُ تَكُن فِتْنَةٌ فِي الْأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ]

“Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo fanya hivi itakuwako fitna katika nchi na fisadi kubwa.” [8:73]

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu