Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  3 Shawwal 1445 Na: 1445 H / 032
M.  Ijumaa, 12 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Droni Zilizoundwa Kuua Watoto mjini Gaza

(Imetafsiriwa)

Dkt. Hadi Bedran, daktari (anaesthetist) wa Uingereza, hivi karibuni alifanya mahojiano juu ya kurudi kwake kutoka Gaza, na aliripoti uchunguzi wake kama mtaalamu wa matibabu. Alisema kwamba aliona majeraha ambayo hajawahi kuyaona katika historia ya kazi yake. Watoto wadogo wamekuwa wakija na majeraha ya risasi moja kwa moja usoni ambayo mara nyingi husababisha kuvunjika kwa mafuvu ya kichwa na sehemu za kichwa zilipuliwa kabisa. Risasi hizi hazikufyatuliwa kutoka masafa ya mbali na mlenga shabaha. Ziliripotiwa na mashahidi kufyatuliwa na droni ndogo ya aina ya helikopta ambayo inaweza kuendeshwa kwa mbali na mtu mwengine. Droni hizi zina uwezo wa sauti na wa video ambazo huruka moja kwa moja mbele ya nyuso za watu kwa kiwango chao na huuliza maswali. Pia hutoa hata maagizo kama “Nenda Kusini, ondoka katika eneo hilo nk ...”. Wakati wowote, droni hizi zinaweza kusababishwa kufyatua risasi kwa wahasiriwa bila kutoa hatari kwa mtu anayeziendesha.

Madaktari wa upasuaji wanaowashughulikia wale ambao wamenusurika mashambulizi kama haya ya droni wamesema kwamba majeraha ya risasi ni tofauti na kitu chochote ambacho wamewahi kuona hapo awali. Kipengele cha kipekee ni kwamba hulipuka nje, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa mwili; Kamwe sio tu majeraha ya kuingia na kutoka. Aliripoti pia kuwa wafanyikazi katika eneo hilo walimwonya asiitazame droni ya helikopta kwani imetengenezwa na utambuzi wa nyuso wa AI, na huenda akapigwa risasi mara moja. Ugunduzi muhimu katika wakati wake alipokuwa anafanya kazi katika hospitali ni kwamba droni hizi zinalenga watoto wanaocheza kwa hivyo walio hatarini zaidi na wasio na hatia wao ndio waliokuwa idadi kubwa ya wahasiriwa.

Hii ni sura nyingine ya uoga na hofu wanayopitia watoto wetu huko Gaza! Je ni majeraha ya aina gani kina mama wa Ummah wanatarajia kukabiliana nayo wakati kucheza kukiwa ni jambo la uhai na kifo? Wakati huo huo, watawala na serikali za ulimwengu wa Waislamu wanaendelea kufumbia macho udhalimu huu wa kutisha unaotekelezwa dhidi ya Waislamu wa Gaza, kuendelea na makubaliano yao ya amani, uhalalishaji mahusiano, na mafungamano ya kibiashara na kidiplomasia na umbile hili la mauaji la Kiyahudi. Ardhi ya Palestina kamwe haitakombolewa na ndugu na dada zetu kamwe hawatalindwa wakati watawala hawa wasaliti wangali wako!

Tunawauliza watoto wa majeshi ya Waislamu, ni kiasi gani cha jinai ya kutochukua hatua kwa watawala hawa wa waoga ambao mnawatumikia mnaweza kushuhudia wakati mnajua kuwa mna uwezo wa kijeshi wa kumaliza mauaji haya ya ndugu na dada zenu?!! Damu yenu hakika inachemka kwa hasira kwa kiwango cha kutisha cha mateso Waislamu wa Gazan wanavumilia, huku mukilazimishwa kubaki kwenye kambi zenu na viongozi hawa wanaounga mkono Mayahudi! Ummah wenu kote ulimwenguni unakulilieni kujibu amri ya Mola wenu (swt) kuwatetea Waislamu wa Palestina na kuikomboa Ardhi hii Iliyobarikiwa kutokana na uvamizi huu wa mauaji ya halaiki milele. Tunakulinganieni kuvunja utiifu wenu kwa hawa mafirauni wa zama hizi ambao wameutelekeza Ummah wenu, wameisaliti Dini yenu, na wakaliletea aibu jina lenu. Ving’oeni viti vyao vya utawala na mutoe Nusrah yenu (msaada wa kimada) kwa ajili ya kusimamisha uongozi wa Kiislamu, mfumo na dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambao utakumbatia dori yenu ya kweli kama watetezi wa Waislamu na Uislamu, na wakombozi wa ardhi zetu. Fuateni nyayo za kamanda mtukufu Salahuddin Ayubi na mupate heshima kubwa ya kuwa wakombozi wa Al Aqsa na Ardhi nzima Iliyobarikiwa ya Palestina!

[فَلْيُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللّهِ الَّذِينَ يَشْرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالآخِرَةِ وَمَن يُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللّهِ فَيُقْتَلْ أَو يَغْلِبْ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا]

Basi nawapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanao uza uhai wa dunia kwa Akhera. Na anaye pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kisha akauliwa au akashinda basi tutakuja mpa ujira mkubwa.” [An-Nisa:74]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu