Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  8 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 H / 039
M.  Alhamisi, 16 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, haijatosha Kwenu kuwa Wanyonge na Watiifu?!
(Imetafsiriwa)

Katika siku ya 220 ya uvamizi wa umbile la Kiyahudi dhidi ya Ukanda wa Gaza, mashambulizi ya angani yaliendelea kwenye kambi ya Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Vikosi vya uvamizi vilifyatua risasi nyingi kwenye vituo vya makaazi katika kambi hiyo kabla ya kuwalazimisha mamia ya Wapalestina kuondoka katika vituo hivyo. Pia vilizidisha mashambulizi yake ya anga kwa Rafah, ambayo imejaa mamia ya maelfu ya wanaume na wanawake waliokimbia makaazi yao, ikiwa ni pamoja na kulipua nyumba juu ya vichwa vya wakaazi wao bila onyo la kabla. Katika muda wa chini ya saa 72, viliua wakaazi 40, wakiwemo watoto 13 na wanawake 12.

Kuongezeka kwa uvamizi kwenye nyumba za makaazi kunasadifiana na kushamiri kwa makombora yaliyolenga eneo la mashariki wa Rafah kama sehemu ya operesheni ya vitisho, mauaji na uharibifu wa kiholela dhidi ya raia, ili kuwasukuma kulazimika kuhama tena kutoka kwa mji huo, ambao ni makaazi ya angalau watu milioni 1.3 waliokimbia makaazi na wakaazi.

Makumi ya maelfu ya watu walihamishwa kutoka mji wa Rafah, hadi eneo la Al-Mawasi, magharibi mwa mji na magharibi mwa Khan Yunis, ambayo ilisababisha msongamano mkubwa katika eneo hili dogo (kama dunum elfu 12), huku watu waliohamishwa wakikimbilia kuweka mahema au vifuniko vya nailoni chini, kando ya barabara, na pwani, bila kuwa na mahitaji ya maisha, na bila eneo hilo kuwa na miundombinu ya kutosha kukidhi mahitaji ya mamia ya maelfu ya wakaazi. Hii inawaathiri hasa wanawake na watoto ambao hawajui waelekee wapi na wafanye nini kuhusu sera ya mauaji ya halaiki, kuleta madhara makubwa ya kimwili na kisaikolojia, uharibifu mkubwa wa nyumba, miundombinu na mahitaji ya maisha, njaa, kiu, kunyimwa matibabu, na kuwasukuma kuyahama makaazi yao katika mazingira ambayo yanakosa haki za kimsingi kabisa za binadamu, na kisha kuwalenga na kuwaua katika sehemu ya kimbilio lao.

Mashambulizi ya angani na mizinga yanaendelea katika eneo lote la Ukanda wa Gaza dhidi ya nyumba na makundi yaliyokimbia makaazi yao. Idadi ya vifo iliongezeka hadi zaidi ya mashahidi 35,000 na zaidi ya majeruhi 78,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na bado kuna mazungumzo ya maelfu ya miili ya mashahidi chini ya vifusi.

Mauaji haya ya halaiki yamekuwa yakifanyika kwa zaidi ya miezi saba chini ya macho ya ulimwengu mzima, kwa kuzingatia kinga inayotolewa na Marekani na uzembe na utiifu wa nchi za Ulaya na za Kiarabu  kwa umbile la Kiyahudi, hazithubutu hata kukemea kile kinachotokea. Utawala wa Misri unasimama na kutazama, hata kusaidia uvamizi huo kupata udhibiti kamili wa kivuko cha Rafah kilicho karibu na mipaka yake!! Kivuko hiki ni njia ya maisha kwa watu wa Ukanda wa Gaza, na bandari pekee ya nchi kavu kwa kuleta chakula na misaada ya matibabu na kuwaondoa waliojeruhiwa. Kwa hiyo, harakati kupitia humo zimesimama kabisa, kwani hakuna usafiri au kuingia kwa msaada ambao tayari ni adimu katika Ukanda wa Gaza. Pia tuliona makumi ya wanawake na watoto waliojeruhiwa ambao hawakuweza kupata matibabu, dawa, au madaktari.

Enyi Majeshi na Maafisa wa Ummah: Hatutachoka na wala hatutachoshwa kuwalingania nyinyi na kuwasihi muwaondolee watu wa Gaza mateso yao, na kuiondolea Masra (mahali pa Isra) ya Mtume Mwenyezi Mungu (saw) na Palestina yote kutoka kwenye mshiko wa uvamizi huu wa kikatili. Hili halitatokea huku watawala hawa wakiwa wamejikunyata juu ya kifua cha Ummah, basi asini dhidi yao na waondoeni kwenye viti vyao vyenye kutu, vilivyooza (vya madaraka) vilivyojaa damu, viungo vya mwili, maombolezi na vilio vya wanawake na watoto huko Gaza, au sauti zao hazijakufikieni?! Je, hamkuona kwa macho yenu maovu waliyofanyiwa?! Wallahi munangoja nini zaidi?! Je, hamkutikiswa na nguvu ya imani ya watu wa Gaza na imani yao juu ya ushindi wa Mwenyezi Mungu?! Je, hazikusukumini Aya za Mwenyezi Mungu, Mtukufu anaye sema:

[أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِنْهُمْ فَاسِقُونَ]

“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu.” [Al-Hadid: 16]?!

Imetosha kwenu kuwa wanyonge na watiifu. Basi, songeni hadi kwenye msimamo unaomridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, ili mupate kheri ya dunia hii na Akhera.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu