Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kyrgyzstan

H.  14 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 H / 06
M.  Jumatano, 22 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ghasia jijini Bishkek na Matokeo yake
(Imetafsiriwa)

Wizara ya Afya iliripoti kwamba watu 29 walijeruhiwa wakati wa ghasia zilizotokea jijini Bishkek, mji mkuu wa Kyrgyzstan, usiku wa Mei 18. Ubalozi wa Pakistan ulithibitisha kuwa raia 14 wa Pakistan walijeruhiwa katika ajali hii.

Maafisa kadhaa, wakiongozwa na Rais, walitoa taarifa rasmi kuhusu tukio hili. Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alitangaza kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba alikuwa akifuatilia tukio hilo kwa wasiwasi. Mnamo siku ya Jumamosi, serikali ya Pakistan iliwaregesha makwao raia wapatao 180 kutoka Kyrgyzstan hadi Pakistan, na kupanga safari za ndege maalum kwa wale wanaotaka kuondoka.

Tukirudi kwenye ratiba ya tukio lililosababisha ghasia, Mei 13, mzozo ulizuka kati ya raia wawili wa Misri na vijana wanne wenyeji wa nchi hii. Vijana hao wa nchi hii kisha waliwafuata wanafunzi hao wa kigeni hadi kwenye bweni lao na vita vikatokea, hali iliyopelekea kupigwa na wanafunzi hao wa kigeni. Baada ya video inayoonyesha tukio hili kuenea mtandaoni, usiku wa Mei 17-18, mamia ya vijana wenyeji wa nchi kwa pamoja waliwapiga raia wa kigeni katika makaazi yao.

Ingawa tukio hili lilisababishwa na kiasi kidogo cha machafuko, hakuna shaka kwamba kulikuwa na nguvu ambazo zilijaribu kulitumia kwa manufaa yao wenyewe. Hasa, makundi ya upinzani yalisambaza nyenzo za kuchochea utaifa na kueneza habari za uongo juu ya tukio hilo lililosababisha vifo vya watu. Lengo lao lilikuwa kuzidisha kulaani kwa vijana waliokusanyika na kuwageuza dhidi ya mamlaka.

Kwa upande mwingine, mamlaka ilijiepusha kuwakamata raia waliofanya uhalifu huo ili kudhibiti hisia za umati, na kutoa hoja ya hili kwa kusema kwamba walitekeleza matakwa ya vijana, au tuseme walichukua hatua dhidi ya wageni haramu.

Serikali ilikuwa imepiga marufuku rasmi shughuli za jukwaa la TikTok nchini, kwa hofu kwamba vijana kama hao wangeungana na maandamano nchini yangegeuka dhidi ya serikali, kwa sababu habari, na haswa, nyenzo za video vinavyoenea haraka kwenye jukwaa hili, imekuwa ndio chombo kikuu cha kuunda upinzani na rai jumla.

Kwa upande mwingine, tukio hili lilikuwa somo kubwa kwa serikali, kwa sababu, ingawa serikali ilikuwa imekandamiza koo nyingi na wanasiasa hadi sasa, imejulikana kuwa taasubi ya vyombo vya sheria juu ya maandamano ya umma ilikuwa dhaifu. Kwa usahihi zaidi, serikali ilishuhudia kwamba juhudi zake kwenye njia ya udikteta hazikuzaa matunda. Kwa hivyo, Rais Japarov alisisitiza katika hotuba yake rasmi kwamba vyombo vya utekelezaji sheria vitachukua hatua kali ikiwa ghasia kama hizo zitatokea tena.

Kwa hakika, maandamano ya wakaazi hayakuhusiana tu na ghasia zilizotokea Mei 13. Kwa usahihi zaidi, kutoridhika kwa watu kunaongezeka dhidi ya mabepari wanaotumia nguvu kazi ya bei nafuu ya wahamiaji wa kigeni ili kupata faida zaidi, kwa sababu waajiri ambao wanazingatia faida kama kipimo cha maisha yao wamezoea kuleta wafanyikazi kutoka nje ya nchi kwa nusu ya mishahara wanayolipa wanati. Hali hiyo imekuwa ya kawaida katika mfumo wa kibepari. Haitakuwa ni makosa kusema kwamba tukio lililotokea Mei 18 lilikuwa dhihirisho la kulaani kwa wananchi dhidi ya utawala huu wa dhulma.

Bila shaka, hakuna shaka kwamba fikra ya utaifa, ambayo ni uwanja wa mfumo fisadi wa kibepari, ina mchango mkubwa katika tukio hili. Wakoloni walizigawanya nchi za Kiislamu katika vijidola vidogo vya kitaifa, baada ya kuvunjwa Khilafah, na waliimarisha utaifa na uzalendo ili kudumisha ushawishi wao huko. Walilenga kudhibiti watu chini ya ushawishi wao kwa kuwagombanisha wao kwa wao. Tuliona hili katika migogoro ya kikabila iliyoandaliwa na Urusi katika kipindi cha 1990-2010 katika nchi yetu.

Kwa hiyo, Waislamu lazima waathiriwe na kila tukio kwa msingi wa imani yao, ili matendo kama hayo mabaya yasijirudie. Kwa maana nyengine, mzozo au ugomvi baina ya watu wawili haupaswi kutatuliwa kwa mtazamo wa utaifa, bali unatakiwa utokane na mtazamo wa Kiislamu unaotokana na Qur’an na Sunnah, kwa sababu Uislamu unaipinga fahamu hii ya kabla ya zama za Uislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ» “Si katika sisi mwenye kulingania wengine katika ukabila” Na akasema: «دَعُوهَا، فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ» “Uwacheni hakika huo ni uvundo.” Na Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوباً وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ]

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” [Surah Al-Hujuraat: 13]

Lakini hii haimaanishi kuwa Muislamu anachukia jamaa zake na jamii anayoishi ndani yake. Kinyume chake, Uislamu unaamrisha mahusiano mema na familia na jamii, na Mwenyezi Mungu Mtukufu alitahadharisha juu ya kukata kizazi katika Sura An-Nisa.

Fahamu ya utaifa ambayo imeharamishwa katika Uislamu ni fahamu iliyojengwa kama badali ya fahamu ya udugu wa Kiislamu, na wale tu walio na utaifa mmoja ndio wanaolindwa, bila kujali wao ni wako sawa au la. Wale wenye fahamu hii wanataka tu watu wao wawe ndio viongozi juu ya watu wengine wote, na wanaweka maadili ya watu wao juu ya kila kitu chengine, na kwa mtazamo wao, watu wao ni bora kuliko Waislamu wengine, hata kama wanafanya uhalifu.

Enyi Waislamu! Kataeni fikra ya utaifa wa Jahiliyah, bali shikamane na Aqida ya Kiislamu (mafundisho) inayowachukulia Waislamu wote, kizazi cha Adam, kama ndugu! Hasa, acheni mfumo fisadi wa kibepari, ambao uliasisi mipaka bandia kati ya watu wawili ndugu na kuwafanya Waislamu kuwa maadui wao kwa wao. Imani yetu haichukulii vita vya Palestina kuwa ni tatizo la Wapalestina, wala umaskini wa Pakistan kuwa ni tatizo la Wapakistani, wala matatizo ya Kyrgyzstan kuwa ni matatizo ya watu wa Kyrgyz pekee! Kinyume chake, inaamini kwamba tatizo la Muislamu yeyote katika uso wa ardhi ni tatizo la Ummah.

Enyi watawala katika nchi za Kiislamu! Ni lazima pia mutatue matatizo ya Ummah. Badala ya kuwasifu watu wenu na kutoa taarifa, inukeni mutatue matatizo ya Ummah mzima, achaneni na mabaki ya utaifa, na angamizeni mipaka bandia iliyochorwa na wakoloni! Si ajabu kwamba kazi yenu hii itakuokoeni hapa duniani na kesho Akhera!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kyrgyzstan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-turkiston.net
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu