Ijumaa, 03 Rajab 1446 | 2025/01/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kyrgyzstan

H.  24 Jumada II 1446 Na: H 1446 / 03
M.  Alhamisi, 26 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tukio la Jalalabad: Kuilinda Dawah ni Wajibu kwa Kila Mmoja Wetu
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 26 Novemba, Mashababu wa Hizb ut Tahrir waliandaa amali dhidi ya rasimu ya sheria ya “Uhuru wa Dini na Mashirika ya Kidini” katika eneo la Jalalabad. Wiki tatu baadaye, kati ya Disemba 10 na 14, Kamati ya Serikali ya Usalama wa Kitaifa ilifanya msako katika nyumba 21 katika eneo hilo na kuwaweka kizuizini kinyume cha sheria wanachama wa Hizb ut Tahrir. Vikosi vya usalama havikuruhusu wanachama waliozuiliwa (Mashababu) kukutana na mawakili wao na badala yake walifanya uchunguzi mbele ya mawakili waliofunzwa mahususi kwa kesi hii. Kutokana na hali hiyo, Mashababu wetu walizuiliwa kwa muda kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa kisingizio cha kusambaza vipeperushi misikitini vinavyopinga sheria hiyo. Kesi ya jinai ilifunguliwa dhidi yao chini ya shtaka la “kuandaa na kuendesha shughuli za itikadi kali.” Hata hivyo, hakuna ushahidi wala ripoti ya kamati ya wataalamu iliyowasilishwa kuhalalisha kukamatwa kwa watu hao. Miongoni mwa waliozuiliwa ni Muradullah, Ali Sher, Manas, Abdul Rahim, mwengine ni Abdul Rahim, Ravshanbek, Nasibbek, Rasulbek, Temirlan, Karimjan, Mirzahid, Abdul Moqim, Bahadir, Sharif, Abdul Qadir na wanawe wawili, na Karim akiwa na mwanawe.

Vikosi vya Usalama wa Taifa vilichukua hatua kubwa wakati wa kukamatwa kwa Mashababu wa Hizb, kana kwamba walikuwa wakiwakamata wahalifu hatari, wafisadi, au wauaji. Kupitia hili, walijaribu kuwaonyesha Mashababu wa Hizb kama wahalifu wabaya mno! Kiuhalisia, hatua hii ya serikali si chochote ila ni kuwahadaa watu, kwani hakuna ufafanuzi wa wazi wa msimamo mkali uliokubaliwa na mfumo wa kimataifa. Kila serikali inafafanua msimamo mkali kulingana na maslahi yake. Kwa mfano, Urusi na China zimefafanua kivyao msimamo mkali ndani ya mfumo wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai. Amerika imefafanua kwa njia tofauti, kama vile nchi za Ulaya, kila moja ikitenda kulingana na ufafanuzi wao. Hata hivyo, fasili hizi zote zinashirikiana sifa moja: “Msimamo mkali ni kutafuta mamlaka kupitia mbinu kali.” Kwa kuzingatia hayo, Kyrgyzstan imeitangaza Hizb ut Tahrir kuwa shirika lenye misimamo mikali, huku baadhi ya nchi nyingine zikilitaja kuwa shirika la kigaidi. Hata hivyo, mtu yeyote aliye akili razini anaweza kutambua kwa urahisi, kupitia kuunganisha mambo kwa usahihi, kwamba huo ni uchonganishi tu. Kwa mfano, serikali ya Kyrgyzstan imebadilika mara tatu, kulingana na ufafanuzi wao au, badala yake, kwa njia ya “radikali”. Hata hivyo, Hizb haikushiriki katika lolote kati ya vitendo hivi, kwani inashikamana tu na njia ya Mtume Muhammad (saw).

Mashababu hawa walikamatwa kwa sababu walifikisha Uislamu kwa kufuata njia ya Kiislamu. Walifichua kusudi la rasimu ya sheria kuhusu “Uhuru wa Dini na Mashirika ya Kidini” na wakazungumza ukweli ambao wengi wanaogopa kuusema. Kupitia sheria hiyo mpya, serikali inaweka vikwazo katika njia ya kulingania Uislamu, kuamrisha mema, na kukataza maovu, huku ikiweka vikwazo zaidi kwa wahubiri. Zaidi ya hayo, rasimu ya sheria hiyo inajumuisha hatua dhidi ya elimu ya Kiislamu katika misikiti, shule, na duara za masomo, na vile vile dhidi ya mahubiri ya mtandaoni.

Ilikuwa ni wajibu juu ya wanazuoni kusema ukweli, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«العُلَمَاءَ وَرَثَةُ الأَنْبِيَاءِ، وَإِنَّ الأَنْبِيَاءَ لَمْ يُوَرِّثُوا دِينَاراً وَلَا دِرْهَماً، إِنَّمَا وَرَّثُوا العِلْمَ، فَمَنْ أَخَذَهُ أَخَذَ بِحَظٍّ وَافِرٍ»

“Wanachuoni ni warithi wa Mitume, na Mitume hawakuacha nyuma dinari wala dirham, bali walirithi elimu, basi mwenye kuichukua itachukua sehemu.” Kwa hiyo, kuwalinda Mashababu wanaoitetea dini yetu na kuunga mkono amali zao kimsingi ni jukumu la wanazuoni wetu. Kwa sababu wabebaji da’wah hawa wanakamatwa na kukandamizwa kwa sababu za kisiasa kwa ajili ya maslahi Umma. Familia za walinganizi hao watapata malipo makubwa kwa ajili ya subira yao, Mwenyezi Mungu akipenda, kwa sababu wameyaamini kabisa maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«لاَ تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي عَلَى الْحَقِّ ظَاهِرِينَ لَعَدُوِّهِمْ قَاهِرِينَ لاَ يَضُرُمْمُمْ فَرَّمْ فَعَدُوِّهِمْإِلاَّ مَا أَصَابَهُمْ مِنْ لَأْوَاءَ حَتَّى يَأْتِيَهُمْ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ كَذَلِكَ»

“Kipote miongoni mwa Umma wangu hawataacha kusimama na haki wakiidhihirisha kwa adui yao wakiitawalisha, mashambulizi ya adui yao hayatawadhuru kitu isipokuwa masaibu tu. Mpaka amri ya Mwenyezi Mungu iwafikie na wao wako katika hali hiyo.” (Imesimuliwa na Abu Dawood na Ahmad)

Mtume (saw) pia amese: «بَدَأَ الْإِسْلَامُ غَرِيباً وَسَيَعُودُ غَرِيباً كَمَا بَدَأَ فَطُوبَى لِلْغُرَبَاءِ» “Uislamu ulianza ukiwa mgeni na utarudi katika hali ulioanzia ya kuwa mgeni. Basi bisha njema ni kwa wale watakaoonekana wageni (kwa kushikamana nao)” قيل: يا رسول الله من الغرباء؟ ikaulizwa, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni kina nani hao wageni?” Akasema: «الَّذِينَ يُصْلِحُونَ إِذَا فَسَدَ النَّاسُ» “Wale watakaorekebisha mambo pindi watu wanapofisidika,” na katika riwaya nyengine: «الَّذِينَ يُصْلِحُونَ مَا أَفْسَدَ النَّاسُ مِنْ سُنَّتِي» “Wale watakaorekebisha yale waliyoyafisidi watu katika Sunna” na pia katika riwaya nyengine: «الَّذِينَ يُحْيُونَ مَا أَمَاتَ النَّاسُ مِنْ سُنَّتِي» “Wale watakaohuisha zile Sunna zangu walizoziua watu.”

Kwa hivyo, sera za ukandamizaji na vitisho hazitavunja azimio la Mashababu wa Hizb utTahrir katika misheni yao ya kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu, na wala haziwezi kuzima mihemko mikali katika nyoyo zao. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ]

“Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!” [As-Saff: 13].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kyrgyzstan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-turkiston.net
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Ghasia jijini Bishkek na Matokeo yake

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu