Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
H. 27 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: H 1446 / 06 |
M. Jumatatu, 23 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Na Mwenyezi Mungu si mwenye Kughafilika na Wanayoyafanya Madhalimu
(Imetafsiriwa)
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
[وَلَا تَحْسَبَنَّ اللهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ]
“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Ibrahim:42].
Tunaona kwamba vyombo vya usalama vya dola nchini Kyrgyzstan vinawakamata wahalifu ambao wamefanya uhalifu mbalimbali, na baadhi yao walishtakiwa kuwa katika genge la wahalifu, huku wengine wakishtakiwa kwa hongo, mauaji, na mashtaka mfano wa hayo. Ikiwa kweli wanahusika katika uhalifu huo, basi wanachukuliwa pia kuwa wahalifu kwa mujibu wa Shariah ya Kiislamu. Lakini wakati huo huo, tunashuhudia kwamba kuna wafungwa ambao hawakufanya kitendo chochote cha jinai, bali walikamatwa kwa sababu tu ya kulingania dini ya Mwenyezi Mungu na kwa kusema: “Mola wetu ni Mwenyezi Mungu”! Na pia wanakamatwa kikatili mithili ya wahalifu wa kweli na kutupwa magerezani ambako hupigwa sana na mbinu nyingine za "kisasa" za mateso. Hawa ni wanachama wa Hizb ut Tahrir, na madhalimu ni maafisa wa serikali na vyombo vyao vya usalama.
Dola za kikoloni za kikafiri za Kimagharibi, ambazo kwa sasa zinatawala dunia, zilibuni simulizi kama vile "ugaidi" na "itikadi kali" ili kupigana na Uislamu. Na katika nchi za Kiislamu, watawala vibaraka wa Waislamu walitoa sheria za kupambana na ugaidi na misimamo mikali ili kuwafurahisha mabawana zao makafiri. Matokeo yake, wale wanaolingania dini ya Mwenyezi Mungu nje ya “mfumo” uliowekwa na dola za kidemokrasia za kisekula wanachukuliwa kuwa “wahalifu” na kupachikwa jina la magaidi na watu wenye msimamo mkali.
Kiuhalisia, mapambano ya madhalimu dhidi ya dini ya Mwenyezi Mungu yamekuwepo tangu zamani. Mojawapo ya mifano mashuhuri ni kisa cha Firauni kama kilivyotajwa katika Qur’an Al-Karim. Firauni alikuwa na kiburi katika utawala wake na kiburi chake kilifikia hatua ya kudai uungu:
[فَحَشَرَ فَنَادَى * فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمْ الْأَعْلَى]
“Akakusanya watu akanadi * Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.” [An-Nazi'at:23-24].
Na viongozi wa dola za kikafiri leo hawana tofauti na Farauni. Katika zama za Firauni, wachawi waliona muujiza wa Musa (alayh as-Salam) na wakamuamini, na Firauni akawaambia:
[آمَنْتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ]
“Oh! Mnamuamini kabla sijakupeni ruhusa?” [Ta-Ha:71].
Na viongozi wa leo wa ukafiri wanawafundisha watu kuamini chochote kinachoendana na matamanio yao, na wanasema: "Mtu yeyote anaweza kuamini dini yoyote anayoichagua. Yeyote anayetaka kuabudu moto, masanamu, au Mwenyezi Mungu peke yake - basi afanye hivyo, mradi ni kwa mujibu wa uhuru wa imani na ndani ya mfumo wa sheria za kidemokrasia, na kwamba ibada za kidini na kushikamana na dini vinawiana na kanuni za kidemokrasia." Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[قَالَ فِرْعَوْنُ مَا أُرِيكُمْ إِلَّا مَا أَرَى وَمَا أَهْدِيكُمْ إِلَّا سَبِيلَ الرَّشَادِ]
“Firauni akasema: Sikupeni shauri ila ile niliyo iona, wala sikuongozeni ila kwenye njia ya uwongofu.” [Ghafir:29].
Na Firauni akawatishia wachawi kwa adhabu kwa kuasi amri zake na akawaahidi kifo na kusulubiwa baada ya mateso. Alisema:
[فَلَأُ قَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ مِنْ خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ وَلَتَعْلَمُنَّ أَيُّنَا أَشَدُّ عَذَاباً وَأَبْقَى]
“Basi kwa yakini nitakukateni mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakutundikeni misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu na kuiendeleza adhabu yake.” [Ta-Ha:71]. Firauni aliwauwa wachawi kama alivyosema, lakini walisimama imara katika imani yao mpaka wakakutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu kama mashahidi. Vitisho vya Firauni havikuwageuza kutoka katika kufuata haki na kubaki imara juu yake. Kwa hivyo, adhabu ya Firauni ilikuwa dhaifu mbele ya imani ya Waumini, na Firauni akabaki hoi mbele ya haki na imani.
Hakika, Mwenyezi Mungu anawajaribu madhalimu leo—kama vile Donald Trump, Vladimir Putin, na Xi Jinping—kwa nguvu zao na ukubwa wa mamlaka yao kama vile alivyomjaribu Farauni katika historia. Hivyo basi, kiburi chao ni sawa na kiburi cha Firauni, na adhabu yao itakuwa sawa. Lakini Uislamu unaondoa kiburi na jeuri zao kwa sababu ulikuja kuondoa ufisadi wa watu kama hao na kuwaokoa wanadamu na dhulma za watu kama wao.
Hii ndiyo hali ya madhalimu wakubwa katika nchi za Magharibi. Lakini watawala wetu wanajaribu kufikia kitu gani kwa kuupiga vita Uislamu, hali wao hawamiliki yale waliyokuwa nayo madhalimu wakubwa? Kwa nini wanaiuza dini yao kwa ajili ya maisha ya dunia ya mabwana zao makafiri? Je, wanasaliti dini yao kwa ajili ya mamlaka hayo madogo ambayo mabwana zao wanayadhihaki kwa kusema: “Yatatoweka kwa pigo moja tu”!?
Ndiyo, kuna msukumo wa ndani kwa wanadamu kutafuta utawala, na msukumo huu ni sehemu ya silika (ghariza) inayohusiana na kuhifadhi maisha. Na ikiwa silika hazidhibitiwi na maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, zinapelekea kwenye upotofu. Mara nyingi tunasikia viongozi wa serikali wakidai kuwa wanatumikia wananchi, huku uhalisia ukiwa wanawatumia ili kufikia madaraka na kuyadumisha. Kwa hivyo, msaada wowote rahisi unaotolewa kwa watu nje ya asili ya kibinadamu hauzingatiwi kuwa huduma katika ngazi ya serikali. Mambo ambayo yanaonekana kuwa ya maendeleo katika ngazi ya dola si chochote zaidi ya huduma zinazotolewa ili kuimarisha serikali.
Enyi maafisa, ndio, hamkuingia madarakani kwa nia ya kutabikisha hukmu za Uislamu—bali fikirieni juu ya hilo: Mafarauni na mabeberu walipitia historia, na walitawala kwa miaka michache tu, lakini adhabu yao katika Jahannam itakuwa ya milele, na utawala wenu hautalingana na wao, lakini tahadharini huenda adhabu yenu ikafanana na yao.
Mumewakamata Waislamu na kuwatesa. Tuseme mumewaondoa baadhi yao kwenye misimamo yao, mutapata nini kwa kitendo hiki? Je, munafikiri kwamba mutawafurahisha mabwana zenu makafiri? Je, hamjifunzi kutokana na hatima ya wenzenu kama Saddam Hussein, Muammar Gaddafi, na Bashar al-Assad? Je, munafikiri kwamba munawafurahisha watu walio wengi? Akayev, Bakiyev, na wengine pia walifikiri wangeweza kuwafurahisha wengi hao. Mujtamaa huu ulilelewa juu ya ubepari, na isipokuwa makafiri wanufaike kutoka kwenu mara kwa mara, hawataridhishwa nanyi kamwe!
Zaidi ya hayo, hamtaweza kuwaondoa wahubiri wote kwenye misimamo yao. Waumini walio imara katika imani na misimamo yao daima hubakia mpaka Yawm Al-Qyamah (Siku ya Kiyama), ingawa idadi yao inatofautiana kulingana na zama. Akifa wa mwisho wao, basi Kiyama kitasimama. Lakini katika zama hizi Uislamu unaporegea na nyayo za Dola ya Kiislamu zikisikika—kama alivyoahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akatoa bishara njema—endapo mtu atajiondoa kwenye msimamo wake, maelfu huapa kutojiondoa; na mtu akiuawa shahidi, maelfu humfuata, wakingoja kuuawa shahidi. Na mumeliona hili katika mifano ya mashahidi iliyowasilishwa na Hizb ut Tahrir mpaka sasa.
Mpaka lini mtaendelea kung'ang'ania sheria mlizozipitisha katika kupiga vita Uislamu kwa ajili ya mabwana zenu wa makafiri? Jana, muliwatangaza Taliban kama "magaidi" kwa kuwafuata mabwana zenu. Na leo, munaitambua serikali ya Taliban, pia kwa kuwafuata mabwana zenu. Je, hamuwezi kufanya hivyo kwa mapenzi yenu wenyewe? Je, pia hamuna uhuru wa kuacha kuwakamata vijana wanaoamrisha mema na kukataza maovu?!
Enyi maafisa wa serikali, tunapenda kukumbusheni yafuatayo kama ndugu zenu Waislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[فَوَيْلٌ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ]
“Ole wao walio dhulumu kwa adhabu ya siku chungu.” [Az-Zukhruf:65]. Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika Hadith tukufu: : «يَا عِبَادِي إِنِّي حَرَّمْتُ الظُّلْمَ عَلَى نَفْسِي وَجَعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّمًا فَلَا تَظَالَمُوا» “Enyi waja wangu, hakika mimi nimeiharamishia nafsi yangu dhulma na nimeiharamisha baina yenu, basi msidhulumiane.” Na akasema (saw) pia: «اتَّقُوا الظُّلْمَ فَإِنَّ الظُّلْمَ ظُمَاتٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ» “Iogopeni dhulma, kwani dhulma itageuka kuwa giza kubwa Siku ya Kiyama” Hivyo basi, enyi maafisa wa serikali na wanachama wa asasi za usalama, tubieni kwa Mwenyezi Mungu kutokana na ukandamizaji wenu wa Mashababu wa Hizb utTahrir. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[إِلَّا مَنْ ظَلَمَ ثُمَّ بَدَّلَ حُسْناً بَعْدَ سُوءٍ فَإِنِّي غَفُورٌ رَحِيمٌ]
“Lakini aliye dhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya ubaya, basi Mimi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.” [An-Naml:11]
Na sasa, ujumbe wetu kwa Waislamu wa Kyrgyzstan, ambao wanashuhudia dhulma hii, na ambao ni sehemu ya Umma wa Muhammad (saw) Enyi Waislamu, ikiwa hamtaiwajibisha serikali kwa dhulma yake, basi kiburi chake, dhulma yake, na udhalimu wake vitaongezeka. Na mwishowe dhulma na udhalimu wake vitaingia ndani ya nyumba ya kila mmoja wenu.
Zaidi ya hayo, katika kisa cha Farauni kilichotajwa hapo juu, kuna funzo kwenu pia, pamoja na maafisa wa serikali. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ * فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفاً وَمَثَلاً لِلْآخِرِينَ]
“Walipo tukasirisha tuliwapatiliza tukawazamisha wote! * Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye.” [Az-Zukhruf:55-56]. Na Yeye (swt) amesema:
[وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]
“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Anfal:25]. Zaidi ya hayo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «إِنَّ اللهَ لَا يُعَذِّبُ الْعَامَّةَ بِعَمَلِ الْخَاصَّةِ حَتَّى يَرَوُا الْمُنْكَرَ بَيْنَ ظَهْرَانَيْهِمْ وَهُمْ قَادِرُونَ عَلَى أَنْ يُنْكِرُوهُ فَلَا يُنْكِرُوهُ، فَإِذَا فَعَلُوا ذَلَكَ عَذَّبَ اللهُ الْخَاصَّةَ وَالْعَامَّةَ» “Hakika Mwenyezi Mungu hawaadhibu watu wote kwa matendo ya kundi makhsusi mpaka wauone uovu ulio miongoni mwao na waweze kuukataa, lakini wao hawaukatai. Wakifanya hivyo, Mwenyezi Mungu huwaadhibu lile kundi makhsusi na wote kwa jumla.”
Kwa ajili hii, Enyi Waislamu wa Kyrgyzstan, Enyi wana wa Umma bora uliotolewa kwa ajili ya wanadamu, tunawalingania nyinyi kusimama dhidi ya dhulma ya madhalimu, kukomesha dhulma yao kwa mikono yenu, na kuwawajibisha kwa makosa yao. Vyenginevyo tumekuhadharisheni na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni shahidi juu ya hayo.
Pia tungependa kuhutubia maneno yafuatayo kwa mashujaa wa kweli wa zama zetu: Enyi wabebaji Da’wah ya Uislamu! Nyinyi mlikuwa watu waliolelewa kwa elimu ya upagani, lakini mlijiunga na safu za waumini kwa kutumia akili zenu, na mkawa miongoni mwa Waislamu waaminifu, wakweli waliojifunza Uislamu kwa fikra na njia yake, na mkafuata njia hii—tofauti na Waislamu ambao hawajauelewa kikamilifu Uislamu. Mulijua kuwa lengo lenu ni radhi za Mwenyezi Mungu, na mukatambua kuwa radhi zake hazipatikani isipokuwa kwa kutabikisha Shariah yake. Mukawa na yakini, bila ya shaka yoyote, kwamba Shariah ya Kiislamu haitekelezeki kikamilifu isipokuwa ndani ya Dola ya Kiislamu, na mukaelewa kikamilifu kwamba kufikia radhi za Mwenyezi Mungu katika zama zetu hizi ni kwa kufanya kazi ya kusimamisha Dola ya Khilafah, ambayo ni taji la faradhi zote. Mwenyezi Mungu ametuahidi ushindi duniani na Jannah kesho Akhera. Kujitolea mhanga katika njia hii kunalipwa na daraja ya kifo cha shahidi. Mukishikilia kwa uthabiti imani yenu, mtajikuta mnangojea kifo cha shahada, na mkiweka lengo lenu mbele ya macho yenu, mtajikuta nyinyi ni wavumilivu, wenye kustarehe, na wenye kufarijika.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ فَلَيَعْلَمَنَّ اللهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ]
“Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo.” [Al-Ankabut:3]. Na Yeye (swt) amesema:
[وَمِنْ النَّاسِ مَنْ يَعْبُدُ اللهَ عَلَى حَرْفٍ فَإِنْ أَصَابَهُ خَيْرٌ اطْمَأَنَّ بِهِ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ انقَلَبَ عَلَى وَجْهِهِ خَسِرَ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةَ ذَلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ]
“Na katika watu wapo wanao muabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia kheri hutulia kwayo, na ukimfikia msukosuko hugeuza uso wake. Amekhasiri dunia na Akhera; hiyo ndiyo khasara iliyo wazi.” [Al-Hajj:11]. Na Yeye (swt) amesema:
[وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِنْ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِنْ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرْ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri, * Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Baqara:155-156] Na Yeye (swt) amesema:
[أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ * الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ * لَهُمْ الْبُشْرَى فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللهِ ذَلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ]
“Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika * Hao ni ambao wameamini na wakawa wanamcha Mungu. * Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hapana mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” [Yunus:62-64]. Na Yeye (swt) amesema:
[إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ * يَوْمَ لَا يَنفَعُ الظَّالِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ وَلَهُمْ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ]
“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi, * Siku ambayo hautawafaa madhaalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata makaazi mabaya kabisa.” [Ghafir:51-52].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kyrgyzstan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kyrgyzstan |
Address & Website Tel: http://hizb-turkiston.net |
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net |