Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  6 Rabi' II 1446 Na: H.T.L 1446 / 06
M.  Jumatano, 09 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kutenganisha Lebanon na Gaza
ni Hatua ya Kuelekea kuweka Amani na Adui Mvamizi na Uhalalishaji Mahusiano!

(Imetafsiriwa)

Mnamo Oktoba 7, 2024, aliyekuwa Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje wa Marekani David Hale alisema kuhusu mpango wa Ruwaza ya 2030 kuhusu LBCI: “Sasa, tunayo nafasi ya kuitaka Hezbollah kupokonywa silaha. Tangu Mkataba wa Taif, kumekuwa na biashara ambayo haijakamilika. Lebanon inapaswa kuunda mpango na kuuwasilisha kwa ulimwengu, sio vyenginevyo.” Aliongeza kuwa “Kukabiliana na maelezo ya Azimio 1701, azimio la zamani ambalo halijatekelezwa kikamilifu, hakutabadilisha mpangilio wa usalama.” Siku hiyo hiyo, ziliibuka kauli za kustaajabisha, zikionyesha mshikamano kati ya baadhi ya wabunge wa upinzani na wanaoiunga mkono serikali ya Lebanon, wakitaka kutenganishwa kwa Lebanon na Gaza! Haya yalijiri sambamba na taarifa za awali za Spika wa Bunge Nabih Berri, ambaye alitaja kwamba katika mawasiliano yake ya mwisho na Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Chama cha Iran (Hezbollah), kabla ya kuuawa kwake, Nasrallah hakuonyesha pingamizi yoyote kuhusu usitishaji vita! Hii ni pamoja na kwamba misimamo ya awali ya kisiasa kutoka kwa Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Waziri wa Mambo ya Nje ilionyesha kuwa pande hizo mbili zilikuwa na uhusiano. Kisha, Oktoba 8, 2024, Sheikh Naim Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Iran (Hezbollah), alisema: “Tunaunga mkono harakati za kisiasa zinazoongozwa na Rais Berri, na lengo lake kuu likiwa ni kusimamisha vita.” Aliongeza, “Pindi usitishaji mapigano utakapoimarishwa na diplomasia inaweza kufanikisha hilo, maelezo mengine yote yatajadiliwa, na maamuzi yatatolewa kwa ushirikiano.”

Enyi Watu wa Lebanon kwa Jumla:

Hebu hata mmoja wetu asisahau kwamba umbile la Kiyahudi ni adui mwenye chuki, anayekalia kwa mabavu, na mwenye kinyongo, anayetamani ardhi na rasilimali zetu. Tangu kuanzishwa kwake, limeendelea kushambulia ardhi zetu kwa usaidizi wa Magharibi, silaha, na ulinzi wa kimataifa kupitia maazimio. Hivi leo, chini ya mamlaka ya serikali ya mrengo mkali wa kulia inayoongozwa na mhalifu Netanyahu, umbile hili limezidi kujitotesha damu ya watu wa Lebanon na Palestina, kufanya uhalifu, mauaji, kuhamisha na uharibifu. Haya yote yanatokea kwa sababu, tangu kuanzishwa kwake hadi sasa, halijawahi kukabiliwa na mfumo wa kweli wa uongozi au jeshi lenye mamlaka ya kuamua vita. Kwa hivyo, yeyote kati yenu asifikirie kufanya amani nalo, kwani ni adui asiyeaminika, na kuishi pamoja nalo haiwezekani. Haijalishi munafanya nini, miradi yake ya upanuzi na majaribio yanayoendelea ya kupanua ushawishi wake katika eneo hili yameundwa kulifanya kuwa chombo cha kikatili na polisi anayehudumia washirika wake wa Magharibi, hasa Amerika. Je, mmesahau enyi watu wa Lebanon, mwendazake Sharon na mauaji yake mwaka 1982, alipoivamia Lebanon na mji mkuu wake, kwa madai ya uongo kwamba hatavuka mpaka wa kilomita 30, akieleza kuwa ni operesheni ya haraka?!

Enyi Waislamu nchini Lebanon, Hasa:

Jihadharini na kuangukia na kung'ang'ania mipaka ya kindoto iliyochorwa na wakoloni, makafiri Magharibi, ambao hawajaleta chochote isipokuwa mgawanyiko na udhaifu juu yenu nchini Lebanon na kanda hii, na kuwaacha hamwezi kusaidia familia na ndugu zenu nchini Palestina na mahali pengine! Nyinyi ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya jumuiya ya Waislamu ya kimataifa. Kama ilivyoelezwa katika Hati ya Madina, iliyoanzishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambayo iliweka msingi wa dola na hadhara yenu ya kwanza:

«أُمَّةٌ وَاحِدَةٌ مِنْ دُونِ النَّاسِ... وَإِنَّ ذِمَّةَ اللهِ وَاحِدَةٌ، يُجِيرُ عَلَيْهِمْ أَدْنَاهُمْ، وَإِنَّ الْمُؤْمِنِينَ بَعْضُهُمْ مَوَالِي بَعْضٍ دُونَ النَّاسِ... وَإِنَّ سِلْمَ الْمُؤْمِنِينَ وَاحِدَةٌ، لَا يُسَالَمُ مُؤْمِنٌ دُونَ مُؤْمِنٍ فِي قِتَالٍ فِي سَبِيلِ اللهِ.. وَأَنَّكُمْ مَهْمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِنْ شَيْءٍ فَإِنَّ مَرَدَّهُ إِلَى اللهِ وَإِلَى مُحَمَّدٍ...»

“Umma mmoja (taifa) kando na watu wengine... Na ulinzi wa Mwenyezi Mungu ni mmoja, na wa chini wao anayeweza kulindwa kwa niaba yao. Na Waumini ni washirika wao kwa wao, kando na watu wengine... Na amani ya Waumini ni moja, hapana Muumini atakayefanya amani kando na Muumini mwengine katika vita katika Njia ya Mwenyezi Mungu... Na kwamba namna mtakalo khitalifiana katika jambo hakika maregeo ni kwa Mwenyezi Mungu na kwa Muhammad...” Hivyo basi, nyinyi ni sehemu ya Ummah huu bilioni mbili. Je, ni zaidi kiasi gani kwa Waislamu walio karibu nanyi, na kwa ujumla nchi za Ash-Sham, na hasa katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina?!

Enyi Waislamu, Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu, Hasa katika Nchi zinazozunguka.

Watawala wa Lebanon na ardhi za Waislamu wamepandikizwa kuharakisha na kufuata mipango ya nchi za Magharibi kila inapoamrishwa. Matarajio yao makubwa zaidi ni kubaki madarakani, hata kama wako chini ya nyayo za mkaliaji wa kimabavu na kwa gharama ya damu na Dini yenu. Kwa hivyo, suluhisho la kimsingi ambalo tunakukumbusheni mara kwa mara hadi Mwenyezi Mungu atakapolidhihirisha au tufe kwa ajili yake, ni kuwataka watoto wenu katika majeshi kukuta vumbi la kusubiri na kutarajia na kusonga kuelekea katika ardhi ya Palestina, wakitangaza takbira (Allahu Akbar). Endapo watawala hawa watasimama katika njia zao, wafagiliwe mbali, na waweke kiongozi atakayewaongoza katika viwanja vya vita, ambaye nyuma yake watapigana na kutafuta ulinzi. Kisha mtashuhudia jinsi Mayahudi watakavyoanguka, na Mwenyezi Mungu atakutieni nguvu juu yao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ * وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ وَيَتُوبُ اللهُ عَلَى مَن يَشَاءُ وَاللهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini (14) Na aondoe hasira ya nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu humkubalia toba ya amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.” [At-Tawba:14-15].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu