Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  8 Jumada II 1446 Na: H.T.L 1446 / 08
M.  Jumanne, 10 Disemba 2024

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon inaomboleza kifo cha mmoja wa watu wake waliobeba dawah katika mji wa Sidon na kambi ya Mieh Mieh:

Fouad Abdullah Mansour (Abu Imad)

Ambaye alifariki asubuhi ya tarehe nane Jumada al-Akhirah 1446 H, sawia na tarehe 10 Disemba 2024 M.

Abu Imad, Mwenyezi Mungu amrehemu, aliubeba ulinganizi pamoja na hizb tangu miaka ya thamanini ya karne iliyopita, na akaendelea kuubeba na kuwa mchangamfu ndani yake hadi alipofungika kitandani kutokana na maradhi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aujaalie ugonjwa wake kuwa ni kafara na utakaso, na akubali kutoka kwake aliyoyatoa na kujitolea mhanga katika njia ya kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na amkusanye kwa rehema yake pamoja na Manabii, wakweli, na Mashahidi, na watu wema, na hao ni maswahaba wema walioje.

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu