Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  6 Jumada II 1446 Na: H.T.L 1446 / 07
M.  Jumapili, 08 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuanguka kwa Utawala Dhalimu nchini Syria ni Furaha kwa Wanyonge
(Imetafsiriwa)

Tunawapongeza Waislamu kwa jumla na watu wa Ash-Sham na Lebanon haswa kwa kuanguka kwa dhalimu wa ash-Sham, Chama cha Baath, familia ya Al-Assad, wapambe wao, majasusi wao na wapumbavu wao, ambaye aliwafanya Waislamu kuonja maovu ya mauaji, mateso, mauaji, kukamatwa na kufurushwa... nchini Lebanon na Syria.

Mnamo Disemba 8, 2024, Bashar aliwakimbia wanamapinduzi na utawala wake wa dhulma ukafikia mwisho. Ni wakati wa kuwaadhibu wahalifu. Waislamu wana haki ya furaha kubwa, na furaha yetu haitakamilika isipokuwa kwa kutabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu na kuziunganisha nchi za Waislamu.

Enyi Watu Wetu nchini Lebanon: Nyinyi ni sehemu ya Ash-Sham na ardhi za Waislamu, na wapumbavu wa dhalimu wa ash-Sham daima wamekufedhehesheni kama walivyowafedhehesha watu waliokimbia makaazi yao wa Palestina. Umefika wakati sasa wa nyinyi kukukuta vumbi la udhalilifu na kuungana katika kuwakabili maadui zenu wanaokuvizieni, kuanzia umbile la Kiyahudi, hadi walinzi wake miongoni mwa watawala, hadi mabwana zao wa Magharibi.

Sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Lebanon tunakuhimizeni mushirikiane nasi katika kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kuhuisha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itatawala kwa Uislamu na kuubeba dunia nzima. Siku hiyo Waumini watafurahia ushindi wa Mwenyezi Mungu, na kuregeshwa kwa chombo cha Ummah kutakuwa ni afueni kwa Waislamu na wengineo. Kama ambavyo kila mtu alifurahia haki zake chini ya Khilafah kwa mamia ya miaka, ikiwa ni pamoja na usalama, amani, kuhifadhi mali, elimu, matibabu, na uchungaji, atafurahia hayo hayo chini ya dola yenu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Mamlaka za Lebanon lazima zichukue hatua ya kuwaachilia huru wafungwa wa Kiislamu kutoka Gereza la Roumieh na jela za Lebanon ambao walikuwa wamefungwa kwa dhulma na kwa ukali, bila ubaguzi, kwa tuhuma za kuunga mkono mapinduzi ya Ash-Sham ili furaha ya Waislamu wa Lebanon ipate kuwa furaha isiyo na kifani.

[وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ]

“Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.” [Al-Qasas 28:5]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu