Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 9 Jumada II 1446 | Na: H.T.L 1446 / 09 |
M. Jumatano, 11 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Taharir / Wilayah Lebanon
Wamzuru Mbunge Osama Saad
(Imetafsiriwa)
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon katika mji wa Sidon, ukiwakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano, Mhandisi Bilal Zaidan na Mjumbe wa Kamati ya Amali katika mji wa Sidon, Hajj Hassan Nahhas, walimtembelea Mwakilishi Osama Saad leo, Jumatano, Disemba 11, 2024. Ujumbe huo uliwasilisha msimamo wa Hizb kuhusu matukio mbalimbali hasa yanayojiri katika eneo hali ya Syria, Lebanon na kanda kwa jumla.
Kisha mjadala ukazunguka pambizoni mwa masuala kadhaa, yakiwemo:
1- Athari ya kuanguka kwa utawala wa Assad nchini Syria kwa Lebanon na kanda hii.
2- Umuhimu wa kufanya uhakiki wa pande zilizounga mkono utawala wa Syria kama mfuasi wa upinzani, na kuangalia upya asili ya uhalisia wa mapinduzi ya Syria yaliyotokea mwaka 2011 kama mapinduzi ya haki dhidi ya udhalimu na dhulma.
3- Uhalisia wa mabadiliko ya kisiasa nchini Lebanon kwa kuzingatia vita vya hivi karibuni vya Mayahudi dhidi ya Lebanon.
4- Kuhisi mukhtasari wa mpango wa kuunda upya ushawishi katika kanda hii kwa kuzingatia kupungua kwa dori ya Iran na kuimarishwa kwa ubora wa kijeshi wa umbile la Kiyahudi.
5- Kutosalimu amri na kuukubali uhalisia mpya ambao Marekani inajaribu kuulazimisha katika kanda hii na Lebanon, hasa kwa vile Marekani ina hamu tu ya kufikia maslahi yake, kupora mali ya eneo hili, na kulinda usalama wa umbile la Kiyahudi.
Mbunge Osama Saad na wahudhuriaji wenzake walitoa mwanga kuhusu masuala kadhaa, ikiwa:
- Kukubali mabadiliko nchini Syria kama badiliko katika uso wa utawala kidhulma kwa watu wake, na kutotumia matamshi ya uchochezi dhidi ya wanamapinduzi nchini Syria, huku tukiwa makini kutoruhusu umbile la Kiyahudi kuendelea kupenya katika ardhi ya Syria na kushambulia silaha za jeshi la Syria, ambazo zinachukuliwa kuwa moja ya mali ya watu wa Syria.
- Akibainisha kuwa mabadiliko ya Syria yaliratibiwa kati ya Uturuki na Amerika.
- Ni wazi kwamba makubaliano ya hivi karibuni ya kumaliza vita na umbile Kiyahudi yalikuwa ya kufedhehesha Lebanon na kusalimisha ubwana wake.
- Licha ya uhalisia unaobadilika katika kanda hii, ni muhimu kupinga miradi na mapendekezo ambayo yanatoa wito wa kujisalimisha kwenye uhalisia na kulazimisha uhalalishaji mahusiano.
- Kuendelea pamoja na nguvu za mabadiliko nchini Lebanon ili kukabiliana na ufisadi na nguvu ambazo zitaweka ushawishi na utiifu kwa Amerika.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |