Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  1 Rajab 1443 Na: HTM 1443 / 03
M.  Jumatano, 02 Februari 2022

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Malaysia Yazindua Kampeni
"Uislamu Kaffah Chini ya Khilafah"

(Imetafsiriwa)

Kipindi cha huzuni cha Ummah kinaendelea Rajab hii kwani karne moja imepita baada ya kuanguka kwa Khilafah. Miaka mia moja sio kipindi kifupi kwa taifa lolote kupoteza nchi, achilia mbali Waislamu kupoteza Dola iliyobarikiwa ambayo ilijengwa kwa damu na machozi ya waumini na amri kutoka mbinguni saba. Hii ndiyo Dola iliyowakomboa Waislamu kutoka katika mateso yote, dunia kutoka katika giza lote na kuwakomboa wanadamu wote kutoka katika ibada za wanadamu wenzao hadi kumwabudu Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla pekee. Hii ndiyo Dola ambayo iliutukuza Uislamu na wafuasi wake na kufedhehesha ukafiri na wafuasi wake. Hii ndiyo Dola iliyoifanya Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) kuwa na ushindi juu ya dini nyengine zote na Dola iliyoeneza baraka za Mwenyezi Mungu (swt) kila pembe ya dunia. Hii ndiyo Dola ambayo imetabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa ukamilifu (Kaffah) na imeleta uadilifu na ustawi sio tu kwa wanadamu, bali pia kwa falme za mimea na wanyama. Hata hivyo, Dola hii yenye nguvu na iliyobarikiwa iliporomoka tarehe 28 Rajab 1342 H (3 Machi 1924 M) kama matokeo ya usaliti wa ndani, ambao umeacha jeraha baya na kubwa katika Ummah huu hadi leo.

Pamoja na kuporomoka kwa Khilafah, utukufu, utakaso na baraka zote pia zilitoweka. Na vilevile utabikishwaji kamili wa Uislamu - "Islam Kaffah" - ambao ulihifadhi Ummah kwa karne 13. Kilichosalia katika nchi za Kiislamu leo ni sheria chache tu za Kiislamu ambazo zinatekelezwa kibinafsi kama vile Swalah, Aurah, ndoa, mirathi na sheria kuhusu vyakula na vinywaji. Utawala wa Kiislamu na jamii ulitoweka kutoka kwa maisha ya Waislamu na baya zaidi, dola za kisekula na sheria za kikafiri za Kimagharibi zikawa badali yake? Kwa sababu hiyo, Waislamu wamesahau upana wa Uislamu na ukamilifu wake - mfumo wake wa utawala, mfumo wa kiuchumi, mfumo wa kijamii, mfumo wa adhabu na kadhalika elimu na sera za kigeni. Kuna Waislamu ambao wamesahau kabisa na kutoujali Uislamu na wamepoteza imani katika mifumo na sheria za Kiislamu.

Kwa misingi hii, na kuambatana na mwezi wa Rajab, mwezi wa kuanguka kwa Khilafah, Hizb ut Tahrir/Malaysia yazindua kampeni kwa anwani “Islam Kaffah Chini ya Khilafah” itakayoanza kuanzia mwanzo hadi mwisho wa Rajab mwaka huu, Insha Allah. Katika mwezi mzima huu, tutakuwa tukiwaeleza na kuwakumbusha Waislamu kwa jumla na haswa watawala, juu ya upana wa Uislamu na wajibu wa kuregesha sheria nzima ya Kiislamu (Shariah) ambayo nayo maana yake ni kuiregesha Khilafah, kuwa ndiyo taasisi pekee yenye uwezo wa kutabikisha Uislamu kwa ujumla wake - "Islam Kaffah". Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aibariki kampeni hii na airahisishe utekelezaji wake. Tunatumai kwamba kampeni hii itaongeza ufahamu kwa Waislamu juu ya wajibu na umuhimu wa kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa ukamilifu chini ya Dola iliyobarikiwa ya Khilafah kwa njia ya Utume.

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir Malaysia

#ReturnTheKhilafah  #YenidenHilafet
 #الخلافة_101 #أقيموا_الخلافة  
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu