Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  29 Safar 1446 Na: HTM 1446 / 05
M.  Jumanne, 03 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Malaysia Inaadhimisha Uhuru: Hata hivyo, Uhuru wa Kweli Uko Wapi na Wasaliti Halisi ni kina Nani?

(Imetafsiriwa)

Wakati wa hotuba yake katika Siku ya 67 ya Uhuru wa Malaysia, Waziri Mkuu Datuk Seri Anwar Ibrahim alizungumzia masuala mbalimbali, akionekana kujiweka kama “shujaa” kwa watu. Anwar amekuwa akizungumzia dhamira yake ya kutokomeza ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ndani ya serikali. Hata hivyo, maswali yanazuka wakati ikizingatiwa kwamba naibu wake mwenyewe, aliyeteuliwa na Anwar, amehusishwa na kesi nyingi za ufisadi, lakini aliachiliwa kwa utata. Umma hauwezi kujizuia kujiuliza: Je, naibu huyu angeweza kuachiliwa kwa urahisi hivyo, hasa baada ya kesi ya awali kuanzishwa, kama  Anwar asingekuwa Waziri Mkuu?

Katika hotuba yake, Anwar alisisitiza sana kujitolea kwake kukomesha vitendo vya muda mrefu vya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka tangu ashike uongozi. Alieleza nia yake ya kukuza utamaduni mpya ambapo viongozi wanawajibishwa na kuzuiwa kutumia utajiri wa taifa kwa manufaa ya kibinafsi. Hata hivyo, je, Anwar hajui kikweli, au anapuuza kwa makusudi ukweli kwamba utajiri wa taifa, kuanzia tawala zilizopita hadi wake mwenyewe, kamwe haujawahi kuwanufaisha watu kikweli? Rasilimali nyingi za Malaysia - kama vile mafuta, gesi asilia, mbao, bauxite na zingine nyingi - zilizoainishwa kama mali ya umma (Al-Milkiyyah Al-Ammah), zinapaswa kutajirisha watu. Badala yake, faida inaonekana kuingia katika mifuko ya nani, ikiwa sio mifukoni mwa wale walio na mamlaka na washirika wao?

Anwar pia alisikitika jinsi, wakati wa ukoloni, mataifa ya kigeni yalivychota utajiri wa Malaysia kwa manufaa yao wenyewe. Ingawa kauli hii ina ukweli, inazua swali muhimu: baada ya kupata “uhuru,” nani amechukua nafasi ya wakoloni, ikiwa sio viongozi wa Malaysia na washirika wao? Uhalisia ulio wazi nchini Malaysia ni kwamba wale walio madarakani mara nyingi huwa matajiri sana, huku raia wakiendelea kuteseka. Je, hawa viongozi wanapata wapi utajiri wao ikiwa sio rasilimali za taifa? Je, Anwar anapuuzia ukweli huu, au anajaribu kuwahadaa watu?

Waziri Mkuu pia alileta suala la kisiwa cha Batu Puteh, ambacho “kiliachiliwa” kwa Singapore. “Ni mataifa machache tu duniani ambayo yangeweza kuachia nchi nyingine kwa urahisi hata shubiri moja ya ardhi au chembe ya jiwe. Wakati tunakubali uamuzi wa ICJ (Mahakama ya Kimataifa ya Haki) kuhusu Batu Puteh... ni uzembe wetu wenyewe ndio uliosababisha khiyana hii ya nchi yetu. Hakuna taifa lolote duniani lenye kusalimisha eneo lake kwa urahisi. Nchini huingia vitani, hupoteza maisha ili kulinda hata sehemu ndogo zaidi ya ardhi zake.” Anwar alisema. Ingawa hakuwataja waliohusika na kupotea kwa kisiwa cha Malaysia cha Batu Puteh, inajulikana nyema kuwa Dkt. Mahathir Mohamad alikuwa ndiye Waziri Mkuu wakati huo.

Kutetea haki zetu za kieneo, hata kama inahusu shubiri moja ya ardhi, ni muhimu mno. Ikiwa huu ndio msimamo wa Anwar, basi Malaysia inapaswa pia kutafuta kurudisha kisiwa cha Singapore, ambacho “kilisalimishwa” kwa Singapore na Waziri Mkuu wa kwanza wa Malaysia mnamo 1965. Zaidi ya hayo, Anwar anapaswa kutetea kuregeshwa kwa majimbo yetu manne ya kaskazini - Songkhla, Narathiwat, Yala, na Pattani - ambayo yalikabidhiwa Thailand chini ya Mkataba “batili” wa 1909 wa Bangkok, uliotiwa saini na Waingereza na Thailand. Maeneo haya ni sehemu zilizopotea za taifa letu, na Anwar anapaswa kufuatilia kwa dhati kurudishwa kwao ikiwa amejitolea kwa dhati kwa maneno yake.

Zaidi ya hayo, Anwar anapaswa kutetea kwa nguvu zote ukombozi wa Msikiti wa Aqsa, ambao ni msikiti wetu, na Ardhi yote iliyobarikiwa ya Palestina, ambayo ni ardhi yetu, ambayo kwa sasa inakaliwa kimabavu na Mayahudi. Je, mataifa hayapaswi kwenda vitani ili kurudisha hata sehemu ndogo ya eneo lao linalokaliwa kimabavu, kama Anwar alivyosema? Kwa nini, basi, Anwar hajachukua hatua hiyo ya kuregesha Msikiti wa Aqsa na Palestina? Inashangaza zaidi kwamba Anwar anaunga mkono suluhisho la dola mbili kwa Palestina. Je, hajui kwamba suluhisho kama hilo linahusisha kukabidhi sehemu kubwa ya ardhi yetu (Palestina) kwa wavamizi wa Kiyahudi? Je, uregeshaji wa angalau kipande cha eneo letu haupaswi kuwa wa lazima? Je, Anwar anawezaje basi kuhalalisha kukabidhi sehemu kubwa zaidi ya ardhi yetu (Palestina) kwa wanyakuzi kwa njia ya dola mbili?!

Anwar pia alielezea hamu yake ya kuifanya Malaysia kuwa taifa kubwa, barani Asia na kimataifa. Ingawa matamanio haya ni ya kusifiwa, yatabaki kuwa maneno tu kama hayatafuatiliwa chini ya mfumo wa Aqida ya Kiislamu na Shariah. Haiwezekani kwa Malaysia kupata utukufu huku ikibaki kuwa dola ndogo ya kitaifa inayotii ushawishi wa Magharibi. Utukufu haupatikani ikiwa Malaysia itaendelea kufuata mifumo, nidhamu, sheria, utamaduni, na hata mawazo ya mabeberu. Kufikia utukufu wa kweli hakuwezekani ikiwa Aqida ya nchi itabaki kuwa ya kisekula, ikitenganisha dini na maisha na utawala. Ni aina gani ya utukufu tunaweza kufikia wakati Malaysia kamwe haijawahi kupata “uhuru” wa kweli katika maana halisi?

Uhuru wa kweli wa nchi hii na watu wake unaweza kupatikana tu pale utiifu na kujisalimisha kwake kutaelekezwa kwa Mwenyezi Mungu (swt), badala ya mifumo, nidhamu na sheria zilizolazimishwa na mabeberu. Maadamu serikali itatawala kwa mujibu wa mifumo, nidhamu na sheria zilizorithiwa kutoka kwa wakoloni, uhuru wa kweli utabakia kuwa ndoto. Kwa hakika wale walioko madarakani wanaotawala kwa kufuata mifumo hii ya kikoloni, kimsingi, ni wasaliti wa kweli wa nchi na Ummah, kwani wameshindwa kuisimamia amana waliyopewa na Mwenyezi Mungu (swt), ambayo ni kutabikisha Shariah yote kwa jumla yake.

Uhuru wa kweli wa nchi hii unaweza kupatikana tu pale Aqidah yake itakapohama kutoka kuwa ya usekula hadi kuwa ya Uislamu, ikifuatiwa na mabadiliko kamili ya mfumo wake na sheria kutoka ya kisekula hadi Shariah. Mabadiliko haya yanalazimu kusimamishwa kwa Khilafah, ambayo sio tu kwamba itatabikisha Sheria za Mwenyezi Mungu kwa ujumla wake bali pia zitatumika kuukomboa na kuuunganisha Ummah na ardhi zake chini ya mwavuli mmoja. Ni kupitia njia hii tu - kusimamishwa tena Khilafah - ndipo Ummah huu na Dola yake utaweza kupata utukufu na izza katika mambo yote, wakijiweka kama dola kuu ya kimataifa inayoheshimika inayoeneza rehema katika pembe zote za dunia, Insha Allah.

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu