Jumamosi, 04 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  12 Rajab 1445 Na: 1445/18
M.  Jumatano, 24 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Misri Yawapa Watu Asali huku Wakinywa Sumu Mikononi Mwake!
(Imetafsiriwa)

Msemaji wa Afisi ya Rais wa Jamhuri, Ahmed Fahmy, alithibitisha kuwa dola hii imepata mafanikio mengi katika ngazi na nyanja zote na kueleza kuwa serikali inajitahidi kukabiliana na changamoto hizo akisema: “Ni jambo la kimaumbile kwa wananchi kuhisi afueni inayotokea wakati utabikishaji umekamilika na juhudi zote kuwekwa wazi.”

Uongo wa wazi, hakuna mtu atakayeamini. Hali ya Misri na watu wake inazidi kuwa mbaya hadi mbaya zaidi, na bei ya bidhaa inazidi kupanda kwa kasi, na serikali inafanya bidii katika kukopa na kujisalimisha kwake kwa hali mbaya na maamuzi ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), ambayo yanawapendelea mabepari wakubwa na kupora utajiri wa nchi. Wanaongelea afueni gani wakati bei ya dolari inazidi pauni 62 katika soko sambamba katika nchi ambayo inaagiza nyingi ya bidhaa inazotumia hata ngano na mchele, ilhali ni nchi ya kilimo, huku watu wakizuiwa kukuza wanachohitaji?!

Misri ina vipengele vyote vinavyoistahili kupata afueni hiyo ambao msemaji wa utawala huo anadokeza, lakini vyote vimepotea au kupuuzwa na watu wamezuiwa kuwanyonya. Ni nani anayepigania watu kwa ajili ya chakula na riziki zao na kuwawekea vikwazo vya kujipatia riziki? Ni nani anayezuia uwezo mkubwa wa kibinadamu ulio nao Misri na kudai kwamba inatafuna maendeleo yake?

Tunakabiliwa na uhalisia mchungu ambao unakuwa mchungu zaidi kadiri masaa na dakika zinavyopita. Siku hizi haziendani tena na kasi ya mporomoko ambao serikali inaisukuma Misri na watu wake, jambo ambalo limefanya wataalamu na wachambuzi wa mambo kupunguza matarajio yao ya kukua kwa uchumi wa Misri. Mfumko wa bei wa kila mwaka wa Misri uliendelea kupanda katika mwezi wa Septemba uliopita, na kufikia 40.3%, ikilinganishwa na 39.7% Agosti iliyopita, kulingana na data ya awali kutoka Wakala Mkuu wa Uhamasishaji wa Umma na Takwimu, ambayo pia ilionyesha kuongezeka kwa kiwango cha mfumko wa bei wa kila mwezi. 2.1%. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na katika kipindi cha mikutano mitano iliyopita, Benki Kuu imepandisha viwango vya riba kwa pointi 300 za msingi, na kufikisha viwango vya riba kwenye amana na mikopo hadi 19.25% na 20.25% mtawalia. (Al-Shrouq).

Katika muktadha huo huo, kuna masharti ambayo IMF imeweka kwa serikali kupata awamu zilizobaki za mkopo wa awali, haswa kiwango cha ubadilishaji wa fedha ambacho kinategemea usambazaji na mahitaji, na kwa upande wa Misri haswa, ni chini ya ugavi pekee na sio mahitaji, kwani nchi haina bidhaa zenye umuhimu wa kimkakati zinazolazimisha nchi kuagiza. Huku Misri ikiagiza bidhaa nyingi, malighafi za kimkakati, na mahitaji ya uzalishaji, hata kwa kile kinachotengenezwa nchini Misri, ambacho hakina anasa ya kudai dolari kutoa bidhaa muhimu inayohitaji, haswa ngano, Misri ndiyo ya kwanza katika dunia kuagiza kutoka nje, wakati inaweza kuikuza si tu kufikia nukta ya kujitosheleza, lakini pia inaweza kuuza nje na kupata sarafu madhubuti kutoka kwayo.

Uhalisia wa kusikitisha unaoikabili Misri una wengi wanaoielezea, lakini ni wachache wanaoishughulikia, na kutoka hapa tunatoa suluhisho la halisi la migogoro yote ya Misri, tukianza na kuwezesha watu kufufua ardhi kupitia kilimo, ujenzi, ujenzi wa viwanda, nk., na kuwaunga mkono katika njia hii, kupitia kuhakiki upya mikataba ya makampuni yote ya utafiti wa mafuta na madini na kuyafukuza yote nchini, na kuanzisha makampuni ya serikali kutoka kwa Ummah ili kufanya operesheni za uchunguzi na kuchimba mali kutoka vyanzo vyake na kuisambaza kwa watu kwa usawa, Na kuitumia kusaidia watu katika kilimo na viwanda vinavyosaidiana nayo, kuanzisha viwanda vizito, na kuvifanya kuwa msingi wa viwanda na viwanda vyote nchini kwa msingi wa kijeshi.

Wakati huo huo, dhahabu na fedha nchini ni kidogo, iwe katika hazina ya serikali au kile masonara na wafanyibiashara wa dhahabu wanacho au hata kile walicho nacho. Watu, na kukusanya dhahabu hii yote ili kutengeneza pesa mpya kwa dhahabu na fedha, huku wakihifadhi haki za watu kwa kile kilichochukuliwa kutoka kwao cha dhahabu ambayo ni mali yao, muradi wamiliki wake watalipwa kwa kubadilishana ardhi au mali isiyohamishika. au mkopo unaandaliwa kwamba serikali itawarudishia thamani yake kamili itakapokuwa na kile kitakachotolewa kwenye migodi ya nchi baadaye. Pesa basi hutengenezwa na sarafu ya nchi inakuwa dhahabu na fedha au badali ya karatasi kwazo, ili ubadilishaji wa karatasi hii upatikane kwa kile ilicho nacho na ni kwa mmiliki wake wakati wowote mtu anapotaka, mtu anaweza kuipata. Wakati wa kuhakikisha kipindi ambacho watu wanaondoa sarafu zisizo na thamani za karatasi ambazo bado ziko mikononi mwao, maadamu serikali itazingatia kununua kile inachohitaji kwa badali ya sarafu  madhubuti za nchi ambazo bado zipo, na haitauza bidhaa zake kwa badali ya sarafu hizo, lakini kwa badali ya ubadilishanaji wa dhahabu na fedha pekee. Hapo hakutakuwa na mfumko wa bei, uchumi wa nchi hautateseka, thamani ya sarafu itapanda, na watu watahisi tofauti kiuhalisia kutoka siku ya kwanza watakapoanza vitendo hivyo.

Yote tuliyowasilisha hapo awali ni hukmu za Sharia ambazo Uislamu ulileta na dola ni ina wajibika kuzitekeleza zote. Haya ndiyo tunayoweza kuyaita mafanikio ya kweli iwapo yatatekelezwa, jambo ambalo utawala wa sasa unaohusisha katika sera zake na nchi za Magharibi haujafanya na hautafanya. Bali, inahitaji mfumo mpya badali, kwa hivyo masuluhisho haya hayatatekelezwa kwa kutenganishwa na hukmu zengine za Uislamu, badala yake, Uislamu wote lazima utekelezwe katika dola yake, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu