Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  4 Rajab 1445 Na: 1445/17
M.  Jumanne, 16 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mayahudi Wamefichua Mzingiro wa Utawala wa Misri kwa Watu wa Gaza na Kuwa ni Mshirika katika Uhalifu wake Dhidi Yao!
(Imetafsiriwa)

Afrika Kusini ilifungua kesi dhidi ya umbile la Kiyahudi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, na umbile la Kiyahudi likajibu kwa kukana mashtaka hayo, likijua kuwa hata ikiwa litakiri na kuhukumiwa na Mahakama ya Kimataifa, hakuna mtu atakayeweza kulishambulia au kulitia hatiani. Kwa kuwa Sheria ya Kimataifa inatumika tu kwa nchi dhaifu au zile ambazo Marekani haiziungi mkono au kuzisaidia. Lakini kinachotuhusu hapa sio tuhma au kukemewa kwao, licha ya kuwa zinafichua uhalisia wa utawala wa Misri, mshirika halisi wa umbile la Kiyahudi katika kuizingira kwake Gaza na watu wake. Inadhihirisha uhalisia ulio hai ambao haufichiki kwa mtu yeyote, ambao ni kushindwa kwa utawala huo kuwanusuru watu wa Gaza na kuwafungia watu mipaka ya bandia; Waliojeruhiwa, mkimbizi wao, waliokimbia makaazi yao, na wale wanaotafuta usaidizi, na ushuhuda wa wale ambao wamedhulumiwa na maafisa wa serikali hiyo kwenye kivuko kukusanya maelfu ya dolari kama badali ya kuwaruhusu wavuke. Bila kusahau kwamba utawala huo unaodai kuwa na uamuzi na ubwana yake juu ya ardhi yake, mipaka na vivuko vyake, haufanyi kuvuka kutoka na kuingia ndani yake kuwa chini ya mtu wa tatu.

Kivuko cha Rafah kiko kati ya Sinai na Ukanda wa Gaza. Ni nini kingefanya kile kinachoingia kwa njia ya kuvuka kuwa chini ya maamuzi ya Kiyahudi, kama si kwa utiifu wa utawala huu? Kwa Mayahudi na kuliwezesha umbile la Kiyahudi kuua na kuwafanyia ukatili watu wetu huko bila kufanya chochote, kutojibu uchokozi wa Mayahudi na kutojitanua. Msukosuko wa vita, na ukandamizaji wa hasira inayounguza ndani ya nafsi za watu na hata jeshi la Al-Kinana?!

Umbile la Kiyahudi linawazingira watu wetu huko Gaza na kuwachinja mshipa hadi mshipa kupitia ulipuaji wa mabomu, udenguaji, njaa na mzingiro kwa njia zote. Hili lisingewezekana bila ya msaada wa tawala zinazotawala ardhi zetu na kushiriki katika uhalifu wake dhidi ya watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa, zinazoongozwa na Misri, njia pekee ya kutokea ya watu wetu huko Gaza. Hata hivyo, hatushangazwi na msimamo wa utawala huu tuliojifunza kuuhusu kutoka kwa umbile la Kiyahudi na kwamba ndio mlinzi wa mipaka ya umbile hilo na kwamba kuhifadhi usalama wa Mayahudi ni moja ya kazi zake za kimkakati ambao unafanya kazi kuunda itikadi ya kijeshi kwa jeshi la Kinana, lakini matakwa yake na ya mabwana zake huko Magharibi yamefeli.

Kinachoshangaza kweli ingawa ni msimamo wa watu watiifu katika Jeshi la Misri mbele ya kile kinachofanyika cha ukiukaji wa matukufu, kuvuruga, kunajisi matukufu, na ukiukaji wa heshima ya ndugu zetu katika Ardhi Iliyobarikiwa. Wao ni mashahidi wa jinai za utawala huo na ushirika wake na umbile la Kiyahudi katika kuwazingira na kuwanyima chakula watu wa Gaza. Wanalia kuomba msaada mchana na usiku. Je, vilio vya wanawake na watoto wenye njaa na majeraha havijawafikia?! Je, hawakusikia sauti ya watoto wakiita “Enyi Wamisri, Ewe Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu”?! Wanaomba msaada kwao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu!

Je, hawakujua kile magazeti na vyombo vya Magharibi vilichapisha kuhusu rushwa ya maelfu ya dolari ili kuruhusu mgonjwa au majeruhi atibiwe katika ardhi ya Kinana?! Uungwana wenu uko wapi?! Sisi na watu wa Ardhi Iliyobarikiwa sio tu ni watu wawili ndugu, bali sisi ni Umma mmoja ambao damu yao ni sawa, ahadi ya ulinzi inayotolewa na wachini wao zaidi inatimizwa na Waislamu wote, na wanaungana dhidi ya maadui zao.

Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kuwanusuru watu wa Palestina ni jukumu juu yenu ambalo hulitaondoka kwenu mpaka muwape ushindi wa wazi na mpaka muikomboe ardhi yote iliyobarikiwa kutokana na uchafu wa Mayahudi.

Enyi Askari wa (Misri) Kinana, Enyi Askari Bora: Sifa ya askari bora mnayopewa sio heshima, bali ni mzigo wa amana ya Uislamu, amana ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), yaani kuwa walinzi wa Ummah na wa matukufu yake. Msipofanya hivyo, na yakakiukwa matukufu ya Ummah na maeneo yake matukufu yakanajisiwa, basi hamna kheri kwenu wala hamna heshima kwenu. Hivyo muonyesheni Mwenyezi Mungu baadhi ya yale yanayomridhisha, muonyesheni kuwa nyinyi munastahiki kuwa bora kwa kubeba bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), katika haki yake na kuwanusuru waliodhulumiwa kama alivyofanya yeye (saw), ili kuikomboa ardhi ya Uislamu iliyonyakuliwa na Mayahudi na kuwanusuru watu wa ardhi iliyobarikiwa ambao matukufu yao yanakiukwa. Na jueni kwamba wajibu wenu ni kuondoa kila kitu ambacho kinakuzuilieni kufanya yale ambayo Mwenyezi Mungu amekuamrisheni juu ya msingi wa kanuni “chochote kinachopelekea kwenye wajibu ni wajibu.” Basi, uondoeni utawala huu unaokuleteeni aibu, unaoshiriki na kumlinda adui wa Mwenyezi Mungu na adui yenu, na simamisheni dola kwa ajili ya Mwenyezi Mungu inayotayarisha majeshi kwa ajili ya haki na kuwanusuru watu wake; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kuweni na hasira, enyi askari wa Kinana na hasira zenu ziwe ni dalili inayothibitisha ukweli kwa maneno ya Mwenyezi Mungu na kukata njia ya wahalifu.

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal: 74]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu