Ijumaa, 10 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hakuna Ziada katika Qur’an Isiyo na Maana

Wanazuoni wa sarufi wamekubaliana kwamba (An) iliyotajwa baada ya ‘lamma’ na kabla ya kitenzi ni ziada. Kwa hivyo Ibn Al-Atheer alijibu vipi? Ibn Al-Atheer alimjibu mwanachuoni wa sarufi na kusema: wanazuoni wa sarufi hawana kauli katika masuala ya umbuji wa hali ya kujieleza kwa ufasaha. Na hawana maarifa ya siri zake, katika suala la kuwa wanazuoni wa sarufi.

Soma zaidi...

Wanawake na Watoto wa Kiislamu Wanakumbwa na Njaa Hadi Kufa Nchini Somalia huku Watawala wa Waislamu Wakiunga Mkono Ukandamizaji Ulimwenguni

Mnamo tarehe 5 Oktoba 2022, BBC iliripoti kuwa Somalia inakabiliwa na baa la njaa inayotokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40. Hadithi ya dada mmoja Muislamu inayofichuliwa na waandishi wa habari, ni ile ya Fatima Omar ambaye alimzika mtoto mmoja wa kiume kutokana na njaa na tayari alikuwa ameshamzika bintiye wa miaka 3 ambaye alifariki huku akitembea kwa siku 10 kutafuta msaada. Anawaambia waandishi wa habari kwamba hakuwa na nguvu za kumzika mtoto wake na alilazimika kuuacha mwili wake kando ya barabara huku akijua kuwa Fisi walikuwa wanakaribia kuingia ndani.

Soma zaidi...

Kipindupindu Kinawaua Watu wa Syria, Hivyo Iko Wapi Dola ya Kuwanusuru?!

Wizara ya Afya ya Utawala wa Syria ilitangaza mnamo Jumatatu kuwa mkurupuko wa kipindupindu katika maeneo kadhaa umewauwa watu 29, vifo na majeruhi vilikolea katika jimbo la kaskazini la Aleppo, ambapo watu 25 walithibitishwa kufariki, na maelfu kadhaa ya visa vinavyoshukiwa kuripotiwa kote nchini kuanzia Septemba 19, kulingana na data iliyopatikana na chama cha misaada kutoka Kitengo cha Afya cha Serikali ya Syria (GoS), Idara ya Kibinafsi ya Mamlaka ya Afya ya Mitaa, Kaskazini na Mashariki mwa Syria.

Soma zaidi...

Jinsi Vita Vilivyoshindwa vya Amerika Dhidi ya ‘‘Ugaidi’’ Vingali Vinawatoa Kafara Watu

Thomas West, Mwakilishi Maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Amerika kwa Afghanistan, katika hotuba yake ya hivi majuzi katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa (CSIS) alisema: "Kwa kweli ninaogopa - na nadhani hii ni itifaki - kwamba tunachokiona sasa ni kusimama kidogo katika miaka 44 ya mzozo na kwamba tunaweza kuona kurudi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika wakati wowote”.

Soma zaidi...

Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Amit Shah Anaongoza katika "Ni Nani anacheza ngumu dhidi ya Waislamu!"

Mnamo tarehe 28 Septemba 2022, Serikali ya India ya BJP ilipiga marufuku shirika la India la Popular Front na mashirika mengine 8 yanayohusiana yaliyosajiliwa kwa miaka 5. Serikali ilidai kuwa imepiga marufuku PFI na makundi washirika wake kwa madai ya kufanya "shughuli zisizo halali" ambazo "zinaathiri uadilifu, uhuru na usalama wa nchi".

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu