Jumatatu, 23 Muharram 1446 | 2024/07/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kwa Tangazo la Misaada ya Kigeni kama Silaha Dhidi ya Sanaa Je, Serikali ya Wokovu Imegeukia Misaada ya Kigeni kwa Sababu ya Uhaba wa Machaguo au Hakuna Chaguo Jengine?!

Gazeti la Kila Siku la Al-Thawra, lililotolewa mjini Sanaa mnamo Ijumaa, Februari 2, 2024, lilizingatia majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Hussein Al-Azzi kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kupitia tweet yake kwenye jukwaa la X. Alisema: “Waingereza kudokeza kutumia misaada kama silaha dhidi ya watu wa Yemen ni aibu,” Naibu Waziri aliongeza katika tweet yake kwamba “dokezo hili halitawazuia watu wa Yemen kuendelea na uungaji mkono wao wa haki wa msaada wa kibinadamu kwa raia mjini Gaza.”

Soma zaidi...

Tarehe 28 Rajab Mwaka huu ni Ukumbusho Mkubwa kuliko Miaka Yote Iliyopita kwamba Kuregea kwa Khilafah ni Hitajio la Haraka

Kumbukumbu ya kuanguka kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab inakuja mwaka huu ikiwa na athari zaidi ya kukumbukwa kuliko miaka iliyotangulia. Inakuja na jeraha la Palestina linalotiririka damu nyingi zaidi kuliko hapo awali, na kutukumbusha kwamba suala la kupotea kwa Palestina lilikuwa na bado lina uhusiano wa karibu na kuanguka kwa Khilafah.

Soma zaidi...

Ni Nani Atakayefuta Aibu Yenu, Enyi Wanajeshi wa Kinana?!

Baada ya mkuu wa ujasusi wa Misri kuwaonya Hamas juu ya ulazima wa kukubali makubaliano ya kubadilishana wafungwa yaliyoandaliwa chini ya mwavuli wa Marekani ndani ya wiki mbili, na kisha tangazo la redio ya jeshi la umbile la Kiyahudi kwamba Misri ingekubali kuivamia Rafah kwa masharti ya kuhakikisha kuwa Wapalestina hawafurushwi hadi Sinai, pia mnamo Jumapili asubuhi, tarehe 11/2/2024, redio hiyo ilinukuu maafisa wa Misri wakiufahamisha upande wa 'Israel' wa kutoupinga uvamizi wa kijeshi wa Rafah katika mji wa Rafah kwa sharti la kuepuka majeruhi ya raia wa Palestina.

Soma zaidi...

Al-Waqiyah TV: Kampeni “Inatosha Miaka 100 ya Unyonge!”

Katika mwezi wa Rajab Tukufu mwaka huu, 1445 H - 2024 M, inarudi kwetu kumbukumbu ya uchungu ya miaka 103 H na 100 M ya kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu na wahalifu wa Kiarabu na Kituruki, ambayo iliasisiwa na Bwana wa Mitume Muhammad (saw), na maswahaba zake watukufu (ra), na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu mwaka 1342 H, sawia na 03/03/1924 M, na ardhi iliyobarikiwa (Palestina) ilipotea kwa kupotea Imam ambaye ni ngao, Khalifa wa Waislamu ambaye kwaye wanapigana nyuma yake na kujihami..

Soma zaidi...

Kwa nini Rafah Inapigwa Mabomu na Kuzingirwa na Serikali ya Misri?!

Katika matangazo ya moja kwa moja kwenye Chaneli ya Al Jazeera mnamo Jumatatu asubuhi, Februari 12, 2024, msemaji wa Wizara ya Afya, Ashraf al-Qudra, alizungumza na Al Jazeera akielezea uharibifu uliotokea huko Rafah na nyumba zilizolipuliwa, ambazo zilikuwa zinakaliwa na wakaazi na watu waliohamishwa makao yao.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu