Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 565
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kujibu kwa takbira, tahlil, na uungaji mkono, pamoja na vyombo vya habari na uhamasishaji wa kisiasa, kisimamo kilifanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kutibua mpango wa kujitenga kwa Darfur kilifanyika mbele ya Msikiti Mkuu mjini Port Sudan. Waumini walikusanyika baada ya swala ya Ijumaa, 20 Rabi' al-Awwal 1447 H - 12 Septemba 2025 M, kwenye Msikiti Mkuu mjini Port Sudan kwa ajili ya kisimamo hicho ikiwa ni sehemu ya kampeni ya hizb kutibua mpango wa kujitenga kwa Darfur.
Mnamo Jumamosi, tarehe 6 Septemba, karibu watu 900 walikamatwa katika maandamano ya kuunga mkono Palestina jijini London. Walikuwa wakipinga kuendelea kwa mauaji ya halaiki na njaa kwa raia wasio na hatia mjini Gaza, pamoja na kupigwa marufuku kwa kundi la Palestine Action ambalo serikali ya Uingereza iliharamisha kuwa shirika la kigaidi mwezi Julai. Waliokamatwa ni pamoja na maaskofu, makasisi, walimu, madaktari, wahudumu wengine wa afya, na vizazi vya wahanga wa mauaji ya Holocaust pamoja na waandamanaji walemavu. Wengi walikuwa wazee – katika miaka yao ya 60, 70 na hata 80 – na walijumuisha mzee mmoja kipofu mwenye umri wa miaka 62 aliye katika kiti cha magurudumu.
Haishangazi kwa mtu yeyote anayefuatilia hali ya kisiasa nchini Sudan kujua kwamba vita hivi viliratibiwa na kusimamiwa na Marekani chafu na yenye nia mbaya ili kufanikisha ajenda yake na kuvunja nguvu za washindani wake wa Ulaya, hasa raia wanaoshirikiana na Uingereza. Vita hivi vinafadhiliwa na Amerika, ni mchezo wao uliolaaniwa. Ushahidi wa wazi zaidi ni kwamba taarifa kuhusu kurefusha vita ilitoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Blinken. Kurefushwa kwa vita hivi si kwa ajili ya utatuzi au kuhifadhi damu au kukomesha uharibifu ambao umeharibu nchi na watu wake; badala yake, ni mapambano ya nyuma na mbele na jaribio la kuweka maono ya kisiasa ambayo yanahakikisha na kuhifadhi maslahi ya Marekani nchini.
Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, tunafuraha kuwaalika ndugu zetu wanahabari, wanasiasa, na wale wenye hamu na masuala ya umma kuhudhuria mkutano na waandishi wa habari ambao msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan atazungumza, kwa kichwa: “Taarifa ya Miezi Mitatu na Ubwana Uliopotea”
Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia inaomboleza mmoja wa Mashababu wake, ndugu Salih bin Muhammad al-Shafrah, aliyefariki mnamo Jumamosi, tarehe ishirini na moja ya Rabi’ al-Awwal 1447 H sawia na 13/09/2025 M. Alikuwa miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika eneo la al-Qayrawān, ambaye alifanya kazi katika safu zake wakati wa zama zenye giza kuu za ukandamizaji na dhulma. Hakika alikuwa ameshikilia imara da‘wah yake, akijitolea katika kuibeba, akilingania Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, mwenye kuiamini ahadi ya Mola wake Mlezi na bishara njema ya Mtume wake Mtukufu (saw), mpaka alipofariki dunia. Hivyo ndivyo tunavyomhisabu, na wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.
Katikati ya milipuko ya mabomu na makombora ya umbile la Mayahudi, ikinyesha moto juu ya vichwa vya watu wetu mjini Gaza, ambapo wanalenga ghorofa za makaazi, vyuo vikuu, shule, hospitali na misikiti, hata kuangusha mahema chini, kiasi kwamba mifupa ya watoto na nyama zao inachanganyika na vifusi, “mkutano wa aibu na waovu” ulikusanyika na kufanywa. Ilikuwa ni mkutano wa kilele wa watawala Ruwaibidha duni, waovu kutoka miongoni mwa Waarabu na wasio Waarabu.
Kisimamo kilichofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan ili kufelisha mpango wa kuitenganisha Darfur kilipokelewa kwa maingiliano makubwa, ikiwemo takbir, tahlil, na kuungwa mkono, pamoja na uhamasishaji wa vyombo vya habari na wa kisiasa mbele ya msikiti mkuu katika mji wa Port Sudan. Waumini walikusanyika baada ya swala ya Ijumaa mnamo 20 Rabi' al-Awwal 1447 H 12 Septemba 2025 M kwenye Msikiti Mkuu wa Port Sudan katika kisimamo kilichofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan mbele ya Msikiti huo Mkuu kama sehemu ya kampeni ya Hizb kukwamisha mpango wa kuitenganisha Darfur.
Serikali ya mpito inaisaliti nchi kwa kuonyesha kusitasita kulinda Mipaka yetu kutoka kwa ‘Jeshi la Arakan’ linaloungwa mkono na Marekani, huku ikitamani kuwatumia wanajeshi wetu kwa Misheni ya Amerika nchini Ukraine. Kuanzia Disemba 2024 hadi Septemba 10, kundi la waasi lenye makao yake nchini Myanmar liliwateka nyara wavuvi 325 kutoka maeneo mengi kando ya Mto Naf na Ghuba ya Bengal. (bdnews24.com, Septemba 12, 2025). Kinaya ni kwamba, serikali ya Yunus ilipuuza Jeshi la Arakan (wakala wa Marekani) linalofanya kazi ndani ya ardhi yetu na kutishia watu wetu na ubwana wetu. Wakati huo huo, ilikuwa haraka kuisaidia Ukraine ili kumfurahisha bwana wake wa ubeberu mamboleo, Marekani.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, imeandaa kongamano la kisiasa la mtandaoni lenye kichwa “Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?” kutoa mwongozo kwa wananchi ili kufikia lengo kuu la Mapinduzi ya Julai 24. Munaalikwa kutazama kongamano hili ili kupata mwamko wa kisiasa na kuamua nini cha kufanya katika hatua hii ya kisiasa nchini.