Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Uhakika wa Misimamo ya Kimataifa na ya Kieneo Juu ya Vita vya Idlib

Serikali ya Syria imepeleka majeshi yake kusini mwa mkoa wa Idlib, na Urusi imetangaza kuwa tayari kupigana vita vya Idlib, “vita vikuu vya mwisho!” nchini Syria, na imefanya mazoezi ya kijeshi; makubwa zaidi kufanya katika historia yake ya hivi karibuni mashariki mwa bahari ya Mediterrania. 

Soma zaidi...

Kuanguka kwa Lira ya Uturuki

Kuanguka huku kumeongezeka baada ya Amerika kutoza ushuru wa forodha juu ya madini ya chuma na alumini yanayoagizwa kutoka Uturuki, ikiongezewa na kadhia ya kuwekwa kizuizini kwa mchungaji wa kidini wa Kiamerika nchini Uturuki tangu 2016, ambaye Amerika imetaka kuachiliwa kwake … ni sababu gani za yote haya? Na je, mgogoro huu waelekea wapi?

Soma zaidi...

Mradi Mpya Juu ya Syria

Yaliyotokea mjini Daraa kutokana na serikali kuyavamia kwa haraka maeneo yaliyo hamwa kwa miaka, na kufuatiwa na Quneitra na kabla ya hapo Ghouta na kabla yake Aleppo na dada zake, na macho yote sasa yanaelekea Idlib, hii inaonesha kuwa yapo mambo ambayo yanastahili kufanyiwa utafiti na utambuzi.

Soma zaidi...

Kampeni ya Hizb ut Tahrir Nchini Sweden: Tumia sauti yako, lakini sio katika uchaguzi!

Risala msingi ya kampeni hii imekuwa ni namna gani Waislamu wanavyo weza kuchangamka katika jamii pasi na kulegeza msimamo wa kitambulisho chao cha Kiislamu.  Kampeni hii na yaliyomo ndani yake imezungumziwa kwa hamu miongoni mwa Waislamu pamoja na mitandao ya kijamii. Imefaulu kuwasilisha barabara mtazamo wa Kiislamu na kuathiri mdahalo kuhusu uchaguzi nchini Sweden na harakati ya kisiasa ya Kiislamu. Kampeni hii pia iliifikia tanabahi kubwa ya vyombo vya habari na imekashifiwa kwa kufanya kazi dhidi ya demokrasia.

Soma zaidi...

Enyi Waislamu…Waokoeni Watoto wa Yemen!

Mnamo 21/11/2018, ripoti ya Shirika la Uingereza la Okoa Watoto ilisema kuwa takribani watoto 85,000 chini ya umri wa miaka mitano wamekufa kutokana na ukosefu wa lishe bora ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya vita ndani ya Yemen.  Idadi hii pekee ni sawa na jumla ya idadi ya watoto walioko chini ya miaka mitano ndani ya Birmingham, jiji la pili kubwa ndani ya Uingereza.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia Ilikuwa Mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Wanawake “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu”

Mnamo Jumamosi 27 Oktoba, kwa Baraka za Allah, Alhamdulillah, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa ushirikiano na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kwa ufanisi kilifanya kongamano kubwa na la kuvutia la kimataifa la wanawake jijini Tunis lenye kauli mbiu, “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu” ili kuelezea sababu na suluhisho la Kiislamu juu ya mgogoro unaoathiri utulivu na umoja wa ndoa na maisha ya familia katika jamii kote ulimwenguni, ikiwemo biladi za Waislamu. Tukio hili muhimu lilihudhuriwa na zaidi ya wanawake 250 kutoka kote nchini Tunisia wakiwemo mawakili, walimu, walezi wa watoto, wahandisi, wanafunzi wa vyuo vikuu, viongozi wa jamii, na watetezi wa vijana. Hotuba zilitolewa na wanachama wa kike wa Hizb ut Tahrir kutoka Tunisia, Uturuki, Ardhi Iliyo Barikiwa – Palestina, Pakistan, Lebanon, Indonesia, Ghuba la Kiarabu. Uholanzi, na Uingereza. Kongamano hilo vile vile lilipeperushwa moja kwa moja mtandaoni kwa washiriki wa kimataifa na kutazamwa na maelfu ya watazamaji kutoka katika pembe tofauti tofauti duniani. 

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu