Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  6 Safar 1442 Na: 1442/13
M.  Jumatano, 23 Septemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuifanya Gilgit-Baltistan kuwa Mkoa ni Khiyana Dhidi ya Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu, na Kuimarisha Mshiko wa Modi

Serikali ya Bajwa-Imran imepitiliza mipaka yote katika khiyana dhidi ya Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu. Baada ya kukataa kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu kupitia kuhamasisha jeshi lenye nia na uwezo la Pakistan, serikali hii ya mapuuza sasa imetangaza kuzikwa kwa kudumu kwa suala la Kashmir kwa kuhakikisha ugawaji wa pande mbili. Kwa lengo hili ovu, Jenerali Bajwa alifanya mkutano na uongozi wa kisiasa wa kidemokrasia ili kuifanya Gilgit-Baltistan iwe mkoa wa tano wa Pakistan, ikibadilisha Laini ya Udhibiti kuwa mpaka wa kudumu na kujisilimisha kwa madai ya Modi juu ya Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu kama sehemu muhimu ya India. Kabla ya mpango huu wa khiyana, hadhi tofauti ya kikatiba ilipewa Gilgit-Baltistan na Azad (Iliyokombolewa) Kashmir kutuma ujumbe wazi kwamba Kashmir yote, pamoja na Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu, ni jeraha lililo wazi katika upande wa Pakistan ambao hautawahi kufungwa hadi Kashmir yote iregeshwe katika mwili wake. Kuifanya Gilgit-Baltistan kuwa mkoa wa tano ni sawa na zawadi kwa Modi, iliyotolewa na serikali ya Bajwa-Imran kwa amri ya Amerika.

Kwa kufanya hivyo, utawala wa Bajwa-Imran unaasi waziwazi amri za Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) kupambana na wale wanaozikalia Ardhi za Waislamu, na kuwafukuza kiasi ya kwamba wasithubutu kurudi. Kwa kufanya hivyo, serikali imelikanyaga bila ya huruma fungamano lenye nguvu la udugu wa Kiislamu, ambalo limewalazimisha Waislamu wa Pakistan kupigana na India dhidi ya Kashmir kwa miongo kadhaa, wakitoa kafara watoto wao kwa hiari katika Jihad, huku wakiombea bendera ya Uislamu ipandishwe juu ya Srinagar. Kwa kweli, utawala huo umekuwa ukiwadanganya Waislamu tangu Modi alipoikamata kwa nguvu Kashmir mnamo 5 Agosti 2019. Kuanzia mwanzo kabisa, serikali ilishirikiana na Dola ya Kibaniani kwa amri ya Washington, ikilizika suala la Kashmir ili India iweze kupeleka tena vikosi vyake kuishughulikia China. Sasa, baada ya kuchukua hatua ya kuifanya Gilgit-Baltistan kuwa mkoa wa tano, usaliti huo unakaribia kukamilika, dhahiri kwa wote isipokuwa wale wanajitia upofu.

Enyi Waislamu wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan! Serikali ya Bajwa-Imran imetangaza wazi uungaji mkono wowote kwa silaha wa Waislamu wa Kashmir kama kitendo cha uadui na ugaidi, ukiwalazimisha kujisalimisha kwa kuwaacha vibaya. Uchokozi wa Modi wa 5 Agosti 2019 ilikuwa fursa ya dhahabu, iliyotolewa na Mwenyezi Mungu (swt), kwa kamanda yeyote mwenye ikhlasi wa jeshi kuvunja taya ya vikosi vya India vilivyochoka na vilivyo vunjwa moyo. Hata sasa fursa ya dhahabu ingalipo, kwani Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu inadai ukombozi, Amerika ni dhahiri inasita kupigana vita vya gharama kubwa eneo la Eurasia, dola za kikafiri zinakabiliana zenyewe kwa zenyewe na Dola ya Kibaniani inakabiliwa na shida kali ya kiuchumi katika historia yake. Hivyo basi, vipi huu utakuwa ni wakati wa kuisalimisha Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu kwa Modi? Imetosha sasa! Lazima muwakamate viongozi hawa wa khiyana, na kuwatupa kwenye jaa la historia huku mkitoa Nussrah kwa ajili ya kuregesha Khilafah kwa Njia ya Utume. Chukueni hatua sasa ya kujilinda na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) kwani nyinyi ni watu wenye nguvu, wenye uwezo kamili wa kung'oa utawala wa khiyana na uasi. Peaneni utii wenu kwa Khalifah ambaye atawaongozeni katika Jihad kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir Iliyokaliwa Kimabavu na Msikiti wa Al-Aqsa, mkitafuta radhi ya Mwenyezi Mungu (swt) na kupata mafanikio katika katika Dunia hii na Akhera ya milele. Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha,

(وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ)

“Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.” [Surah al-Baqarah 2:191].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu