Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  27 Muharram 1445 Na: 1445 / 05
M.  Jumatatu, 14 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

14 Agosti, Risala ya Siku ya Uhuru

Waislamu wa Pakistan, Bangladesh na Afghanistan Lazima Wasimamishe Khilafah ili Kuwaunganisha na Kukabiliana na Tishio Kubwa la Muungano wa Marekani na India

(Imetafsiriwa)

Baada ya kugawanya India mnamo 14 na 15 Agosti 1947, mamilioni ya Waislamu waliobaki nchini India sasa wanateseka sana chini ya kasumba ya dhehebu ya "Hindutva", ili Modi aweze kushinda uchaguzi. Mithili ya watawala wa Pakistan, watawala wa Bangladesh wanatabanni sera ya kujizuia hapo mbele ya, na kujisalimisha kwa, Dola ya Kibaniani. Lakini, sehemu nyingine iliyokandamizwa ya Ummah wa Kiisilamu, baada ya kugawanyika kwa India, Waislamu wa Burma, ni wahasiriwa wa ukatili mkubwa na Mabudha. Kama ilivyo kwa Pakistan, ambayo ina nguvu ya kutosha kutoa majibu yanayofaa kwa uchokozi wowote wa "Hindutva", sasa inaomba India kwa mazungumzo na kutangaza kuipeleka timu ya kriketi hadi India. Hii ni licha ya kuwa, baada ya kuunganishwa kwa nguvu kwa Kashmir inayokaliwa kwa mabavu na India mnamo Agosti 2019, Dola ya Kibaniani imeteka nyara karibu elfu kumi ya dada zetu wa Kiislamu. Sasa, kwa kuzingatia msaada mpana wa Marekani kwa serikali ya Modi, pamoja na utoaji wa silaha za kijeshi za hivi karibuni na kuunda tena mazingira ya kimkakati, Waislamu katika kanda hiyo hawana chaguo ila kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume. Hakika, ni kwa kusimamishwa tena Khilafah ndiko kutakakobadilisha siasa nzima ya kanda hii. Itahakikisha kwa mara nyengine tena kuinuka kwa Uislamu hadi katika kiwango cha utawala usiopingika, katika bara dogo la India, kama ilivyokuwa hali kwa karne nyingi, katika zama za Khilafah.

Urafiki wa Marekani-India ulipata uchangamfu kwa mkutano wa Clinton-Vajpayee mnamo Septemba 2000. Ulifika katika mpango kiraia wa nyuklia katika mkutano wa Bush-Manmohan mnamo Julai 2005. Sasa unazidi kugeuka kuwa uhusiano wa kimkakati, kwa mkutano wa Biden-Modi Mnamo Juni 2023. Mafungamano haya yamepanuka hadi ushirikiano wa injini za manuari, droni za kijeshi, akili bandia na silsila mbali mbali za usambazaji za Marekani. Kwa kushajiishwa na hili, Modi ameshambulia Waislamu nchini India na eneo hili. Marekani inatoa teknolojia yake ya hali ya juu kwa Dola ya Kibaniani kutumia kama silaha dhidi ya China na Waislamu katika eneo hili. China ndio tishio la sasa kwa Marekani, huku Waislamu katika eneo hili wakiwa na uwezo wa kuzipaza usingizi Washington na New Delhi, kupitia kusimamisha tena Khilafah. Ndio njia pekee ya kupindua mipango ya muungano wa Marekani-India.

Enyi Majeshi ya Pakistan! Ni kipi kitakacho onekana, pindi mtakapowapindua watawala hawa vibaraka na kuipa Nusrah Hizb ut Tahrir iliyojiandaa kikamilifu kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume ?! Amiri wa Hizb ut Tahrir, Sheikh Ata bin Khalil Abu al-Rashtah ataunganisha kwa ufanisi madhihirisho yote ya nguvu za dola, na kuunganisha kwa haraka Afghanistan, Asia ya Kati na Bangladesh ndani ya dola moja ya Khilafah. Khilafah itaunda athari kubwa ya fuatanishi, kupiti kuzipindua serikali za nchi zengine za Kiislamu katika eneo hili, na nje ya eneo hili, kupitia rasilimali za kisiasa, kiuchumi na kijeshi za dola kubwa, iliyozidishwa na nguvu kubwa ya kiroho ya Uislamu, Dini ya Haki. Itavunja mfumo huu wa wakoloni na kung’oa muundo huu wa ukandamizaji wa kibinadamu. Itapanua mara moja mamlaka ya Khalifa kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu. Khilafah, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), itaenea kwa haraka sana katika ulimwengu wa Kiislamu, kwamba watawala wa nchi za Kiarabu na zisizo za Kiarabu hawatapata wakati wa kukimbilia nchi za Magharibi, na mikoba yao iliyojaa.

Khilafah kwa Njia ya Utume itapigania ukombozi wa Palestina na Kashmir. Itachukua udhibiti wa njia kuu za kibiashara za ulimwengu, iwe ni mkondo wa Suez, Milango ya Bahari ya Malacca au ya Hormuz. Itaanzisha mfumo mpya wa Kiislamu, baada ya kuuzika mfumo wa sasa, fisadi wa kimataifa. Khilafah hii itakuwa ndio dola kubwa zaidi ulimwenguni. Itakuwa na rasilimali nyingi na idadi kubwa zaidi ya watu ulimwenguni. Majeshi na silaha zake na itakuwa na nguvu zaidi ulimwenguni. Zaidi ya yote, itakuwa na nguvu ya Iman kwa Mwenyezi Mungu (swt), ambayo inamzidi yeyote anayesubutu kuikabili.

Kwa hivyo, Enyi vikosi vya jeshi la Pakistan! Jitokezeni na mupate Nusra ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa damu, jasho na roho zenu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[لِيُحِقَّ الۡحَـقَّ وَيُبۡطِلَ الۡبَاطِلَ وَلَوۡ كَرِهَ الۡمُجۡرِمُوۡنَ]

“Ili ahakikishe Haki na auvunje upotovu na wangachukia wakosefu.” [Surah Al-Anfal 8:8].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu