Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  7 Rabi' I 1442 Na: 1442/01
M.  Jumamosi, 24 Oktoba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala wa Sudan Wanathibitisha Kumsaliti Kwao Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini kwa Kujiunga na Hadhira ya Usawazishaji Mahusiano, Kushirikiana na Makafiri, na Kuwakabidhi Ardhi Iliyobarikiwa!!

]سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِندَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ]

 “Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-An’am: 124]
(Imetafsiriwa)

Kwa kiburi chake cha kawaida, Rais wa Amerika Donald Trump alitangaza kwamba Sudan na umbile la Kiyahudi wamekubali kusawazisha mahusiano. Na aliikadiria hii kama hatua nyingine kubwa kuelekea kujenga amani katika Mashariki ya Kati na nchi nyingine ambayo inajiunga na makubaliano ya "Abraham". Maafisa wakuu wa Amerika walisema kwamba Rais wa Amerika alihitimisha makubaliano hayo kwa njia ya simu mnamo Ijumaa 10/23/2020 M pamoja na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi Benjamin Netanyahu, Mwenyekiti wa Baraza la Enzi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, na Waziri Mkuu Abdullah Hamdok. Trump alisema alitarajia kwamba Wapalestina na nchi nyingine nyingi watakubali uhusiano wa karibu na umbile la Kiyahudi katika miezi ijayo. Alisema kuwa angalau nchi 5 zengine zinataka kujiunga na makubaliano ya amani na umbile la Kiyahudi, na akaitaja haswa Saudi Arabia, akisema kwamba ana hakika kuwa itajiunga na bogi hili hivi karibuni.

Kwa upande wake, Netanyahu alijigamba juu ya makubaliano haya, akilichukulia tukio hili kuwa mapinduzi nchini Sudan! Na alikadiria kuwa Khartoum, ambayo ilikuwa mwenyeji wa Kongamano la Hapana Tatu mnamo 1967, leo inasema ndio kwa amani na umbile la Kiyahudi, ndio kwa majadiliano nalo, ndio kwa kusawazisha mahusiano nayo.

Ndio, ndivyo ilivyo, kwa urahisi, na kupitia tu maongezi ya simu, Trump anawaongoza watawala wa Sudan kwenye hadhira ya usawazishaji mahusiano, kama vile alivyofanya na watawala wa Imarati na Bahrain, na hata kutoa "habari njema!" za ridhaa ya watawala zaidi kujiunga na makubaliano haya ya kihalifu yanayoitwa "Abraham"!

Huyu Trump, hakika amewapeleka watawala wa Sudan katika makubaliano haya ili kufanikisha maslahi yake ya uchaguzi, kwani anatarajia kuwa makubaliano ya kusawazisha mahusiano na fidia iliyolipwa na watawala wa Sudan (mrabaha) kwa familia za Wamarekani (wahasiriwa) itaongeza nafasi zake za kushinda, pamoja na pigo la kimaadili ambalo Netanyahu aliimba ambalo limezifanya hapana tatu kudhibitiwa, kushindwa na kutelekezwa.

Wimbi hili la kusawazisha mahusiano ni sehemu ya mpango wa Trump, kwani unatoa njia mpya ya kisiasa ambayo idara ya Amerika inaifuata katika kushughulika na suala la Palestina, kwani inaitenganisha na masuala ya usawazishaji na ya kikanda ili liwe ni suala kwa Wapalestina pekee, wakitafuta kulichuja. Kama ambavyo inatumia pia serikali za Kiarabu kuweka shinikizo kwa watu wa Ardhi hii Iliyobarikiwa ili kuwatiisha kujisalimisha. Kwa upande wa upinzani wa Mamlaka ya Palestina na PLO kwa makubaliano haya, wao sio chochote isipokuwa ni chembe ya jivu ndani ya macho, kwani wao ni viongozi wa kwanza kusawazisha mahusiano na kuratibu usalama na umbile la Kiyahudi, na hata kufikia kiwango kikubwa ndani yake, kwani mkuu wao Abbas ameyafanya kuwa "matakatifu!"

Amerika hutumia usawazishaji huu wa mahusiano kama chombo cha kupambana na Umma wa Kiislamu na kuvunja moyo juhudi zake za kuregesha tena mamlaka yake na kusimamisha Khilafah yake, na kama chombo cha kumaliza kabisa kadhia ya Palestina.

Amerika inataka kuimaliza kadhia ya Palestina ili iweze kuanzisha miungano ya kikanda kati ya serikali za vibaraka na umbile la Kiyahudi chini ya majina anuwai, ambayo kwayo inakusudia kuimarisha udhibiti wake juu ya eneo hilo kwa ala za kieneo, kulioanisha umbile la Kiyahudi ndani ya eneo hilo kwa njia ya kimaumbile, na kuuzuia Umma kutokana na kusonga mbele barabara kwa ajili ya ukombozi kutokana na mshiko wake wa kikoloni, kwani inafuatilia harakati za ukombozi za watu wake na kukusanyika kwao pambizoni mwa Uislamu na hamu yao ya kusimamisha dola ambayo inawakilisha tishio la kistratejia kwa Amerika na ushawishi wake.

Hakika makubaliano ya usawazishaji mahusiano yaliyotiwa saini na watawala vibaraka ni tangazo la usaliti kwa kadhia ya Palestina na usaliti kwa Waislamu wote kama Umma mmoja bila ya watu, na ni kabla na baada ya kumsaliti Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw) na kuiharibu Ardhi Iliyobarikiwa.

Hakika watawala wa Sudan na watawala wengine wa Waislamu ambao ni dhaifu na wenye ubaguzi kwa maadui wa Umma huu hawawakilishi Waislamu na matarajio yao, na watu wa Ardhi Iliyobarikiwa wanatoa wito kwa Umma kukataa makubaliano haya na kutaharaki kuviondoa viti vya enzi vya madhalimu na kuhamasisha majeshi yake kuikomboa Masra ya Nabii wake (saw), na kuzifuta kurasa nyeusi zilizoandikwa na vibaraka hawa kwa matendo yao maovu.

Hakika kadhia ya Palestina haina suluhisho isipokuwa kwa kuikomboa, maazimio yote ya UN na makubaliano yote ya khiana yako chini ya miguu ya Umma, na sisi tunatoka katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, tunajadidisha wito wetu kwa majeshi ya ulinzi ya Umma huu na wanajeshi wake, kurudia urithi wa washindi na wakombozi, na kutokubali Palestina kuwa kadi ya kura ambayo Trump anacheza kamari kwayo, wala sadaka inayotolewa na watawala kwa wakoloni ili kuhifadhi viti vyao. Kwa hivyo vizazi vya Al-Faruq na Salah al-Din na wasimame mara moja na waite, "Enyi, Farasi wa Mwenyezi Mungu tembeeni, na msubiri bishara njema ya Pepo"; Bila hivi, Palestina na Umma mzima itabakia katika unyonge na fedheha hadi Mwenyezi Mungu atakapoubadilisha kwa watu wengine badala yao, kisha hawatakuwa kama wao. Basi harakisheni, kwani hakika ujumbe huu ni mkubwa na muda uliokadiriwa (Ajal) unakaribia.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ * وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa. * Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Anfaal: 24-25].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu