Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  11 Muharram 1443 Na: 1443 / 03
M.  Alhamisi, 19 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

            Kwa Jina la Kugawanya Mamlaka, Watawala wa Pakistan Wanajitahidi Kuokoa Muundo wa Dola ya Kikoloni ya Amerika nchini Afghanistan

(Imetafsiriwa)

Mkutano wa dharura wa Kamati ya Usalama wa Kitaifa ya Pakistan (BMT) uliofanyika mnamo 16 Agosti 2021, ikiongozwa na Imran Khan na kuhudhuriwa na mawaziri wa shirikisho na makamanda wa vikosi vya jeshi la Pakistan, kuhusu Afghanistan, kana kwamba uamuzi huru wa sera ya kigeni ulikuwa ufanywe. Lakini, tamko lililotolewa baada ya mkutano huo lilionyesha tu lile la Mwakilishi Maalum wa Amerika wa Afghanistan, Zalmay Khalilzad, lililotolewa mnamo 13 Agosti, baada ya mkutano wa mamlaka ya kimataifa huko Doha, Qatar, ambapo matakwa matano yalipelekwa kwa Taliban, ambayo mikopo ya kifedha na kutambuliwa kimataifa kunategemea. Matakwa haya yalikuwa kuundwa kwa serikali inayojumuisha kila mtu, serikali ya uwakilishi (demokrasia), kulinda haki za binadamu (Magharibi) kwa wanawake na walio wachache, kudhamini kwamba ardhi ya Afghanistan haitatumika dhidi ya nchi zengine na utiifu kwa sheria za kimataifa (ambazo kiasili zinahifadhi ubwana wa Magharibi). Washiriki wa mkutano wa Baraza la Usalama wa Kitaifa walithibitisha kwamba Pakistan "itaendelea kufanya kazi na jamii ya kimataifa na wadau wote wa Afghanistan kuwezesha suluhu ya kisiasa ya pamoja," wakiita kama "njia ya kusonga mbele" kwa ajili ya uwakilishi wa makabila yote ya Afghanistan. Uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan uliwasilisha matakwa hayo ya Amerika wao wenyewe, wakiwataka Taliban, "kuhakikisha kuwa ardhi ya Afghanistan haitumiki na kundi lolote la kigaidi dhidi ya nchi yoyote," wakati wao sio chochote ila wawezeshaji waajiriwa tu wa matarajio ya Magharibi. Hii ndio sababu pia, wakati upinzani wa Afghanistan ulikuwa ukiikomboa Kabul, uongozi wa Pakistan uliitishia Taliban kutoikomboa Kabul "kwa nguvu," huku wakiishinikiza Taliban kufanya mazungumzo na vibaraka wa Amerika na kushiriki kikamilifu katika ugawanyaji kamili wa mamlaka ndani ya Taghut ya Demokrasia.

Serikali ya Bajwa-Imran inajitahidi mchana na usiku kama mwezeshaji mwajiriwa Ikulu ya White House na Pentagon, kuokoa ushawishi wa Amerika katika eneo letu. Huu ndio wakati ambapo hitaji la zama hizi ni kubomoa uzio wa Durand Line, kukata laini za usambazaji za angani na ardhini za Amerika na kufunga vituo vya ujasusi katika misheni za kidiplomasia za Amerika, kama baadhi tu ya hatua muhimu za kuhakikisha kuwa Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati zinaweza kuungana kama dola moja ya Khilafah. Lakini, serikali ya Bajwa-Imran imejikita kupata maslahi ya mabwana zake makruseda, ambayo yako mbali sana na matakwa ya Waislamu wa Pakistan na vikosi vyao vya kijeshi. Serikali hii imesikitishwa na Amerika kuondoka Afghanistan, baada ya kuitisha mazungumzo wakati vikosi vya Amerika vilipokuwa kwa idadi kubwa, ili Taliban ikubali uwepo mkubwa wa Amerika. Kwa hakika, wenye ikhlasi na ufahamu anaweza kuona kuwa serikali ya Bajwa-Imran ndio nguzo yenye nguvu zaidi ya maslahi ya Amerika katika eneo hili. Ilikuwa ndio imani kamili ya Biden katika utiifu wa utawala wa Bajwa-Imran ambayo ilimruhusu kuondoa wanajeshi kutoka Afghanistan, akijua kwamba watawala wa Pakistan watarahisisha unasaji wa Taliban ndani ya mipaka ya mazungumzo yaliyoelekezwa na Amerika, mfumo wa kimataifa wa wakoloni na Uvumbuzi wa Magharibi wa mipaka thabiti ya dola ya kitaifa.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Matunda halisi ya kuikomboa Kabul kutoka kwa uvamizi wa Amerika yatakuja tu wakati Rawalpindi na Islamabad zitatakaswa kutokana na ushawishi wa Amerika wa kikoloni. Kuimaliza Amerika Raj mkoloni wa kikanda iko ndani ya uwezo wenu pamoja na ndani ya mzunguko wa matendo ambayo  Mwenyezi Mungu (swt) amewapa udhibiti kamili, ambayo kwayo mutaulizwa Siku ya Kiyama. Nyinyi ndio mnaoweza kubadilisha wimbi la historia kuelekea Uislamu, kama ilivyokuwa hapo awali. Hizb ut Tahrir chini ya Amiri wake wa kiulimwengu, Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah yuko tayari na mpango kamili, kwa hivyo toeni Nussrah yenu kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itaziunganisha kwa haraka dola zilizoko sasa chini ya Uisilamu, ikiasisi utawala wa Uislamu wa kiulimwenguni sasa, kama ilivyokuwa kwa karne nyingi hapo awali. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [إِنَّمَا ذَلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ]

“Hakika huyo ni Shet'ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.” [Surah Aali Imran, 3:175].

#Afghanistan             #Afganistan           أفغانستان#

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu