Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  16 Muharram 1443 Na: 1443 / 04
M.  Jumanne, 24 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala wa Pakistan Wanaishawishi Taliban ya Afghanistan katika Mtego wa Uhalali wa Kimataifa, Licha ya Kuwa Umeiumiza Pakistan Kisiasa na Kiuchumi

(Imetafsiriwa)

Mnamo 23 Agosti 2021, Mrengo wa Uenezi wa Nje wa Pakistan ulituma ujumbe wa tweet wa taarifa moja kutoka kwa Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Pakistan, Moeed Yusuf, ikisema, "Tumeweka wazi kabisa kuwa tuko pamoja na jamii ya kimataifa mahali inapokwenda." Hapo awali Jenerali Bajwa alisema, "Pakistan inatarajia kuwa Taliban itatimiza ahadi zilizotolewa kwa jamii ya kiulimwengu kuhusu wanawake na haki za binadamu." Kwa hivyo, watawala wa Pakistan wanajaribu kuokoa ushindi kwa Amerika na washirika wake wa Ulaya, baada ya kushindwa kwao kwa udhalilifu kwenye uwanja wa vita, kwa kuwashawishi Mujahidina wa Afghanistan katika mtego wa uhalali na kutambuliwa kimataifa.

Uhalali na utambuzi wa kimataifa ni mkakati wa wakoloni ambao unakusudia kulazimisha mfumo wa kiulimwengu wa Kimagharibi kama kipimo stahiki kwa dola zote, ili kusiwe na yeyote wa kuweza kupinga utawala wa kibepari. Ilipelekea Pakistan kusalimisha mito mitatu kwa India, na pia uharibifu wa IMF wa uchumi wa Pakistan. Ilipelekea msako wa Mujahidina huko Kashmir kwa zabuni ya FATF, na vile vile kumchukulia jasusi wa India Kulbhushun kama mgeni wa serikali, badala ya kumuua, kwa amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki. Ilipelekea ulegezaji usalama wetu wakati wa Vita dhidi ya Ugaidi, na pia kupeleka wanajeshi wetu katika kuhudumia misheni za UN, badala ya kuzikomboa Kashmir na Msikiti wa Al-Aqsa. Kwa kushikamana na agizo la kimataifa, watawala wa Pakistan hawakumfukuza Balozi wa Ufaransa, wakati Macron alipounga mkono mashambulizi kwa heshima ya Mtume (saw), huku wakiwazuia majeshi wetu wenye nia na uwezo, wakati Modi akiiunganisha Kashmir kwa nguvu mnamo 5 Agosti, 2019. Hata hivyo, licha ya wao wenyewe kupooza kisiasa na kiuchumi, watawala wa Pakistan wanawashawishi Mujahidina wa Afghanistan katika mtego ule ule wa mfumo wa kiulimwengu wa wakoloni.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Uislamu unafungamanisha uhalali na kutambuliwa kwa serikali kwa utabikishaji wa Shariah ya Kiislamu pekee. Uhalali wa Khalifah umefungamanishwa na ridhaa na chaguo la Ummah, kupitia mchakato wa Ba’yah. Ba’yah inapewa kwa sharti la Khalifah kutabikisha Uislamu, na badali ya Ummah unamtii. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) hakutafuta kuhalalisha mamlaka yake mjini Madinah kulingana na sheria za Warumi au Wafursi, dola kuu za ulimwengu za wakati huo. Badala yake (saw) alipindua mfumo wa kiulimwengu wa uliokuwepo kupitia upanuzi wa haraka kwa Jihad. Katika Khilafah, ubwana ni kwa Sheria ya Kiislamu, huku kumchagua Khalifah ni haki ya Waislamu. Uteuzi wa Khalifah mmoja ni wajibu kwa Waislamu wote, wakati Khalifah peke yake ndiye mwenye haki ya kutabanni sheria za Kiislamu. Kwa hivyo, watawala wa sasa ni waporaji wa mamlaka, mawakala wa wakoloni katika nchi zetu na hawana uhalali wowote uliojengwa juu ya Uislamu. Hakika, kuwaondoa watawala kama hawa na kumteua Khalifah muadilifu mahali pao ni wajibu kwa Waislamu wote.

Enyi Waislamu katika Jeshi la Pakistan! Amerika imekuwa mada ya kejeli na dhihaka, kwani inaiomba Taliban kuuachilie ubalozi wa Amerika, huku wakihangaika kwa haraka kuwahamisha raia na washirika wake waliokwama. Ni fursa nzuri kwenu kuwaondoa vibaraka wa Amerika walioko nchini Pakistan kutoka madarakani, na kuipa Nussrah yenu Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamishwa Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah ndiyo itakayounganisha Pakistan, Afghanistan, Asia ya Kati na ulimwengu wote wa Kiislamu kama dola moja, yenye nguvu, itakayopuuza maombi ya dola za kikruseda za Kimagharibi ya kuhifadhi dola za kitaifa ambazo zimetugawanya na kutudhoofisha kwa

[وَلَنۡ تَرۡضى عَنۡكَ الۡيَهُوۡدُ وَلَا النَّصارى حَتّٰى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمۡ‌ قُلۡ اِنَّ هُدَى اللّٰهِ هُوَ الۡهُدى‌]

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu.” [Al-Baqarah 2: 120]

#أفغانستان         #Afganistan         #Afghanistan

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu