Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  19 Muharram 1443 Na: 1443 / 05
M.  Ijumaa, 27 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pazeni Sauti kwa Ajili ya Kuachiliwa Huru kwa Muneeb ur Rehman kutokana na Utekaji Nyara. Kulingania Kwake Kuunganishwa kwa Ulimwengu wa Kiislamu Chini ya Khilafah, ni Wajib sio Uhalifu

(Imetafsiriwa)

Muneeb Ur Rehman, mtetezi wa Khilafah, alitekwa nyara mchana kweupe mnamo Ijumaa 20 Agosti 2021, kabla ya Swala ya Ijumaa, na mashirika ya ujasusi ya Pakistan. Muneeb ni baba wa kujitolea mwenye umri wa miaka thelathini na mbili wa binti wa miaka minne. Yeye ni mtoto mtiifu wa mama yake mgonjwa, ambaye anaugua maradhi ya Alzheimer, huku akiwa mjane mapema mwaka huu. Muneeb ni mtaalamu aliyejitolea na anayefanya kazi kwa bidii, akifanya kazi kama mshirika wa uuzaji katika kampuni moja mashuhuri, huku akiwa na shahada ya uzamili katika Utawala wa Umma. Lakini, watawala wa Pakistan walimteka nyara Muneeb, wakimdhulumu yeye na familia yake inayomtegemea, licha ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «اتَّقِ دَعْوَةَ الْمَظْلُومِ فَإِنَّهَا لَيْسَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ اللَّهِ حِجَابٌ» “Iogopeni dua ya mwenye kudhulumiwa, kwani haina pazia baina yake na Mwenyezi Mungu (swt).” [Bukhari].

Kwa kweli, Muneeb ametekwa nyara huku kukiwa na msako waa kitaifa dhidi ya wale wanaotetea utawala wa Kiislamu kwa eneo hilo, baada ya Amerika kujiondowa kwa udhalilifu kutoka Afghanistan. Msimamo wa Muneeb na maarufu kwa umma ulikuwa kwamba Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati, lazima ziunganishwe chini ya Khilafah kwa Njia ya Utume kama dola moja, yenye nguvu. Ambapo kamwe sio uhalifu, msimamo wa Muneeb ni msimamo unaolazimishwa kwa Waislamu wote na Dini ya Uislamu. Lakini, watawala wa Pakistan walimdhuru Muneeb, licha ya kuwa Mwenyezi Mungu (swt) alionya katika Hadeeth Qudsi, «مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ» “Yeyote anayemfanyia uadui Walii wangu nimetangaza vita dhidi yake.” [Bukhari].

Huku wakitoa kauli tupu ya Dola ya Madina, watawala wa Pakistan wametabanni msimamo mkali wa Maquraishi wa Makkah dhidi ya Dini yetu, kwa sababu wako upande wa Amerika. Badala ya kutafuta Khilafah wakati wa fursa hii ya kihistoria, watawala wa Pakistan wanaitaka Taliban kushiriki katika serikali ilioasisiwa na Amerika, wakigawanya mamlaka na mawakala na vibaraka wake. Badala ya kudai kuunganishwa kwa dola za Waislamu za eneo hili chini ya Khilafah, wanafanya kazi ya kuimarisha mipaka kati ya Waislamu, ukiwemo Mstari wa Durand, kama sehemu ya sera ya wakoloni ya gawanya utawale. Wakichukizwa na utiifu wetu kwa Uislamu na Waislamu, watawala wa Pakistan wamegeukia utekaji nyara ili kutulazimisha tukubali ushirikiano wao na Amerika. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَنْ يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ]

“Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.” [Surah Al-Barooj 85:8].

Enyi Waislamu wa Pakistan na Ndugu zao Wanasheria, Wanaharakati wa Haki za Binadamu na haswa Wanachuoni!

Kwa kweli tumebarikiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kumhisabu kijana Muneeb na wengineo wengi miongoni wenetu. Wamepaza sauti zao katika zama za madhalimu kwa niaba yetu, wakilingania kuabudiwa kwa Mwenyezi Mungu (swt) peke yake, bila kumwogopa yeyote ila Mwenyezi Mungu (swt). Lakini, huku tukipendezwa na msimamo wa wale mithili ya Muneeb, tusisahau kwamba lazima tuwaunge mkono wana kama hawa watiifu kama kadri tuwezavyo, tukishirikiane nao katika matatizo yao, huku tukiondoa matatizo yoyote yanayowapata katika njia yao tukufu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,  «مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ اَلدُّنْيَا, نَفَّسَ اَللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ اَلْقِيَامَةِ “Yeyote anayemuondolea muumini tatizo miongoni mwa matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamuondolea tatizo miongoni mwa matatizo ya Siku ya Kiyama.” [Muslim]. Hivyo basi wale wanaotamani Dini ya Uislamu na kuwaheshimu watetezi wake, na wapaze sauti!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu