Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  27 Safar 1443 Na: 1443 / 13
M.  Jumatatu, 04 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Majeraha ya Baluchistan Yahitaji Tiba ya Uislamu na Khilafah, Sio Kubughudhiwa na Nguvu za Serikali
(Imetafsiriwa)

Mnamo 2 Oktoba 2021, polisi walimpiga risasi na kumuua mtoto, Ramiz Khalil, wakati wa uvamizi wa nyumba katika mji wa Bulaida, Kech, eneo la Baluchistan. Familia yake ilifanya maandamano, na maiti hiyo ndogo, huko Fida Chowk, Turbat. Mapema, mnamo Septemba 21, katika tukio lingine huko Kech, bikizee, Taj Bibi, alipigwa risasi na kuuwawa karibu na kituo cha ukaguzi wa usalama. Hii sio mara ya kwanza kwa matukio kama hayo mabaya kutokea Baluchistan. Mauaji kinyume na sheria ya Hayat Baloch na vikosi vya usalama huko Turbat mnamo Agosti 2020 yalitikisa watu, kwani walimuona mama huyo aliye na huzuni akiinua mikono yake kuomba Dua, lakini haikuwa na athari yoyote kwa uongozi katili wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan! Baluchistan mwanzoni ilikuwa sehemu ya Ardhi za Kiislamu katika zama za Khaleefah Rashid, Umar al-Farooq (ra). Tangu wakati huo jimbo hilo limekuwa Waislamu wengi, huku, matakwa, hamasa na hisia za watu wake daima zimeshikamana na Uislamu. Pindi Usultani wa Delhi alipodhoofika na Ahmad Khan Abdali (Ahmad Shah Durrani) kulishinda jeshi la kikafiri la Maratha katika Vita vya Tatu vya Panipat, 1761, vikosi vyake viliimarishwa na Khan wa Kalat, Mir Naseer Noori, pamoja na jeshi la maelfu ya Mujahidina wa Baloch. Kwa hivyo ni sababu gani inayoifanya Baluchistan kuungua leo katika moto wa mapigano ya kikabila, baada ya urithi huu wa kifahari wa utiifu kwa Uislamu?

Leo, Uislamu peke yake ndio unaoweza kuunganisha vikundi anuwai vya kikabila na lugha nchini Pakistan, kwani makabila yaliyopigana ya Aws na Khazraj yaliunganishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Lakini, tangu kuanzishwa kwa Pakistan, kumekuwa na domo tupu pekee kuhusu udugu imara wa Uislamu. Badala ya kuunganisha kwa Uislamu, juhudi zilifanywa kuwaunganisha Waislamu wa Pakistan kupitia miundo ya kifederali, demokrasia ya kisekula na katiba, sheria na sera zisizokuwa za Kiislamu, katika jaribio la kuunda kitambulisho kipya cha kitaifa. Juhudi hizi ziliongeza tu mafuta kwenye moto wa uhasama. Maadui zetu wanaweza kutugawanya kwa urahisi, ikiwa ugomvi kama huo unazidi kuwa mbaya kutokana na uzembe, ufisadi, uonevu wa serikali na kunyimwa mahitaji ya kimsingi. Sera za kimabavu za operesheni za kijeshi, kupotezwa kwa nguvu kutekelezwa kwa mauaji kinyume cha sheria zimetufelisha kufikia kiwango vikosi vyetu vya usalama vimenaswa katika vita dhidi ya raia wetu wenyewe, "vikinyakua" eneo letu wenyewe. Machafuko yanayoendelea huko Baluchistan hakika hayana maslahi kwa vikosi vyetu vya usalama wala watu wa Baluchistan. Ikiwa serikali ya Bajwa-Imran inaweza kumwachilia huru rubani mshambuliaji wa India, Abhinandan Varthaman, kwa kisingizo cha "amani," basi ni kwa nini bado ingali inafuata kwa upofu sera ya Baloch ya farauni mwenye kiburi Musharraf ambaye alisema, "Wakati huu hamtaweza hata kujua kilichokupigeni.” Matumizi ya nguvu ya kibaguzi mwanzoni yalichochea na kueneza tu uasi mchache, kote Baluchistan.

Khilafah itamaliza muundo wa kifederali wa serikali, ambayo mikoa na maeneo machache hunyonywa. Khilafah itakomesha nidhamu ya demokrasia, ambapo haki za kisiasa na rasilimali zinasambazwa kwa msingi wa wengi. Khilafah itamaliza siasa zilizojengwa juu ya msingi wa utaifa na mgawanyiko wa kikabila, ikiwaunganisha Waislamu chini ya mamlaka ya Khaleefah mmoja, ndani ya udugu wa Uislamu. Khilafah itatabikisha Shariah na kuwapa Waislamu wote haki zilizotolewa na Qur'an Tukufu na Sunnah iliyobarikiwa. Ugavi wa rasilimali ndani ya Khilafah ni kwa mujibu wa amri zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) na sio kwa msingi wa wengi. Khilafah itakomesha ukandamizaji wa watu wa Baloch na itaiimarisha Baluchistan na Islamabad kwa njia ile ile, kupitia nidhamu yake wa umoja, ikiziunganisha nyoyo pamoja kama ndugu. Hivyo basi, enyi watu wa Nguvu na Uwezo, jitokezeni kuponya majeraha ya Ummah. Toeni Nusra kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, kuweka amani na usalama katika Baluchistan, Pakistan na Ulimwengu mzima wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلاَ تَفَرَّقُوا وَاذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنْتُمْ عَلَى شَفَا حُفْرَةٍ مِنْ النَّارِ فَأَنْقَذَكُمْ مِنْهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ]

“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.” [Surah Ali Imran, 3:103].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu