Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  5 Rabi' I 1443 Na: 1443/15
M.  Jumanne, 12 Oktoba 2021

Kumiliki Zana za Kinyuklia Kunathibitisha Uwezo wa Umma wa Kiislamu Kuhakikisha Kujitosheleza, kuwa Huru na Khilafah Imara

(Imetafsiriwa)

Kwa kumiminwa ghafla kwa rambirambi za dhati, Waislamu kote ulimwenguni wanaomboleza tangu Dkt. Abdul Qadeer Khan, mwanzilishi wa mpango wa nyuklia wa jeshi la Pakistan, alipotangulia katika Rehema ya Mola Wake (swt) mnamo 10 Oktoba 2021. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Surah al-Baqarah 2: 156]. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) ampe Dkt Abdul Qadeer msamaha wa kutosha, thawabu nyingi na makao ya juu Peponi. Ulikuwa ni uchangamfu wa Dkt Abdul Qadeer Khan na timu yake iliyojitolea ya wanasayansi na wahandisi ambao walipata uwezo wa nyuklia, kwa kufanya majaribio ya uchanganyaji baridi ndani ya kipindi kifupi cha miaka michache. Wamethibitisha barabara kwamba watoto mahiri wa Umma huu wa Kiislamu wana uwezo kamili wa kumiliki teknolojia ya kijeshi ya hivi karibuni, kwa msaada wa serikali, wakichochewa na hamu kubwa ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt).

Kwa rasilimali chache na vizuizi vingi, tumeunda mabomu ya nyuklia, MIRV, makombora ya masafa, droni, nyambizi na manuari. Hata hivyo, cha kusikitisha, uwezo wetu ulitumiwa na Kruseda Amerika kuikalia Afghanistan kwa miaka ishirini. Zaidi ya hayo, usaliti wa watawala wa Waislamu ulihakikisha misiba hiyo hiyo huko nchini Syria, Iraq, Myanmar (Burma), Turkestan Mashariki, Assam, Ardhi Iliyobarikiwa-Palestina na Kashmir, licha ya uwezo wetu. Hata hivyo, ni Khilafah ndiyo itakayoimarisha majeshi na teknolojia ya kijeshi ya Pakistan, Uturuki, Iran, Saudi Arabia, Misri, Algeria na Indonesia, ili kutugeuza kuwa jeshi lenye nguvu zaidi duniani. Hakika, chini ya uongozi wa dola yenye ruwaza ya Khilafah, tutaimarisha uwezo wa kijeshi mbali zaidi, ikiwemo teknolojia ya upekuzi, uhodari wa kubuni, mechatronics na hesabati za kompyuta, kumaliza utawala wa kijeshi wa dola za Magharibi, kupitia mfumo wao fisadi wa ulimwengu.

Mfumo huo wa kimataifa ambao umeundwa ili kuendeleza ubwana wa Magharibi, ambapo kamwe hatuwezi kuendelea kutokana na pingu za sheria za kimataifa za Magharibi na taasisi za wakoloni. Mpango wa nyuklia wa Pakistan wenyewe ni mfano wazi wa haja yetu ya kupuuza pingu za mfumo wa sasa wa ulimwengu, huku Washington ikiendelea kuitaka Pakistan iharibu makombora yake ya masafa marefu. Vivyo hivyo, kufikia uhuru wa kiuchumi hakuwezekani kupitia kuisujudia IMF na kukubali utawala wa dolari katika biashara ya kimataifa, huku uhuru wetu wa kisheria na kikatiba hauwezi kupatikana, bila ya kuipuuza jamii ya kimataifa, kama inavyoonekana kwa ndugu zetu katika harakati ya Taliban, ambao wanashinikizwa kuachana na Shariah, kupitia pingu za Mkataba wa Doha.

Matunda ya upinzani mdogo kwa mfumo kandamizi wa kimataifa wa Magharibi yanajumuisha mpango wa nyuklia wa Pakistan, mali yenye thamani kwa Ummah sasa na kwa Khilafah itakayosimamishwa hivi karibuni. Kwa hivyo itakuwaje wakati utawala wa kisheria, kiuchumi, kijamii, kisiasa na kijeshi wa Magharibi utakapopinduliwa, baada ya kusimamishwa tena kwa Khilafah? Khilafah itaunganisha Pakistan, Afghanistan, Asia ya Kati na kwengineko, kama dola inayojitosheleza yenyewe, yenye nguvu, inayotikisa ukumbi wa Eurasia na kulazimisha kuendelea kurudi nyuma kwa Amerika, huku ikihakikisha ukombozi wa Ardhi za Waislamu zinazokaliwa, ikiwemo Kashmir na Palestina. Kwa hivyo, Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Je! Humtatafuta heshima hii kwa ajili ya Mola wenu (swt), Ambaye roho zenu ziko mikononi mwake? Jitokezeni ili kusimamisha tena utawala na fahari ya Dini yetu kuu, Uislamu, kupitia kuipa Nussrah yenu Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ)

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Surah Muhammad 47:7].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu