Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  30 Rajab 1440 Na: 1440/45
M.  Jumapili, 07 Aprili 2019

Matakwa ya Kuachiliwa Huru kwa Mhandisi Naveed Butt, Mtetezi wa Khilafah, Ambaye Angali katika Utekaji Nyara tangu 11 Mei 2012

 (Imetafsiriwa)

11 Mei 2019 ni miaka saba tangu Mhandisi Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, alipotekwa nyara na maafisa wa usalama, mbele ya watoto wake na majirani. Katika miaka saba mirefu, Naveed hajaruhusiwa kuwasiliana na familia yake kwa vyovyote vile, hata mara moja, iwe kwa simu au ana kwa ana. Hakika, utekwaji nyara ni mateso ya hali ya juu, yenye kuiadhibu familia pamoja na muumini. Kwa yakini, ni dhambi kubwa kumtesa muumini anayelingania Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) bila ya huruma. Katika Hadith Qudsi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إِنَّ اللَّهَ قَالَ مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ»

“Hakika Mwenyezi Mungu amesema, yeyote atakayemdhuru Walii wangu basi nimekwisha tangaza vita naye” [Bukhari]. Lakini, huku ikidai utiifu kwa Dola ya Madina, serikali ya sasa inamzuilia Naveed katika utekaji nyara hadi leo, ingawa alifanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuregesha tena Uislamu kama mfumo kamili wa maisha. Lakini, huku ikidai kuwa "huru" na Amerika, serikali ya sasa inamzuilia Naveed katika utekaji nyara hivi sasa, ingawa kwa ujasiri alifichua mipango ya Amerika dhidi ya Waislamu wakati alipokuwa huru. Lakini, huku ikidai kuwa inajali "maslahi ya kitaifa," serikali ya sasa inaendelea kumweka Naveed katika utekaji nyara, ingawa hili ni kwa maslahi tu ya Kruseda Amerika na ujasusi wake wa kigaidi na jeshi la kibinafsi linalofanya kazi kwa uhuru nchini Pakistan mpaka leo. Hakika, katika enzi ya vita vya ulimwengu vya Amerika dhidi ya Waislamu na Uislamu, kuna rehema na huruma kwa rubani wa adui mshambuliaji wa Dola la Kibaniani, Abhinandan, lakini ukatili na utekaji nyara ni kwa mtetezi wa Khilafah, Naveed Butt. Hakika, ni serikali inayocukiza na ya uonevu inayopanua fungamano na usawazishaji kwa wale wanaoikalia Ardhi ya Waislamu, huku ikitumia nguvu na ukandamizaji dhidi ya wale wanaofanya kazi kwa dhati ili kusimamisha utawala wa Uislamu.  

Enyi Waislamu wa Pakistan! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إنَّ النَّاسَ إَذا رَأوُا الظَّالِمَ فَلمْ يَأْخُذُوا عَلى يَدَيْهِ أوْشَكَ أن يَعُمَّهُمُ اللَّهُ بعِقَاب»

“Hakika watu pindi wanapomuona dhalimu na wasimzuie mikono yake basi Mwenyezi Mungu atakaribia kuwachanganya wote kwa adhabu.” [Abu Dawud, Tirmidhi, ibn Majah]. Utekaji nyara unaoendelea wa Naveed ni uonevu mkali katikati yetu, ambao kwao tutahesabiwa na Mwenyezi Mungu (swt), kwa hivyo hatuwezi kukaa kimya. Ni wajibu kwetu kusema dhidi ya uhalifu huu, katika kila jukwaa linalopatikana kwetu, tukitaka kuachiliwa huru mara moja kwa Naveed. Kwa hivyo, Waislamu wote, haswa wale wanaomiliki nguvu na ushawishi, nawatafute rehema za Mwenyezi Mungu (swt) kupitia juhudi ya dhati na ya pamoja ya kumpa unafuu Naveed heshima inayostahiki, baada ya miaka saba migumu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ اَلدُّنْيَا، نَفَّسَ اَللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ اَلْقِيَامَةِ»

“Yeyote mwenye kumpa afueni muumini kutokana na mazito ya duniani, Mwenyezi Mungu atampa afueni kutokana na mazito miongoni mwa mazito ya Siku ya Kiyama.” [Muslim].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu