Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  5 Ramadan 1440 Na: 1440 /55
M.  Ijumaa, 10 Mei 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hakika Wamenyimwa, Watawala wasio na huruma wa Pakistan Wanadumisha Miaka Saba ya Utekaji Nyara ndani ya Ramadhan.

(Imetafsiriwa)

Mwezi wa ulioteremshwa Qur'an Tukufu, Ramadhan, unashuhudia kutekwa nyara kwa mja mwaminifu wa Mwenyezi Mungu (swt), aliyelingania hukmu kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Ramadhan hii, ni miaka saba tangu Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, alipotekwa nyara tarehe 11 Mei 2012, na maafisa wa usalama, mbele ya watoto wake na majirani zake. Na Ramadhan hii, watawala wa Pakistan wanamzuia Naveed kufuturu na familia yake, achilia mbali kuwajulisha juu ya ustawi wake, lakini, walimpa chai na kumwacha huru mapema rubani aliyekamatwa, mshambuliaji wa Dola ya Kibaniani, Abhinandan Varthaman. Je! rehema, huruma na unyenyekevu ni kwa adui wa Waislamu pekee na sio kwa yule alinganiaye Uislamu?!

Enyi Waislamu wa Pakistan na Maafisa wao wa Upelelezi haswa! Watawala wa Pakistan wanakataa kumwachilia huru Naveed, ingawa yule aliyenyimwa kheri ya Ramadhan, hakika amenyimwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إِنَّ هَذَا الشَّهْرَ قَدْ حَضَرَكُمْ وَفِيهِ لَيْلَةٌ خَيْرٌ مِنْ أَلْفِ شَهْرٍ مَنْ حُرِمَهَا فَقَدْ حُرِمَ الْخَيْرَ كُلَّهُ وَلاَ يُحْرَمُ خَيْرَهَا إِلاَّ مَحْرُومٌ»

“Hakika mwezi huu (Ramadhan) umewajieni, na ndani yake uko usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu moja. Yeyote atakayenyimwa basi amenyimwa kheri zote, na hakuna yeyote anayenyimwa kheri zake isipokuwa aliyenyimwa kabisa.’” [Ibn Majah]. Watawala wa Pakistan wanaendelea katika dhambi lao, ingawa Mwenyezi Mungu (swt) amerahisisha sana kuepukana na madhambi ndani ya Ramadhan. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إِذَا جَاءَ رَمَضَانُ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ النَّارِ وَصُفِّدَتِ الشَّيَاطِينُ»

“Pindi Ramadhan inapokuja, milango ya Pepo hufunguliwa na milango ya Moto hufungwa, na mashetani hufungwa minyororo.” [Bukhari]. Watawala wa Pakistan kwa jeuri wanamdhulumu Naveed, ingawa Mwenyezi Mungu (swt) hujibu Dua ya aliyefunga na aliyedhulumiwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«ثَلاَثَةٌ لاَ تُرَدُّ دَعْوَتُهُمُ الإِمَامُ الْعَادِلُ وَالصَّائِمُ حَتَّى يُفْطِرَ وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ يَرْفَعُهَا اللَّهُ دُونَ الْغَمَامِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَتُفْتَحُ لَهَا أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَيَقُولُ بِعِزَّتِي لأَنْصُرَنَّكِ وَلَوْ بَعْدَ حِينٍ»

“Watu watatu Dua yao hairegeshwi: Kiongozi mwadilifu, na aliyefunga mpaka afuturu, na dua ya aliyedhulumiwa Mwenyezi Mungu ataipandisha hadi mawinguni Siku ya Kiyama na itafunguliwa milango ya mbingu, na Mwenyezi Mungu atasema, 'Kwa Utukufu Wangu nitakunusuru (dhidi ya dhalimu) hata kama ni baada ya muda.’” [Ibn Majah]. Je! Haitoshi ukandamizaji wa muda mrefu, wenye dhambi kwetu angalau kuzungumza kwa manufaa ya kuachiliwa huru Naveed, ikiwa sio kupata kutolewa kwake halisi?! Na je! Sio juu ya watawala wa Pakistan kumwachilia huru mara moja Naveed Butt ili kuepusha hasira za Mwenyezi Mungu (swt) juu yao?! Mwenyezi Mungu (swt) ameonya,

 [إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَئِكَ فِي الأَذَلِّينَ]

“Hakika wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho.” [Surah Al-Mujadilah 58:20]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu