Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  30 Shawwal 1443 Na: 1443 / 67
M.  Jumatatu, 30 Mei 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Watawala wa Pakistan, Jihadharini! Umma wa Kiislamu Utawafanya Mfano Wale Wanaoanzisha Mahusiano na Uvamizi wa Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Akihutubia mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi la Dunia jijini Davos mnamo tarehe 26 Mei 2022, Isaac Herzog, rais wa umbile la Kiyahudi, alielezea furaha yake wakati wa ziara ya ujumbe wa Pakistan kwa uvamizi wa Mayahudi. Hapo awali, picha zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii za ziara ya Ahmad Qureshi, mtangazaji wa PTV inayomilikiwa na serikali ya Pakistan na mwakilishi maarufu wa uongozi wa kijeshi. Habari pia zilizuka mwezi Juni mwaka jana, kuhusu ziara ya siri ya Zulfiqar Bukhari, msaidizi maalum wa waziri mkuu wa zamani, Imran Khan. Baada ya usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi, na tawala za Kiarabu, sasa kuna ongezeko la mawasiliano kati ya uvamizi wa Kiyahudi na Pakistan.

Iwe ni utawala wa Bajwa-Imran au utawala wa Bajwa-Shahbaz, kuna utiifu kamili kwa amri za Marekani, kutokana na mfumo wa utumwa wa wakoloni ulioingizwa nchini kutoka nje. Hata hivyo, watawala nawatambue kwamba Ummah hautakubali chochote isipokuwa kuutokomeza kabisa uvamizi wa Kiyahudi. Al-Masjid Al-Aqsa na viunga vyake vimebarikiwa na Mwenyezi Mungu (swt), ambapo hakuna mamlaka yoyote ya kikafiri yenye haki ya kupata hata shubiri yake moja. Ni suala la muda tu kabla ya wale wanaopanua usawazishaji mahusiano na uvamizi wa Kiyahudi, chini ya shinikizo la Marekani, kupinduliwa.

Kwa hakika, maelezo ya Afisi ya Mambo ya Nje ya ziara ya hivi majuzi ya wajumbe wa Pakistan ni uongo mtupu juu ya dhambi iliyo wazi. Je, Shirika Lisilo la Kiserikali la kigeni linawezaje kuthubutu kuwatumia raia wa Pakistan kuanzisha mahusiano na umbile vamizi la Kiyahudi? Je, serikali ilichukua hatua gani dhidi ya watu hawa na mashirika yasiyo ya kiserikali juu ya kitendo hiki kiovu? Je, sauti zinawezaje kupazwa kwa niaba ya Pakistan kwa ajili ya kuugawanya Msikiri wa Al-Aqsa na suluhisho la dola mbili, wakati kila shubiri ya Palestina ni lazima ikombolewe? Je, sauti kama hizo zinawezaje kupazwa wakati wa mikutano ya Kiyahudi ya kitaifa, kusherehekea uvamizi na kutoa miito dhidi ya Waislamu?

Ni wazi kwamba uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan unasonga mbele katika usaliti wa Waislamu na Uislamu, kwa mapato duni ya kidunia. Uongozi wa Pakistan umetuma idadi kubwa ya pili ya wanajeshi kwa ajili ya zile zinazoitwa misheni za 'kulinda amani' za chombo cha Marekani, Umoja wa Mataifa, katika misheni 46 kote duniani, lakini haukusanyi wanajeshi katika Jihad kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir na Palestina! Watawala wa Pakistan sio tu kwamba wanaudanganya Ummah, wanakaribisha adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt). InshaAllah, Khilafah itakayosimamishwa hivi karibuni kwa Njia ya Utume itayahamasisha majeshi yenye nguvu ya Pakistan hatimaye kuzikomboa Ardhi zote za Waislamu kutokana na kukaliwa kimabavu, ili Waislamu waweze kupazaTakbira za ushindi huko Srinagar na Msikiti wa Al-Aqsa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu