Jumatatu, 11 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  8 Dhu al-Qi'dah 1360 Na: 1443 / 68
M.  Jumanne, 07 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Shutma na Ususiaji Vimeshindwa Kukomesha Msururu wa Kufuru, Hivyo Kwa Nini Tusichukue Hatua Kuelekea kwenye Suluhisho Halisi Sasa, Kusimamishwa Khilafah?

(Imetafsiriwa)

Msururu wa kufuru umeenea kutoka Denmark na Ufaransa, hadi sehemu nyingine za Ulaya na kisha Marekani. Sasa imeenea hata kwa washirikina Mabaniani duni. Heshima ya Mtume wetu kipenzi (saw) imekuwa chanzo cha kejeli za wazi. Leo, mwanamume au mwanamke yeyote duni anaweza kukufuru, kwa sababu hakuna Khalifa wa kulinda heshima ya Mtume wetu (saw). Awe mtawala wa kidemokrasia au dikteta, watawala wa sasa wa Waislamu kamwe sio walinzi wa heshima ya Mtume wetu (saw). Badala yake, wao ni walinzi wa mfumo wa kikoloni wa kiulimwengu, wa kisekula, ambao Ummah hauna uzito mbele yake, huku kukiwa hakuna utakatifu kwa dini yoyote, achilia mbali Uislamu. Watawala hawa watatoa tu shutma tupu kwa shinikizo la umma. Watavaa tu miwani za umaarufu; kama vile ishara duni dhidi ya chuki kwa Uislamu. Watajiondolea jukumu lao kwa kuzungumza kwenye vikao vya wakoloni, kama vile Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, kamwe hawachukua hatua yoyote thabiti. Katika zama za Khilafah, dola kuu za wakati huo zilizingatia na kufuru zilinyamazishwa. Hivyo, Khalifah Abdul Hameed II alizilazimisha Uingereza pamoja na Ufaransa kuinyamazisha kufuru, kutokana na tishio la Jihad la vikosi vya kijeshi vya Umma wa Kiislamu.

Bila ya Khilafah kama ngao, Raja Dahir Modi wa leo amekulia katika uadui. Aliinyakua Kashmir kwa mabavu, akatoa kifungo cha maisha kwa uongozi huko Kashmir na akasimamia ubomoaji wa masikiti. Aliwanyima mabinti wa Kiislamu haki ya kuvaa hijab, huku mahakama zake zikiwanyima Waislamu haki ya kutekeleza Dini yao. Kwa nini Modi asifanye hivyo, wakati Jenerali Bajwa na wafuasi wake, walio na jukumu la kumsitisha Modi, wanatembea mbele ya Modi kwa amri ya Marekani? Wanampa Modi zawadi ya kusitisha mapigano kwenye Mstari wa Udhibiti, huku jeshi lake likitikiswa na China. Wanazungumza juu ya kuongeza uhusiano wa kibiashara kupitia njia rasmi. Wanadumisha njia za siri za nyuma. Wanachukua sifa mbele ya mabwana zao wa Magharibi kwa kuwazuia Waislamu wa Pakistan dhidi ya India. Wanachukua hatua za kikatili kuwazuia Waislamu wasishawishiwe na fahamu za Jihad na Khilafah. Wananukuu uchumi dhaifu na haja ya uchumi wa kijiografia kuvunja moyo vikosi vya jeshi na kutupilia mbali hamu yao ya shahada na ushindi. Wanafanya hivyo ingawa Waislamu wa Pakistan wako tayari kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt), kuhuisha roho ya Vita vya Tabuk, huku wakiikomboa Kashmir nzima.

Enyi Maafisa wa Vikosi vya Wanajeshi wa Pakistan! Ulinzi kamili na wa kudumu wa heshima ya Mtume wetu unahitaji hatua chache tu kwenu. Toeni Nusra yenu kwa Hizb ut Tahrir sasa kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah ndiyo itakayonyamazisha ndimi na kuifunga mikono ya makafiri wenye kiburi. Wakati huo hata kuwaza kukufuru kwa bahati mbaya kutawapa jinamizi katika ndoto zao. Khilafah ndiyo itakayokuhamasisheni kwa ajili ya Ufunguzi wa Hind, na kukushajiisheni katika jitihada zenu za kutafuta shahada au ushindi, kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Khilafah ndiyo itakayochukua nafasi ya watawala hawa wanyakuzi na makamanda wa kijeshi, kwa makamanda na watawala wanaowapenda nyinyi, nanyi mnawapenda. Kwao hakuna kitakachokuwa muhimu zaidi kuliko utakatifu wa Waislamu, Dini ya Haki na Mtume (saw). Yote yanaweza kutokea ndani ya saa chache tu mikononi mwenu. Hakika ni mzigo mkubwa juu ya shingo zenu ambao inawapasa kuuheshimu, kwani mutahesabiwa kwa Mwenyezi Mungu (swt). Toeni Nussrah yenu sasa na mubadilishe maneno matupu, kwa Takbira za ushindi juu ya makafiri. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

 [وَمَا عَلَيْنَآ إِلَّا ٱلْبَلَٰغُ ٱلْمُبِينُ]

“Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi.” [Surah Yasin 36:17].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu