Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  26 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 1443 / 72
M.  Jumamosi, 25 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Khilafah Pekee Ndiyo Inayoweza Kutoa Afueni kutokana na Mfumko wa Bei, Kupitia Utoaji Sarafu ya Dhahabu na Fedha

(Imetafsiriwa)

Pakistan inahitaji suluhu iliyojaribiwa ili kuvunja mfumko wa bei, ambayo Uislamu hutoa kipekee. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliidhinisha uundaji wa dinar za dhahabu, zenye uzito wa 4.25g, na dirham za fedha, zenye uzito wa 2.975g, kama sarafu ya dola. Hivi ndivyo Khilafah ilivyohakikisha utulivu wa sarafu, na vivyo hivyo katika bei za bidhaa na huduma zinazonunuliwa na sarafu, kwa karne nyingi. Si urasilimali unaoporomoka, wala ukomunisti uliofeli, hutoa suluhisho lolote kwa mfumko wa bei uliokithiri ambao sarafu ya karatasi, isiyo na thamani ya dhati imesababisha. Bila shaka, mwaka baada ya mwaka, iwe ni Rupia ya Pakistan, dolari ya Marekani, ruble ya Urusi au Yuan ya China, sarafu ya isiyo na thamani ya dhati inapoteza thamani, na kuongeza bei za bidhaa na huduma zote. Hakika Khilafah ni hitajio la wakati.

Utoaji suluhisho la viraka kwa urasilimali unaokufa, au kujaribu kufufua ukomunisti uliokufa zamani, ni juhudi zisizo na maana za wanadamu. Kwa hakika, utabikishaji msingi wa Uislamu kupitia Khilafah sio pagao wala ndoto. Hapo awali, kwa karne nyingi, kwa kukua na kutawala kwa Khilafah, dinar ya dhahabu ilikuwa sarafu kuu inayotawala, kutoka pwani ya Magharibi ya Afrika, hadi kaskazini mwa India. Leo, kuregea kwa kiwango cha dhahabu na fedha kwa Waislamu ni jambo la kivitendo. Ardhi za Waislamu, ambazo dola ya Khilafah inatarajiwa kusimama hivi karibuni inshaa Allah, zina dhahabu na fedha nyingi, kama vile viwanja vya Saindaq na Reko Diq nchini Pakistan. Umma wa Kiislamu una rasilimali nyingi zinazohitajika na nchi nyingine, kama vile mafuta, gesi, makaa ya mawe, madini na bidhaa za kilimo, ambazo zinaweza kutumika kwa ubadilishanaji wa dhahabu na fedha zaidi. Kwa kuunganishwa chini ya Khilafah, Ardhi za Waislamu zitakusanya rasilimali zake nyingi na mbalimbali, zikijitosheleza kwa bidhaa za kimsingi, na kupunguza bili kutokana na uagiziji bidhaa nje. Uchumi halisi wa Khilafah utakuwa thabiti na unaostahimili ghilba na uvumi, mara tu uchumi wa vimelea wa vyombo vya riba vya kifedha utakapokomeshwa. Kwa kusimamisha tena dhahabu na fedha katika biashara ya kimataifa, Khilafah itamaliza faida ya kidhulma ambayo Amerika inayo, kwa kulazimisha dolari ya Kimarekani kwenye biashara ya kimataifa, kupitia chombo cha Washington, IMF.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Ipeni migongo yenu mifumo yote iliyotungwa na mwanadamu, iliyojengwa juu ya akili finyo na matamanio yasiyo na mwisho, na jitahidini kwa ajili ya hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Simamisheni Khilafah kwa Njia ya Utume, ili upate mafanikio katika Dunyah pamoja na Aakhira. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

 [وَأَنْ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Mai’dah 5:49].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu