Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  22 Rabi' II 1444 Na: 1444 / 16
M.  Jumatano, 16 Novemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Demokrasia na Mfumo wake wa Kiulimwengu ni Minyororo ya Utumwa wa Kimarekani

Simamisheni Tena Khilafah kwa Ajili ya Mabadiliko Halisi

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 27 Machi 2022, Imran Khan alifichua operesheni ya mabadiliko ya serikali kupitia njama ya Marekani kwenye mkutano wa hadhara, na akatangaza mapambano ya umma dhidi ya udhibiti wa Marekani juu ya Pakistan. Hata hivyo, katika muda wa miezi saba na nusu tu, Imran Khan alimaliza rasmi kampeni hii. Katika mahojiano na gazeti la Financial Times lililochapishwa mnamo Novemba 12, alisema, "Kwa mujibu wangu mimi mambo sasa kwisha, yote sasa yako nyuma yangu ... Uhusiano wetu na Marekani umekuwa ni uhusiano wa bwana na mtumishi, au uhusiano wa bwana na mtumwa, na tumetumiwa kama bunduki iliyokodiwa. Lakini kwa hilo nalaumu serikali zangu zaidi kuliko Marekani.”

Chini ya mfumo wa sasa wa kimataifa na Demokrasia, fahamu ya uhuru wa halisi haiwezekani kwa sababu ushawishi wa Amerika nchini Pakistan sio kupitia watu binafsi pekee. Ni kupitia serikali ya majimbo ya kidemokrasia na mfumo wa kiulimwengu ambao Pakistan inanyenyekeshwa. Hii ndiyo sababu, licha ya mabadiliko kadhaa ya watawala, ushawishi wa Marekani nchini Pakistan una nguvu na uko imara. Hakuna mtawala nchini Pakistan aliyejaribu kuiondoa Pakistan kutoka kwa mfumo huu wa kidemokrasia uliofeli, mfumo wa serikali ya majimbo na mfumo muovu wa kiulimwengu. Badala yake watawala wote hawa walichagua kuimarisha mshiko wa serikali ya majimbo ya kidemokrasia na mfumo wa kiulimwengu wa kikoloni.

Ni kutokana na utumwa wa mfumo wa kiulimwengu wa kikoloni, kwamba kuna hifadhi kubwa ya mafuta na gesi kwenye mipaka yetu, Iran na Asia ya Kati, lakini hofu ya vikwazo vya Marekani ni kubwa sana, kwamba watawala wetu wanaogopa kuchukua mafuta na gesi kutoka Iran na Asia ya Kati, licha ya uhaba wa mafuta na gesi nchini Pakistan.

Ni kutokana na utumwa wa mfumo wa kiulimwengu wa kikoloni, ambapo Pakistan na nchi nyingine za Kiislamu zinafanya biashara kati yao kwa dolari, wakati Uislamu umeamuru kutabanniwa kwa dhahabu na fedha kama sarafu, kwa ajili ya biashara ya ndani na ya kimataifa.

Ni kwa sababu ya utumwa wa mfumo wa kiulimwengu wa kikoloni, kwamba watawala wa Pakistan wanakataa kuhamasisha jeshi letu lililo tayari kujitolea, kwa ajili ukombozi wa Kashmir. Matokeo yake, India imeendesha vita vya ukandamizaji sio tu kwa Kashmir Inayokaliwa kimabavu, bali pia juu ya Waislamu wanaoishi ndani ya India.

Ni Demokrasia ambapo mwelekeo wa siasa, ni ndio mrefushaji wa viti, na nyadhifa za watawala. Katika Demokrasia, serikali inalinda tu maslahi ya watawala na kipote cha mabwenyenye. Katika Demokrasia, mfumo wa kiuchumi uliojengwa juu ya riba unaendelea, licha ya uharamu wazi katika Uislamu. Katika Demokrasia, sheria kama vile Sheria ya Waliobadili jinsia hupitishwa ili kuifurahisha Magharibi. Demokrasia inampa mwanadamu haki ya kutunga sheria, ambapo katika Uislamu, uwezo wa kutunga sheria upo kwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee.

Uhuru kutoka kwa thaqafa ya Kimagharibi, sheria za Magharibi na udhibiti wa kisiasa wa Magharibi hauwezekani hadi Waislamu wa Pakistan wajiondoe minyororo ya Demokrasia, mfumo wa serikali ya majimbo na utumwa wa mfumo wa kiulimwengu wa kikoloni.

Ni Khilafah pekee ndiyo itakayosimamisha hukmu kupitia Qur'an Tukufu na Sunnah za Mtume. Khilafah itamakinisha rasilimali za mafuta, gesi na madini za Waislamu chini ya mamlaka ya Khalifa, ili rasilimali hizi zitumike kwa Waislamu wote. Khilafah itaunganisha majeshi ya maeneo ya Waislamu na kuitoa Marekani nje ya Ardhi za Kiislamu. Khilafah itawakomboa Waislamu wa Kashmir, Palestina, India na Turkestan Mashariki (Xinjiang). Khilafah itabeba Dawah ya Uislamu kwa ulimwengu mzima kupitia Jihad.

Khilafah pekee ndiyo inayotoa ruwaza na ramani ya utendakazi kwa ajili ya uhuru wa kweli. Kwa hivyo, Enyi Watu Wenye Nguvu, jitokezeni na mtoe Nussrah kwa ajili ya kusimamisha Khilafah ili kuifanya ruwaza hii kuwa uhalisia!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu