Alhamisi, 02 Rajab 1446 | 2025/01/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  27 Jumada I 1444 Na: 1444 / 20
M.  Jumatano, 21 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Migawanyiko ya Mipaka Inayopuuza Mafungamano ya Kina ya Kitamaduni na Kihistoria, Inaweza Tu Kuchochea Taharuki ya Mipaka

Suluhu ya Kudumu ni Kuwaunganisha Waislamu, Waliogawanywa kwa Mipaka, Chini ya Uongozi Mmoja wa Kisiasa wa Kiislamu, Khilafah

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 19 Disemba 2022, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Ned Price, alisema katika taarifa, "Tuko tayari kusaidia, iwe kwa hali hii inayojitokeza au kwa upana zaidi." Ingawa Waislamu wa Pakistan wamekuwa wakiteseka kutokana na "msaada" wa Marekani kwa miaka 75, baadhi ya watunga sera na jumuiya ya kimkakati ya Pakistan bado wanalitazama "tatizo la Afghanistan" kwa mtazamo wa Kimagharibi, ambao hauwezi kutoa suluhisho la kudumu. Watunga sera wa Pakistan wamejaribu kila suluhisho linalowezekana, ikiwemo matumizi ya nguvu, kutoka kwa mtazamo Kimagharibi wa dola za kitaifa, kwa kuzingatia mpaka uliochorwa na Waingereza kama mstari uliowekwa kwenye jiwe. Hata hivyo, suluhisho pekee endelevu la tatizo hili ni kuunganisha Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati chini ya mamlaka moja ya Kiislamu (Khilafah), ambayo itakuwa ndio nukta kianzilishi ya kuunganisha Umma mzima!

Kuna sababu mbili kuu za mvutano kwenye mpaka wa Pakistan na Afghanistan:

Kwanza, jaribio la kuimarisha Mstari wa Durand, uliochorwa na Waingereza, huku wakipuuza uhusiano wa kihistoria wa karne nyingi kati ya Pakistan na Afghanistan, ikijumuisha Uislamu, rangi, jografia, mila, lugha, desturi, tabia, kutegemeana, mashujaa wa pande zote na mafungamano ya kifamilia. Ndiyo maana uongozi wa sasa wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan umeweka mahitaji ya hati, na mfumo wa kibayometriki, katika vivuko vyote vitano vya mpakani. Unahujumu mafungamano kati ya mataifa hayo mawili, kwa kuweka uzio wa thamani ya mabilioni ya rupia, na kupeleka wanajeshi kwenye mamia ya kilomita ya mpaka ulioundwa na wakoloni.

Pili, ni hamu ya Marekani kwamba vikosi vya jeshi la Pakistan kamwe visihamasishwe, kutoka mpaka wa magharibi hadi mpaka wa mashariki. Hii ni ili Dola ya Kibaniani ipate afueni kutokana na kukabiliana na vikosi vya Pakistan, na badala yake iweze kushughulika na China. Ni kwa sababu hii kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini kwenye Mstari wa Udhibiti mwaka wa 2020. Juu ya hili, uongozi wa Pakistan umekuwa ukiongeza shinikizo kwa serikali ya Afghanistan, ili kukuza ajenda ya kiliberali ya kisekula nchini Afghanistan, kwa amri ya Magharibi. Hii ni pamoja na kujumuishwa kwa vibaraka wa Marekani ndani ya miundombinu ya serikali, utekelezaji wa ajenda ya kiliberali ya Magharibi na wito wa kukandamiza makundi yenye silaha. Mivutano ya sasa na matokeo ya umwagaji damu ya Waislamu, ni matokeo ya moja kwa moja ya sababu hizi.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan, Enyi Jumuiya ya Kimkakati! Marekani haikuweza kudhibiti Afghanistan kwa nguvu. Hatuwezi kudhibiti Balochistan na maeneo ya kikabila ya FATA kwa nguvu. Machafuko hayo yamezimwa kwa muda tu, kutoka kizazi hadi kizazi, lakini hurudi tena kwa nguvu zaidi. Waislamu wote, wa rangi zote, watatulizwa tu baada ya utiifu kwa mamlaka halisi ya kisiasa ya Kiislamu. Kataeni ajenda na amri za Magharibi. Unganisheni Pakistan na Afghanistan chini ya Khilafah kwa ajenda ya Kiislamu. Ni Khilafah ndiyo itakayoleta pamoja Ummah mzima, unaoanzia nje ya Asia ya Kati hadi nje ya Ghuba, chini ya dola moja na Khalifa mmoja. Khilafah ndiyo itakayoizunguka Dola ya Kibaniani kutoka kila upande. Kisha hapo hamtaikomboa Kashmir pekee, bali pia India kutoka kwa ukandamizaji wa ukafiri. Tunakulinganieni mutimize wajibu wa kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Kwa hivyo, ni nani kati yenu atakayechukua njia hii ya heshima na adhama? Msiogope yeyote ila Yule Ambaye nafsi yenu imo Mikononi Mwake. Hakika Mwenyezi Mungu (swt) atakuwa Msaidizi na Mwenye kuwanusuru.

[وَاللّٰهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكۡثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Surah Yusuf: 21].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu